Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, August 30, 2022

MORO VETERAN KUTINGA DAR KIBABE

   Mwandishi wa Mtandao huu akitinga mazoezi leo na ndinga yake

 

MAZOEZI NI AFYA.

Leo Agost 30 majira ya saa 11 jion mchezaji tegemo wa timu ya Moro Veterani Dunstan Shekidele’Mkude Simba’aliwasili uwanja wa Shujaa na usafiri wake wa baiskeri a.k.a ‘Anita’unaomilikiwa na tawi kuu la Simba la Mkoani Morogoro, kufanya  mazoezi na timu hiyo kabambe mkoani Morogoro.

 

Kwa sasa timu hiyo ya Morogoro Veterani inajianda na na Safari ya jijini Dar kwenye bonanza litakarofanyika mwishoni Mwa wiki hii.

 

 lfahamike kwa sasa Moro Veterani inayoundwa na wachezaji wengi maarufu nchini akiwemo tajiri Aziz Abood ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Arbet Msando, Maprofesa wa vyuo Vikuu vya Mkoani Morogoro wakiongozwa na Profesa Madundo Mtambo, Maafande wa Majeshi ya Polisi ,JWTZ na Magereza.

 

Wengine ni wachezaji nyota wa zamani wa Simba na Yanga, akiwemo Ramadhan Kichuya baba mzazi wa Shiza Kichuya na Hamis Kidingile ambaye ni baba mzazi wa beki Hassan Kessy.

Awari  Moro Veteran walikuwa wakifanya mazoezi  viwanja vya hospital ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro vilivyopo jirani kabisa na chumba cha kuhifadhia maiti’Mochori’,

 

Kwa sasa Uongozi wa hospital hiyo umeamua kuongeza majengo kwenye eneo hilo hivyo tumelazimika kuutumia uwanja wa Shujaa uliopo Mji Mpya ambapo Vijana wa timu za Shujaa Under 10,Under 17 na Under 20 zinazomilikiwa na tawi la Simba wanaanza mazoezi saa 9 alasri na kumaliza saa 11 jioni.

 

 Wanawapisha Moro Veteran wanaoza mazoezi muda huo wa saa 11 mpaka saa moja kasoro usiku.

UTANI WA JADI,KWENYE DRAFT KIJANA AMPA ADHABU YA KUBEBA JIWE MZEE WAKE.



 


             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kijana mmoja Mfanyabiashara Maarufu wa Mitumba Mkoani Morogoro Jose Matei’Maarufu ‘Juto Mitumba’amempa adhabu ya kubeba jiwe, Salum Said Maarufu Mzee Kipese’baada ya kumfunga bao 6-0 kwenye mchezo wa Draft.

 

Tukio hilo lililojaza watu wengi limetokea hivi karibuni kwenye Soko la Nguo Maarufu Mnada wa Saba saba uliopo Kata ya Saba saba Manispaa ya Morogoro,ambapo wawili hao walikubaliana kwele ya ushahidi wawatu kwamba wacheze Draft  sharti la  atakayenza kufungwa bao 1 atapewa adhabu ya kubeba jiwe huku anacheza mchezo huo kwa mkono mmoja mpaka atakapo komboa bao hilo.

 

Hivyo walipoanza Mzee Kipesa alifungwa bao moja na Juto  katafuta jiwe kubwa na kumbebasha Mzee huyo bila huruma, Mzee kipese alijipapatua kurejesha bao hilo  bila mafanikio na kujikuta akiongezwa mabao mengine 5,uzito ulivyozidi dingi huyo alitupa jiwe hilo na kuondoka zake huku Vijana wakimsindikiza na maneno ya utani.

 

 Mzee Kipese aliwajibu kwamba anakwenda kula ugari kwa mkewe akirejea atakuwa na nguvu na akili Mpya.

 

”Huyu Majuto hana uwezo  kanifunga kwa sababu ya uchovu na Njaa bibi yeni kanitumia meseji ugari ukotayari ngoja nikale nikirudi nitalipa kisasi cha kumbebesha jiwe Majuto”alisema Mzee Kipese huku akiondoka zake.

 

Alipohojiwa na Mtandao huu Mzee Kipese alikiri kufungwa kasha kibabeshwa jiwe na Majuto.

 

Kwa upande wake Majuto anayemiliki banda la Mitunda katikati ya Mji wa Morogoro jirani na Ofisi kuu za kampuni ya Mabasi ya Abood alisema uwezo wake kwenye mchezo huo ni wakiwango cha juu.

