Mzee Mwambeta akimkabidhi jezi msemaji wa famili hiyo
Kocha wa Shujaa Under 2o akitoa melekezo kwa vijana
Wazungu wakiingia Uwanja wa Shujaa huku watoto wakiwa wametinga jezi za Bayan
Samora Mwarabu akihojiwa na Mtandao huu
...Wazungu akiondoka zao uwanja wa shujaa huku wakiwa wamependeza na uzi wa Simba
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
TIMU ya Simba yenye Maskani yake Mtaa wa Msimbazi jijini Dar, kupitia tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro wamepata marafiki kutoka nchini Ujeruman.
Mwenyekiti Msaidizi wa tawi hilo, Maarufu tawi la Shujaa ‘Ngome Kuu’Samora Mwarabu amesema wamebahatika kuwa na Urafiki na familia ya Friedrick raia wa Ujerumani ambao ni wanachama na mashabiki wa mabingwa wa nchini hiyo Bayern Munich.
“Ndio maana tunaitwa Simba Taifa kubwa hawa jamaa ni marafiki zetu kupitia tawi letu la Simba na timu yetu ya Simba, baada ya mazungumzo yetu walisema tuandae mchezo wa kirafiki ili waje na marafiki zao wazungu wenzao kuishuhudia timu yetu.
Kama unavyojua tunatimu zetu za Vijana wa Shujaa Under 20 Wenye jezi za karoti, tukaandaa mchezo wa kirafiki wakacheza na wadogo zao wa Under 17 wenye Jezi za mistaristari, kama ulivyoshuhudia gemu hiyo tafu iliyopigwa kwenye uwanja wetu wa shujaa na timu hizo zimetoka sale ya bao1-1 huku mgeni wetu mzungu Luia Friedrich akitia fora kwenye mchezo huu akitoa Assit ya bao la kusawazisha”alisema Samora ambaye pia anamiliki gereji kubwa eneo la kituo cha Mafuta cha Simba Oil Morogoro..
Kwa upande wa msemaji wa familia hiyo Dieter Friedrich alisema wanajivunia kuwa na urafiki na timu kubwa ya Simba na kwamba watafanya mipango kuwatafutia mchezo wa kirafiki nyumbani kwao Ujerumani ikiwa ni njia moja wapo ya kudumisha urafiki wao.
Mara baada ya gemu hiyo kutamatika Viongozi wa Simba wamewapa zawadi ya jezi za Simba familia hiyo Luia, Friedrich aliyeichezea timu ya Under 20 ambaye picha zake akiwa uwanjani akifanya yake zitaruka hewani hivi Punde, kaka Mkubwa wa familia hiyo Dieter Friedrich na dada yao Caroline Friedrich
No comments:
Post a Comment