MAZOEZI NI AFYA.
Leo Agost 30 majira ya saa 11 jion mchezaji tegemo wa timu ya Moro Veterani Dunstan Shekidele’Mkude Simba’aliwasili uwanja wa Shujaa na usafiri wake wa baiskeri a.k.a ‘Anita’unaomilikiwa na tawi kuu la Simba la Mkoani Morogoro, kufanya mazoezi na timu hiyo kabambe mkoani Morogoro.
Kwa sasa timu hiyo ya Morogoro Veterani inajianda na na Safari ya jijini Dar kwenye bonanza litakarofanyika mwishoni Mwa wiki hii.
lfahamike kwa sasa Moro Veterani inayoundwa na wachezaji wengi maarufu nchini akiwemo tajiri Aziz Abood ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Arbet Msando, Maprofesa wa vyuo Vikuu vya Mkoani Morogoro wakiongozwa na Profesa Madundo Mtambo, Maafande wa Majeshi ya Polisi ,JWTZ na Magereza.
Wengine ni wachezaji nyota wa zamani wa Simba na Yanga, akiwemo Ramadhan Kichuya baba mzazi wa Shiza Kichuya na Hamis Kidingile ambaye ni baba mzazi wa beki Hassan Kessy.
Awari Moro Veteran walikuwa wakifanya mazoezi viwanja vya hospital ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro vilivyopo jirani kabisa na chumba cha kuhifadhia maiti’Mochori’,
Kwa sasa Uongozi wa hospital hiyo umeamua kuongeza majengo kwenye eneo hilo hivyo tumelazimika kuutumia uwanja wa Shujaa uliopo Mji Mpya ambapo Vijana wa timu za Shujaa Under 10,Under 17 na Under 20 zinazomilikiwa na tawi la Simba wanaanza mazoezi saa 9 alasri na kumaliza saa 11 jioni.
Wanawapisha Moro Veteran wanaoza mazoezi muda huo wa saa 11 mpaka saa moja kasoro usiku.
No comments:
Post a Comment