Sunday, August 28, 2022

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA









 


Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele. 

Kama kawaida mtumishi wako kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.
 
Miongoni mwa jumbe jizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU.
Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto. 
 

Saturday, August 27, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU WANADAMU WENGI WANAPOTAKA KUONA AU KUOLEWA WANATANGULIZA TAMAA MBELE.


 


 

MITHALI 31-10.

 

 “Mke Mwema ni Nani awezaye kumwona? Maana Kima Chake Cha Pita Kima Cha Marijani”

 

1.SAMWELI .16-7.

 

”Lakini Bwana akamwambia Samweli,Usimtazame Uso wake,wala urefu wa Kimo Chake,Kwa Maana Mimi nimemkataa,Bwana hangalii Kama binadamu aangaliavyo,Maana binadamu utazama sura ya nje, bali Bwana hutazama  Moyo.”

 

Somo letu la leo Jumapili ya Mwisho ya Mwezi wa 8 linatuongoza kumjua  Mke au Mume Mwema.

 

Baadhi ya wanadamu wa kizazi hiki cha kidigital cha kuanzia miaka ya 80 mpaka 2022 tunapoingia kwenye mchakato wa kutafuta mke au mume tunavipa kipaumbele vigezo vya matamanio ya nje na si ya ndani Kwa maana ya Moyo na tabia njema za mtu.

Wanandoa hao wanapotaka kuingia kwenye ndoa hutafuna hutangulia tama za Mwili na Mali,kama vile  Shepu, Sura,Mali, Madaraka au Cheo, huku tukikipa kisogo kigezo Mama cha moyo safi na tabia njema.

 

 Hali hiyo ndiyo inayotajwa kuwa chanzo cha ndoa nyingi cha kizazi hicho cha kutoka miaka ya 80 mpaka mwaka huu 2022 tofauti na ndoa za wazee wetu ambao ndoza zao hudumu mpaka mmoja wao anapotangulia mbele za haki’wanazikana’.

 

Kuna siku nilistuka sana baada ya kusikia taasisi moja ikitoa takwimu kwamba kwa mwaka jana pekee talaka mia tano[500] zimetolewa kwa maana ndoa 500 zimevunjika.

 

 lkumbukwe kuna dini nyingine ndoa zao zikifungwa hakuna kipengere cha kupeana taraka sasa huenda idadi hiyo ya taraka 500 ndoa hizo hazijajumuishwa ingawa huko Mtaani tunashuhudia  wanandoa hao wengi wao wameshabwagana kitambo.

 

 Kwa sasa wanaume wengi  wanapotaka kuoa wanatafuta mwanamke mrembo mwenye shepu, rangi iliyokorea wengine wanafika mbali zaidi wanasaka mwanamke mwenye jina kubwa mjini ili naweze kuwatambia marafiki zake kwamba ameoa mwanamke Super Star Mjini.

 

Hali kama hiyo pia iko kwa wanawake,  wao vigevyo vyoa vikuu ni kutafuta mwanaume mwenye Pesa, au Mali Kwa maana ya nyumba na Magari hawaangalia tabia njema na moyo safi wa mwanaume atakaye kuwa baba bora wa watoto zake au Mama bora wa familia yako.

 

lnafaida gain unaolewa na mwanaume mwenye Pesa na Mali mwisho wa siku anakuwa sio baba bora wa watoto wako kila siku anarejea nyumbani 8 usiku akiwa amerewa.

 

Hana hata muda wa kuketi na familia yake kupanga Maisha  nyakati za jioni baada ya kumaliza kazi.

 

Mwisho wa siku huyo mwanaume akifirisika ndoa inavunjika kwa sababu ulichofuata hakipo tena,.

 

 Hakika ukitafuta mwanaume mwenye tabia njema na moyo safi hutakumbana na kadhia hiyo kila siku ndoa yenu itakuwa mpya.

 

Najua kwenye ndoa sio peponi kwamba ukiingia utakutana na furaha ya Milele hapana,kuna changamoto zake kwa sababu binadamu sio mkamilifu kama Malaika, hivyo nawasihi na kuisihi nafsi yangu tubebeane Misalama ya changamoto zetu ili tufike kwenye ile nchi ya ahadi tunayoitamani.

 

Kwa kizasi hiki cha kuanzia miaka hiyo ya 80-2022 natoa Kongore kwa wanandoa wote ambao mpaka sasa ndoa yao inaumri wa kuanzia miaka 5 na kuendelea hongereni sana na Mungu aendelee kuibariki ndoa hiyo.

