Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, August 25, 2022

MCHEZAJI WA YANGA ATINGA MAZOEZI YA SIMBA MASHABIKI WAPIGWA NA KUTWAA.


Kocha Mkuu wa timu za Shujaa Under 10, Shujaa Under 17 na Shujaa Under 20 Jumanne Mussa akiwakochi wachezaji wa Shujaa Under 10

 


                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Katika hali ya kushangaza Mchezaji wa timu ya Watoto wa Yanga wenye umri  chini ya miaka 10 Rashid Salum’Maarufu Mukoko’ kwa sasa anashiriki kufanya mazoezi kila siku na timu ya Watoto wa timu ya Simba wenye umri huo inayomilikiwa na tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro.

 

Tukio hilo la kushangaza lililonaswa live na Mtandao huu limetokea hivi karibuni Uwanja wa Shujaa unaomilikiwa na tawi hilo la Simba ambapo siku hiyo kulifanyika mchezo Maalumu wa Kirafiki Kati ya timu ya Simba Under 20 na Simba Under 17 zote zikimilikiwa na tawi hilo Maarufu tawi la Shujaa Ngome Kuu.

 

 Kabla ya mchezo huo kuanza timu hiyo ya watoto ya Simba Under 10 ilifanya mazoezi kwenye uwanja huo chini ya Kocha Mkuu wa timu hizo tatu za tawi la Shujaa kocha Jumanne Mussa[Pichani mwenye uzi wa Simba]ambapo mchezaji huyo wa Yanga alishiriki mazoezi hayo kama anavyoonekana Pichani na jezi yake ya Yanga.

 

Tukio hilo lilizua mjadi mzito huku baadhi ya mashabiki wa Simba walidai kwamba dogo huyo anamapenzi na Simba lakini baba yake ambaye ni shabiki wa Yanga anamlazimisha mwanae kuipenda Yanga kwa  kumnunulia Jezi za timu hiyo.

 

”Huyu Mtoto kila siku anakuja kufanya mazoezi na timu yetu ya Simba anamapenzi na Simba ila baba yake anamlazimisha kuipenda Yanga akimvuta kwa kumvarisha jezi za Utoporo siumemuona mazoezi yamekwisha anaendelea kujumuika na wenzake  akimsikiliza Ticha Mussa”alisema Shabiki wa Simba aliyejitamburisha kwa jina la Shaban Mohamed.

 

 Ili kupata ukweli wa jambo hilo Mwandishi wa Mtandao huu alimfuta dogo huyo na kuzungumza naye na mahojiano yalikuwa kama hivi.

Mwandishi. Hujambo dogo.

 

 

 Dodo.Sijambo Shikamoo.

 

Mwandishi. Marahaba wewe ni shabiki wa timu gain?.

 

Dodo. Haa mkuu kusoma hujui hata Picha huioni huoni nimetinga uzi wa timu ya Wananchi Yanga.

 

Mwandishi. Kuna taarifa zinadai wewe ni shabiki wa Simba na baba yako ni shabiki wa Yanga hivyo baba yako anatumia cheo chake cha ubaba kukuvuta uipende Yanga kwa kukupatia  zawadi ya jezi za timu hiyo  je madai hayo yana ukweli yoyote?

 

 Dogo. Madai hayo hayana ukweli wowote ingawa ni kweli baba yangu ni Yanga na kweli jezi za Yanga ananinunulia akijua mimi ni Yanga damu na kamwe sipendi Simba.

 

Mwandishi.  Kama hivyo ndivyo mbona unaomekana kufanya mazoezi na Simba kila siku huenda jambo hilo ndilo linalowasukuma watu hao kuamini kwamba wewe unamapenzi na Simba.

 

Dogo. Kufanya mazoezi na Simba aina maana kwamba naipenda Simba, nafanya hivi kwa sababu ya kuibua na kuendelea kipaji changu ili nikiwa mkubwa nitumikie timu yangu ya Yanga, nafanya mazoezi na Simba kwa sababu tawi letu la Yanga hapa Moro halina uwanja wa mazoezi wenzetu Simba wanauwanja wao huu, marafiki zangu wengi ni wachezaji wa Simba hivyo wamenikaribisha kufanya nao mazoezi.

 

 Mwandishi. Unaushauri gani kwa timu yako ya Yanga hasa  Uongozi wa tawi kuu la Yanga la hapa Morogoro chini ya Mwenyekiti wa tawi hilo lssa Kitukwa ‘Chabala’

 

Dodo.Nawaomba Viongozi wetu wa Yanga na tawi la Yanga hapa Morogoro kuanzisha timu za watoto za timu yetu ya yanga kwa lengo la kukuza na kuibuka vipaji vyetu ili baadae  tuitumikie timu yetu ya Yanga.

 

Mwandishi. Asante kwa ushirikiano wako.  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...