Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, August 26, 2022

UDAKUZ SPESHO,BODA BODA AFUMANIWA NA HOUSE GIRL CHUMBANI KWA BOSI WAKE.


                                Mfano wa boda boda hiyo


 

              Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

UKISTAAJABU ya Mussa Hutoyaona ya Filahuni,dada wa Kazi’House Girl’amefumaniwa na boda boda chumbani kwa bosi wake wakiibanyua bila woga amri ya 6 ndani ya mjengo huo wa kisasa.

 

Fumani hilo la aina yake limetokea Mwanzoni mwa wiki hii,Kata ya Kihonda Maghorofani Mkoani hapa, baada ya kutokea tukio hilo lililojaza nzi’watu wengi’, wambea walimrambisha ubuyu huo wa moto moto Mdakuzi wa Mtandao huu.

 

Kwa kuwa Mtandao huu haujapata nafasi ya kuzungumza na wahusika wote kwa maana ya wafumaniwa na mfumaniaji,hivyo kwa kuzingatia maadili ya Uandishi wa habari kwa sasa majina yao tunayahifadhi mpaka hapo tutakapofanikiwa kuzungumza nao tutayaweka bayana majina yao sambamba na maelezo yao.

 

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kwamba dada huyo wa kazi alikuwa na kawaida ya kumpigia simu   boda boda huyo masaa machache baada ya bosi wake kuelekea kazini na kumwingiza chumbani wakipiga ‘Love Story.’

 

lnadaiwa katabia hako kachafu kuliota mizizi na wahusika hao kujisahau na kuifanya nyumba hiyo kama yao wakijiachia wapendavyo.

 

 Kufuati hali hiyo baadhi ya Majirani waliamua kumtonya mmiliki wa nyumba hiyo ambaye ni Mwanamke wakimueleza A-Z kwamba kila siku anapoondoka huku nyuma inakuja boda boda anazama ndani na kukaa kwa muda mrefu huku pikipiki yake ikiwa nje ya nyumba hiyo.

 

Baada ya kupewa taarifa hizo sahihi Mwanadada huyo Mrembo,aliwaomba majirani hao wanapoina boda boda hiyo wampigie simu,bila kujua kama wako kwenye mtego,mwanzoni mwa wiki hii baada mmiliki wa Mjengo huo kuelekea kazini dada huyo wa kazi alimtwangia simu boda boda wake akitumia simu ya ofisi kwa maana simu ya bosi wake aliyomkabidhi kwa lengo la matumizi sahihi ya nyumbani na si ya kuita wanaume ndani.

 

Kama kawaida boda boda huyo aliacha kazi ya kusaka kipande cha tajiri alipiga gia Pikipiki yake kuelekea ‘Rocation’alipofika kama kawa kaegesha chombo yake nje ya nyumba hiyo bila wasi wasi kana kwamba yeye ndiye baba Mjengo.

 

Yule jirani baada ya kuiona boda boda hiyo kamvutia waya mmiliki wa nyumba hiyo na kumjulisha kwamba boda boda huyo tayari yuko ndani ya nyumba, fasta dada huyo naye kapiga gia gari yake na kutinga nyumbani huku akiwa amefura kwa hasira kama tembo aliyejeruhiwa, nini kilitokea stori hii itaendelea badae hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...