 Ushauri kwa wale wanaohitaji kuingia kwenye ndoa na wale wanaohitaji kuinge  tena kwenye ndoa  baada  ya ndoa zao za awari kuvunjika kwa  kamwe usimtafute mwenzi wako kwa tama za Sura, Shepu au Mali mshirikishe Mungu na kigezo chako kiwemo tabia njema na Moyo safi mwengine yatapatikana kwa juhudi zenu kwenye mipango yenu ya kimaisha.

 

Kwa leo mtumishi wako naishia hapa tukutane Jumapili ijayo kwa uchambuzi mwingine wa neno la Mungu.

Amani ya Mwenyezi Mungu na iwe Juu yenu wote tuseme Amen’

SEHEMU YA PILI STORI BODA BODA KUDAIWA KUFUMANIWA NA DADA WA KAZI.


 


          Na Mdakuzi Dunstan Shekidele.Morogoro.

 

 STORI hii ya fumani ya boda boda kudaiwa kufumaniwa na dada wa Kazi chumbani kwa bosi wake Kihonda Maghorofani Mkoani hapa,ilianza kuripotiwa jana kwenye Mtandao Pendwa wa Shekidele.

 

Stori hiyo iliishia sehemu tamu ya Mmiliki wa nyumba hiyo Mwanadada Mrembo kutonywa na Majirani zake na kuludi fasta nyumbani akitokea kazini kwa lengo la kuwafumani Wapenzi hao waliogeuza ‘geto’ nyumba yake alipofika hapo nini kiliendelea  twende pamoja kumalizia stori hii.

 

Mrembo huyo baada ya kufika nyumbani akiwa na gari lake la kisasa nje ya Mjengo wake wa kifahari alikuta boda boda mpya imepack alishuka kwenye ndinga yake  kazama ndani kwa lengo la kuwafumania wapenzi hao kwa lengo la kukomesha mchezo huo mchafu unaofanyika nyumbani kwake bila ridhaa yake. 

 

Dili limebuma House Girl huyo baada ya kusikia mngurumo wa gari la bosi wake ambao kimsingi anaufahamu vizuri, fasta kumfungulia boda boda huyo mlango wa nyuma,katimua mbio kama zile za swala anayekimbizwa na chita’Chui’kaiacha boda boda yake pamoja na kofia ngumu’Herment’ kwenye moja ya Masofa yaliyopo kwenye sebreni ya Mjengo huo.

 

Mmiliki wa  nyumba hiyo zlipzama ndani alianza kumtafuta boda boda huyo maeneo yote ya nyumba hiyo bila mafanikio,  alipoingia chumbani alikuta shuka za kitandani zimekunyamana kama vile zilitafunwa na Ng’ombe kisha zikatemwa.

 

Big boss huyo wa Mjengo huyo baada ya kumkosa boda boda huyo alimvaa house girl, alipoulizwa alikosa majibu sahihi kutokana na ushahidi wa Pikipiki, Herment na kule chumbani ushahidi wa kuvulugika kwa akitanda kwa ushahidi huo dada huyo wa kazi hakuwa na jibu lingine  zaidi ya kukubali kosa na kumuomba msamaha bosi wake.

 

House Girl huyo baada ya kukubali kosa hilo la kumwingiza boda boda chumbani na kushirikiana naye kuivunja amri ya 6 ya Mwenyezi Mungu ya Usizini,Mmiliki huyo wa mjengo aliamua kuichukua boda boda hiyo na kuifungia ndani akihitaji kulipwa kiasi cha pesa akidai  kwa  siku nyingi vitu vyake zilikuwa vikiibiwa ndani kwa ushahidi huo anaamini mwizi wake ni boda boda huyo hivyo kamua kuikamata Pikipiki hiyo mpaka alipwe laki tano.

 

Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mdakuzi ulibaini boda boda huyo alipewa Pikipiki hiyo na bosi wake kwa mkataba wa kila siku kukusanya elfu 10 na pesa hiyo walikubaliana kuikabidhi kwa wiki elfu 70.

 

Utamu unakuja hadi jana ljumaa habari hii inakwenda hewani ni takribani siku 5 hivyo bado siku 2 boda boda huyo kuhitajika kupeleka kipande cha elfu 70 kwa tajiri yake huku boda boda hiyo iking’ang’aniwa na ‘Mother House’ huyo.

