Morgoro Mji kasoro Bahari. ndiyo kauli ya Waluguru wa Mkoa wa Morogoro.
Hii sio Meli na wala sio Uwanja wa Ndege 'Air Port' ni stend ya mabasi ya Mikoani ya Msamvu Morogoro. Picha na Dustan Shekidele.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WANANCHI Mkoa wa Morogoro wamelipongeza Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Usalama barabara kilichopiga marufuku wakatisha tiketi wa stend ya Mabasi ya Msamvu kuwakatia tiketiki abiria wakati basi husika halijafika ndani ya stendi.
Awari baadhi ya wafanyakazi wa mabasi,Mawakala, wakatisha tiketi na wapiga debe’Masalange’ wamekuwa na tabia ya kuwakatia tiketi abiri wakati wanajua fika basi husika halijafika stend huenda liko Gereji au bado liko safarini likitokea mikoani.
Kufuatia kero hiyo hivi karibuni Maafisi wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro walitinga kwenye stend hiyo ya kisasa na kupiga marufuku abiria kukatiwa tiketike wakati basi husika halijafika stendi,
Vijana hao wa IGP Wambura wamewakata wakatishaji tiketi hao kumkabidhi tiketi abiria wakati basi husika lipo stend hivyo na kwamba abiria anapokabidhiwa tiketi moja kwa moja anaingia kwenye basi.
Mtandao huu unaungana na wananchi hao kulipongeza Jeshi la Polisi kukomesha kero hiyo kwa wananchi
Ifahamike mara kwa mara msimulizi wa habari hii hukatiza kwenye stendi hiyo kwa shughuri zake mbali mbali alishuhudia ‘Live’ kero hiyo huku wanaofanya jambo hilo wakiambizama maneno haya ya kejeri.
“ Twenda tukasake abiria mwingine Yule nimeshamnyofoa mbaya hanauwezo tena wa kuruka atasubiri mpaka chuma lifike”
Kauli zao nyingene “Yule abiri nimeshamkata miguu hatembei tena tukatafute abiri mwingingine tuingize posho kwa tajiri”
Wapigadebe hao wanamaanisha kwamba abiri huyu hawezi kupanda basi lingine kwa sababu tayari wameshamuzia tiketi hivyo hata kama basi litafika baada ya masaa matatu au manne mbele atasubiri tu ndio maana wanakauli zao hizo za kumnyofoa mbaya na kumkata miguu.
Wapiga debe hao wanajisahau kwamba kuna wasafiri wengine wanaharaka, mfano wengine wanakwenda msibani, wengine wanakwenda kwa wagonjwa na wengine ni wanafunzi .
No comments:
Post a Comment