Na Dustan Shekidele,Morogoro.
REHEMA za Mwenyezi Mungu na ziwe juu yenu wadau wote wa Mtandao Pendwa wa Shekidele,natumai mna afya njema na wale wagonjwa na wenye changamoto mbali mbali namuomba Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi.
Kwenye maombi yetu hayo hatukulazimishi Mwenyezi Mungu ila ni kwa utashi wako tukitekeleza maagizo yako kwamba tusikome kukuomba na kukukimbila tunapokumbana na changamoto mbali mbali.
Ama baada ya salaam hizo tuingia kwenye mada yetu ya leo Ijumaa ya Agost Mosi 2025, kwenye mada hii bila hiyana Mtandao huu unaupongeza Uongozi wa Makampuni ya Bakhresa chini ya Mmiliki na Mwenyekiti wa Mkampuni hayo Mzee Said Salim Bakhresa na Mzee Abdallah Ngemo, anayemiliki nyumba tatu zilizopo Mikoa ya Tanga na Morogoro.
KWA NINI TUNAWAPONGEZA.?
Tunawapongeza na kuwatia moyo kwa kufanya matendo mema kwa jamii,wakitimiza maagizo ya Mwenyezi Mungu aliyetuagiza viumbe wake kutenda mambomema yakiwemo ya kuwasaidia wenye uhitaji.
Kwa Mzee Bakhresa kwa miaka ya hivi karibuni kupitia meli zake zote ameamua kusafirisa maiti bure kutoka Tanzania bara kwenda Zanzibar na kutoka Zanzibar kuja Tanzania Bara.
Kwa upande wa Mzee Ngemo yeye kwenye nyumba zake zote tatu kila unapofika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wapangaji wake wote hawatozi kodi.
Baada ya kupokea taarifa hizo Leo ijumaa Mtandao huu ulimtwangia simu Mzee Ngemo ambaye alithibitisha taarifa hizo.
“ Mgosi Shekidele Mwenyezi Mungu kanijalia kumiliki nyumba tatu ambazo kila moja inanyumba 15, nyumba moja iko hapo Morogoro mtaa wa Tubuyu ‘B’ kata ya Tungi na mbili ziko hata jijini Tanga moja ipo Chumbageni na nyingine ipo barabara ya 18.
Hiyo ya 18 hivi karibuni wenye pesa wamenishawishi nimeiuza hivyo zimebaki mbili, ni kweli miaka yote ikifika mwezi Ramadhani wapangaji wangu wote ziwatozi kodi awe Mwislam au asiwe Mwislam nimeamua kufanya hivyo wale waliojaliwa kufunga wahangaike kutafuta Futari na Daku wasihangaike kutafuta kodi ya Nyumba” amesema Mzee huyo ambaye makazi yake ni chumbageni Tanga.
Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mtandao huu umebaini kwenye nyumba za Mzee huyo mpangaji anapo hama watu wengi wanagombea kuhamia kwenye nyumba hizo hasa wale majirani wanaijua ofa hiyo wanaradhimika kuhama kwenye nyumba wanazoishi na kuhamia kwenye nyumba hizo.
Kwa upande wa Azam wiki iliyopita nilikutana na Selemam Mpemba mkazi wa Kata ya Mji Mkuu mkoani hapa akisimulia Azam walivyomsaidia kwenye tatizo lake.
“ Kuna siku ndugu yangu mzanzibar mwenzangu alifariki dunia hapa Morogoro na familia wamesema lazima akazikwe nyumbani Pemba kichwa niliniuma nikiwaza gharama za kusafirisha maiti kutoka Morogoro Mpaka bandarini Dar es salaam kisha kusafirisha kwenye meli kuelekea nyumbani pemba.
Kwa bahati nzuri wakati tunajadiri hilo kuna Mpemba mwenzetu katuambia Azam anasafirisha maiti bure, hivyo tumekodi gari kutoka hapa Moro mpaka bandarini Dar tukapewa kibari cha kusafirisha maiti bure huku sisi wengine tulilipa nauli za kawaida kipekee tunamshukuru sana Azam kwa jambo hili jema”alisema Mzee Seleman.

No comments:
Post a Comment