 

 Baadhi ya marafiki wa boda boda huyo walimshauri amtafute Mzee mwenye busara  waendele kwa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa lilipotokea tukio hilo wakamuombe Msamaha dada huyo ili amludishie  Pikipiki yake aendelee na ajira yake.

 

lnadaiwa boda boda huyo mwenye jina la Moja ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa anaogopa kufanya hivyo akihisia majanga yanaweza kuwa makubwa zaidi akihofia huenda akakamatwa na kupelekwa Polisi.

 

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani’Mei Mosi’ yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma Mwaka huu  Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hotuba yake alisema Wafanyakazi wa ndani wanahaki kama wafanyakazi wengine.

 

Wakistahili kupata huduma zote kama wafanyakazi wengine ikiwemo yakuutengewa chumbani na bosi wake endapo akitokea house Girl akipata mchumba aweze kuishi naye  kwenye nyumba hiyo  bila bughoza yoyote.

 

 Kauli hiyo ya Mpendwa Rais wetu Mama Samia iliyobeba zana kuu ya kuwatetea wafanyakazi hao wa ndani, iliamsha vicheko kwa umati wawatu waliokuwepo kwenye mkutano huo na wale waliokuwa wakimfuatilia  kupitia Luninga.

Friday, August 26, 2022

UDAKUZ SPESHO,BODA BODA AFUMANIWA NA HOUSE GIRL CHUMBANI KWA BOSI WAKE.


                                Mfano wa boda boda hiyo


 

              Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

UKISTAAJABU ya Mussa Hutoyaona ya Filahuni,dada wa Kazi’House Girl’amefumaniwa na boda boda chumbani kwa bosi wake wakiibanyua bila woga amri ya 6 ndani ya mjengo huo wa kisasa.

 

Fumani hilo la aina yake limetokea Mwanzoni mwa wiki hii,Kata ya Kihonda Maghorofani Mkoani hapa, baada ya kutokea tukio hilo lililojaza nzi’watu wengi’, wambea walimrambisha ubuyu huo wa moto moto Mdakuzi wa Mtandao huu.

 

Kwa kuwa Mtandao huu haujapata nafasi ya kuzungumza na wahusika wote kwa maana ya wafumaniwa na mfumaniaji,hivyo kwa kuzingatia maadili ya Uandishi wa habari kwa sasa majina yao tunayahifadhi mpaka hapo tutakapofanikiwa kuzungumza nao tutayaweka bayana majina yao sambamba na maelezo yao.

 

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kwamba dada huyo wa kazi alikuwa na kawaida ya kumpigia simu   boda boda huyo masaa machache baada ya bosi wake kuelekea kazini na kumwingiza chumbani wakipiga ‘Love Story.’

 

lnadaiwa katabia hako kachafu kuliota mizizi na wahusika hao kujisahau na kuifanya nyumba hiyo kama yao wakijiachia wapendavyo.

 

 Kufuati hali hiyo baadhi ya Majirani waliamua kumtonya mmiliki wa nyumba hiyo ambaye ni Mwanamke wakimueleza A-Z kwamba kila siku anapoondoka huku nyuma inakuja boda boda anazama ndani na kukaa kwa muda mrefu huku pikipiki yake ikiwa nje ya nyumba hiyo.

 

Baada ya kupewa taarifa hizo sahihi Mwanadada huyo Mrembo,aliwaomba majirani hao wanapoina boda boda hiyo wampigie simu,bila kujua kama wako kwenye mtego,mwanzoni mwa wiki hii baada mmiliki wa Mjengo huo kuelekea kazini dada huyo wa kazi alimtwangia simu boda boda wake akitumia simu ya ofisi kwa maana simu ya bosi wake aliyomkabidhi kwa lengo la matumizi sahihi ya nyumbani na si ya kuita wanaume ndani.

 

Kama kawaida boda boda huyo aliacha kazi ya kusaka kipande cha tajiri alipiga gia Pikipiki yake kuelekea ‘Rocation’alipofika kama kawa kaegesha chombo yake nje ya nyumba hiyo bila wasi wasi kana kwamba yeye ndiye baba Mjengo.

 

Yule jirani baada ya kuiona boda boda hiyo kamvutia waya mmiliki wa nyumba hiyo na kumjulisha kwamba boda boda huyo tayari yuko ndani ya nyumba, fasta dada huyo naye kapiga gia gari yake na kutinga nyumbani huku akiwa amefura kwa hasira kama tembo aliyejeruhiwa, nini kilitokea stori hii itaendelea badae hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 

 

 

Thursday, August 25, 2022

MCHEZAJI WA YANGA ATINGA MAZOEZI YA SIMBA MASHABIKI WAPIGWA NA KUTWAA.


Kocha Mkuu wa timu za Shujaa Under 10, Shujaa Under 17 na Shujaa Under 20 Jumanne Mussa akiwakochi wachezaji wa Shujaa Under 10

 


                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Katika hali ya kushangaza Mchezaji wa timu ya Watoto wa Yanga wenye umri  chini ya miaka 10 Rashid Salum’Maarufu Mukoko’ kwa sasa anashiriki kufanya mazoezi kila siku na timu ya Watoto wa timu ya Simba wenye umri huo inayomilikiwa na tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro.

 

Tukio hilo la kushangaza lililonaswa live na Mtandao huu limetokea hivi karibuni Uwanja wa Shujaa unaomilikiwa na tawi hilo la Simba ambapo siku hiyo kulifanyika mchezo Maalumu wa Kirafiki Kati ya timu ya Simba Under 20 na Simba Under 17 zote zikimilikiwa na tawi hilo Maarufu tawi la Shujaa Ngome Kuu.

 

 Kabla ya mchezo huo kuanza timu hiyo ya watoto ya Simba Under 10 ilifanya mazoezi kwenye uwanja huo chini ya Kocha Mkuu wa timu hizo tatu za tawi la Shujaa kocha Jumanne Mussa[Pichani mwenye uzi wa Simba]ambapo mchezaji huyo wa Yanga alishiriki mazoezi hayo kama anavyoonekana Pichani na jezi yake ya Yanga.

 

Tukio hilo lilizua mjadi mzito huku baadhi ya mashabiki wa Simba walidai kwamba dogo huyo anamapenzi na Simba lakini baba yake ambaye ni shabiki wa Yanga anamlazimisha mwanae kuipenda Yanga kwa  kumnunulia Jezi za timu hiyo.

 

”Huyu Mtoto kila siku anakuja kufanya mazoezi na timu yetu ya Simba anamapenzi na Simba ila baba yake anamlazimisha kuipenda Yanga akimvuta kwa kumvarisha jezi za Utoporo siumemuona mazoezi yamekwisha anaendelea kujumuika na wenzake  akimsikiliza Ticha Mussa”alisema Shabiki wa Simba aliyejitamburisha kwa jina la Shaban Mohamed.

 

 Ili kupata ukweli wa jambo hilo Mwandishi wa Mtandao huu alimfuta dogo huyo na kuzungumza naye na mahojiano yalikuwa kama hivi.

Mwandishi. Hujambo dogo.

 

 

 Dodo.Sijambo Shikamoo.

 

Mwandishi. Marahaba wewe ni shabiki wa timu gain?.

 

Dodo. Haa mkuu kusoma hujui hata Picha huioni huoni nimetinga uzi wa timu ya Wananchi Yanga.

 

Mwandishi. Kuna taarifa zinadai wewe ni shabiki wa Simba na baba yako ni shabiki wa Yanga hivyo baba yako anatumia cheo chake cha ubaba kukuvuta uipende Yanga kwa kukupatia  zawadi ya jezi za timu hiyo  je madai hayo yana ukweli yoyote?

 

 Dogo. Madai hayo hayana ukweli wowote ingawa ni kweli baba yangu ni Yanga na kweli jezi za Yanga ananinunulia akijua mimi ni Yanga damu na kamwe sipendi Simba.

 

Mwandishi.  Kama hivyo ndivyo mbona unaomekana kufanya mazoezi na Simba kila siku huenda jambo hilo ndilo linalowasukuma watu hao kuamini kwamba wewe unamapenzi na Simba.

 

Dogo. Kufanya mazoezi na Simba aina maana kwamba naipenda Simba, nafanya hivi kwa sababu ya kuibua na kuendelea kipaji changu ili nikiwa mkubwa nitumikie timu yangu ya Yanga, nafanya mazoezi na Simba kwa sababu tawi letu la Yanga hapa Moro halina uwanja wa mazoezi wenzetu Simba wanauwanja wao huu, marafiki zangu wengi ni wachezaji wa Simba hivyo wamenikaribisha kufanya nao mazoezi.

 

 Mwandishi. Unaushauri gani kwa timu yako ya Yanga hasa  Uongozi wa tawi kuu la Yanga la hapa Morogoro chini ya Mwenyekiti wa tawi hilo lssa Kitukwa ‘Chabala’

 

Dodo.Nawaomba Viongozi wetu wa Yanga na tawi la Yanga hapa Morogoro kuanzisha timu za watoto za timu yetu ya yanga kwa lengo la kukuza na kuibuka vipaji vyetu ili baadae  tuitumikie timu yetu ya Yanga.

 

Mwandishi. Asante kwa ushirikiano wako.  

Tuesday, August 23, 2022

YA SARAMBA YA KUOMBA VIATU KWA MZUNGU YAMEJIRUDIA MORO

                Mchezaji wa Simba akimuomba Viatu Mzungu

 Mzunguyo akiwajibika uwanjani huku akiwa ametinga Viatu hivyo kabla ya kuvigawa na mchezaji wa Simba Under 20


.

                 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mchezaji wa timu ya tawi kuu la Simba la Mkoani Morogoro  Shujaa Under 20 Denis Michael, amemuomba Viatu Mzungu Luia Friedrich raia wa Ujerumani mara baada ya kutamatika kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu mbili za tawi hilo za Vijana chini ya miaka 20 na 17.

 

Gemu hiyo iliyopigwa  uwanja wa Shujaa uliopo Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro unaomilikiwa na tawi hilo la Simba Maarufu tawi la Shujaa Ngome Kuu’Denis alimkimbilia mzungu huyo na kumuomba Viatu ambapo bila hiyana Mjerumani  huyo alimvulia viatu na kumkabidhi..

 

Hata hivyo kwa muonekano Viatu hivyo vilionekana kuwa vikubwa’Over Size’ kwa mchezo huyo kutokana na utofauti wa maumbile ya wawili hao.

Kufutia hali hiyo Mwandishi wa habari hizi alimfuata Denis na kuzungumza naye ambapo awari amekili kumuomba Viatu Mzungu huyo na alipoulizwa ukubwa wa Viatu hivyo alijibu.

 

” Ni kweli Jamaa Miguu yake ni mikubwa kuliko yangu kwa vile na mimi  bado na kua nitavitunza mpaka nitakapokuwa mtu mzima nitavivaa na kuvitumia kwenye michezo mbali mbali ”alisema Denis huku akiwa na furaha ya kupewa Viatu hivyo OG.

 

lkumbukwe miaka kadhaa iliyopita Simba ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Sevilla inayoshiriki ligi kuu ya Hispania na ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Mara baada ya mchezo huo uliopigwa dimba la Mkapa jijini Dar kutamatika Mchezaji wa Simba Saramba alimkimbilia mchezaji mmoja wa Sevilla na kumuomba Viatu, ambapo mzungu huyo alivua viatu hivyo na kumkabidhi mchezaji huyo.

LETE MZUNGU-LETE MZUNGU. MZUNGU MWINGINE WA SIMBA AFANYA BALAA KUBWA MOROGORO.

Mzungu wa Simba Moro Luia Friedrich[kulia] akigombea Mpira na beki Shariff Salum




.....Baada ya kufanikiwa kumpoka mpira beki huyo Mzungu akitoa basi ya bao kw amfungaji
.....Mfungaji akifunga bao baada ya kupeka pasi ya upendo kutoka kwa mzungu

 Friedrich akihojiwa na Mtandao huu,huku akiwa ametinga uzi wake wa Simba

       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kwa sasa habari ya Mjini hasa  kwenye Mitandao ya Kijamii ni mchezaji mpya wa Simba Bejan Raia wa Sebria,baada ya kuzihakiwa na mashabiki wa timu pinza, wakidai mchezaji huyo hana uwezo wa kucheza soka na kwamba Simba wamepigwa kwenye usajiri wa mchezaji huyo.

 

Wanazi hao walifikia dhihaka hiyo  baada Mzungu huyo  kutofanya vizuri kwenye michezo miwili mmoja wa ligi kuu na ule wa kirafiki siku ya tamasha la Simba Day, juzi Mzungu huyo alikata ngebe na Viherehere vya mashabiki hao waliomdhihaki baada ya kufunga bao la kideo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.

 

Baada ya Bejan kufunga bao hilo alikwenda kulishangilia jukwaani akiwasaka wale mashabiki  waliomdhihaki na kukata mauno kwa Style ya kucheza kale kamziki kao ka Lete mzungu Lete Mzungu akiwajibu kwamba amekuja sasa wana semaje.?.

 

Wakati hayo yakiendele huko jijini Dar,huku Morogoro’Mji Kasoro Bahari’ Mzungu Mwingine Luia Friedrich ameibuka akiitumika timu ya Simba B inayomilikiwa na tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro.

 

Friedrich raia wa Ujerumani ambaye yeye na familia yake ni marafiki wa tawi hilo, Maarufu tawi la Shujaa Ngome Kuu wiki iliyopita aliitumikia timu ya Shujaa Under 20 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu C ya Shujaa Under 17.

 

Katika mchezo huo wa kirafiki uliopigwa  Uwanja wa Shujaa uliopo Kata ya Mji Mpya Morogoro timu hizo zilitoka sale ya bao 1-1 huku Mzungu huyo wa Simba Morogoro aking’ara kwenye mchezo huo huku akito basi ya bao’Assit’baada ya kumtoka kwa kasi beki wa Shujaa Under 17 Shariff Salum na mzungu huyo akampenyezea pasi ya Upendo mfugaji wa bao hilo la kusawazisha.

 

Cheki Picha za tukio hilo Mzungu huyo akimchekeza beki huyo, ifahamike Vijana hao wa Shujaa wenye umri chini ya 20 na 17 wanapoonyesha viwango vya juu hupelekwa timu ya Simba B ya jijini Dar na baadae kupandishwa hadi timu wa wakubwa Simba inayoshika nafasi ya 14 kwenye viwango wa CAF.

 

lkumbukwe kwenye ramani ya dunia bara la Afrika  ndio bara kubwa duniani likiwa na nchi 54 na timu zaidi ya lakini,  kupitia takwimu za Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika’CAF’za mwaka huu zinaonyesha Simba inashika nafasi ya 14 kwa ubora barani Afrika.      

Monday, August 22, 2022

TAWI KUU LA SIMBA MORO LAPATA MARAFIKI RAIA WA UJERUMANI.

Kaibu Katibu Mkuu wa tawi la Shujaa Fadhiri Msuya akiwakabidhi zawadi wa jezi wazungu hao
Mzee Mwambeta akimkabidhi jezi msemaji wa famili hiyo



Kocha wa Shujaa Under 2o akitoa melekezo kwa vijana
Wazungu wakiingia Uwanja wa Shujaa huku watoto wakiwa wametinga jezi za Bayan
                Samora Mwarabu akihojiwa na Mtandao huu

 ...Wazungu akiondoka zao uwanja wa shujaa huku wakiwa wamependeza na uzi wa Simba


              Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Simba yenye Maskani yake Mtaa wa Msimbazi jijini Dar, kupitia tawi  kuu la Simba  Mkoani Morogoro wamepata marafiki kutoka nchini Ujeruman.

 

Mwenyekiti Msaidizi wa tawi hilo, Maarufu tawi la Shujaa ‘Ngome Kuu’Samora Mwarabu amesema wamebahatika kuwa na Urafiki na familia ya Friedrick raia wa Ujerumani ambao ni wanachama na mashabiki wa mabingwa wa nchini hiyo Bayern Munich.

 

 “Ndio maana tunaitwa Simba Taifa kubwa hawa jamaa ni marafiki zetu kupitia tawi letu la Simba na timu yetu ya Simba, baada ya mazungumzo yetu walisema tuandae mchezo wa kirafiki ili waje na marafiki zao wazungu wenzao kuishuhudia timu yetu.

 

Kama unavyojua tunatimu zetu za Vijana wa Shujaa Under 20 Wenye jezi za karoti, tukaandaa mchezo wa kirafiki  wakacheza na wadogo zao wa Under 17 wenye Jezi za mistaristari, kama ulivyoshuhudia gemu hiyo tafu iliyopigwa kwenye uwanja wetu wa shujaa na timu hizo zimetoka sale ya bao1-1 huku mgeni wetu mzungu Luia Friedrich akitia fora kwenye mchezo huu akitoa Assit ya bao la kusawazisha”alisema Samora ambaye pia anamiliki gereji kubwa eneo la kituo cha Mafuta cha Simba Oil Morogoro..

 

   Kwa upande wa msemaji wa familia hiyo Dieter Friedrich alisema wanajivunia kuwa na urafiki na timu kubwa ya Simba na kwamba watafanya mipango kuwatafutia mchezo wa kirafiki nyumbani kwao Ujerumani ikiwa ni njia moja wapo ya kudumisha urafiki wao.

 

Mara baada ya gemu hiyo kutamatika Viongozi wa Simba wamewapa zawadi ya jezi za Simba familia hiyo Luia, Friedrich aliyeichezea timu ya Under 20 ambaye picha zake akiwa uwanjani akifanya yake zitaruka hewani hivi Punde, kaka Mkubwa wa familia hiyo Dieter Friedrich na dada yao Caroline Friedrich

 

 

 

Sunday, August 21, 2022

UTOAJIA WATOTO KAFARA,UPIGAJI RAMLI NA UCHAWI VYOTE HIVYO VIMEKATAZWA NA MUNGU.


Majira ya saa 1 kasoro usiku mwenzi ukichomoza eneo la Milima ya Uluguru

Mwandishi wa Mtandao akiw akileleni kabisa mwa Milima ya Uluguru
Muonekna wa Mji wa Morogoro baada ya Mpiga Picha wa Mtandao huu kupiga Picha hii akiwa keleleni kabisa mwa Milima ya Uluguru eneo la Morning Site Kata ya Mlimani Manispaa ya Morogoro

 Mwandishi wa Mtaa huu akiwa juu ya Milima ya Uluguru eneo la Mgeta Wilaya ya Movome
 

 

KATAZO HILO LINATOKA KUMBUKUMBU YA TORATI SURA 18 -9-14.

”Utakapokwenda kuingia katika nchini,akupayo Bwana Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya Mataifa yale.

Asionekane kwako mtu ampitishaye Mwanawe au binti yake kati ya Moto, wala asionekane mtu atazamaye bao,wala mtu atazamaye nyakati mbaya,wala mwenye kubashiri wala msihiri.

 

 Wala mtu alogaye kwa kupiga Mafundo,wala mtu awaombeaye wafu.

 

Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana Mungu wako anawafukuza mbele yako.

 

Uwe mkamilifu kwa Bwana Mungu wako.Maana Mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao,bali wewe Bwana Mungu wako hakukupa ruhusa  kutenda hayo” Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya Agost 21.

                      UCHAMBUZI.

Nakumbuka kuna siku nilikwenda kushiriki msiba wa Mzee mmoja Maarufu mkoani Morogoro ambaye ni Mluguru, kwenye lbada ya msiba huo uliofanyika nyumbani kwa marehemu Kigurunyembe Mizambarauni Padre aliyeongoza lbada hiyo alikuwa  pia ni Mluguru na alipotupa jicho kwa waombolezaji alibaini wengi wao ni Waluguru.hivyo  Kwenye mahubiri yake kuna sehemu aliweka msisitizo kwa kutumia lugha ya Kiluguru.

 

” Kwa sasa kuna baadhi ya familia mtu akifariki hata kwa ajari ya gari wao hawaamini kama kafa kwa agizo la  Mungu kwa kina nafsi itaonja umauti, wao wana kwenda kupiga bao kuangalia nini kimemuua ndugu yao.

 

Baadhi ya Waluguru wenzangu  tabia hiyo tunayo utasikia familia iliyofiwa ikisema kwa Kiluguru [Chimkomile Choni?] Yaani nini kimemuua? Basi hapo familia itachanga pesa kwenda kwa Mganga kupiga bao kupata majibu la kichomuua ndugu yao.

 

Majibu hayo ni uchonganishi Mtupu, utaambiwa marehemu wenu amerogwa na yule mzee mwenyekipata pale mtaani kwenu.

 

Mnajifunga kibwembwe kwenda kugombana na huyo mzee wa watu mwisho wa siku mnajikuta mkiongeza matatizo kwa kukamatwa na Polisi”alisema Padre huyo na kupokea zawadi ya makofi mawili matatu kutoka kwa waombolezaji.

 

Naamini Padre huyo aliyasema hayo akinukua maneno haya kutoka kwenye Biblia, Somo hili linakemea uchowi na ushirikina na kutegemea nguvu za binadamu huku ukimpa kisogo Mungu.

 

Baadhi ya mambo ya kuliyokatazwa na Mungu kwenye neno hilo ni Pamoja na kupiga Ramli, kuvaa hirizi’hapo wamesema fundo na kubashiri wale mashabiki wa soka wanao Bet mjuwe  kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu. Kwa leo mtumishi wako naishi hapa Mungu akipenda tukutane Jumapili ijayo endelea kuwa jirani na Mtandao huu siku zote.

                        


                               

                              

Saturday, August 20, 2022

MKUU WA MKOA WA MOROGORO LEO AMESHIRIKI MARATHON



                                                   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro


                                     Mfamasia maarufu Morogoro akishiriki mbio hizo


 

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Mh Fatma Mwasa leo asubuhi ameshiriki mbio za  Solous Marathon, habari kamili na picha zaidi za tukio hilo zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtndao huu muda wote.

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...