Majira ya saa 1 kasoro usiku mwenzi ukichomoza eneo la Milima ya Uluguru
Mwandishi wa Mtandao akiw akileleni kabisa mwa Milima ya Uluguru
Muonekna wa Mji wa Morogoro baada ya Mpiga Picha wa Mtandao huu kupiga Picha hii akiwa keleleni kabisa mwa Milima ya Uluguru eneo la Morning Site Kata ya Mlimani Manispaa ya Morogoro
Mwandishi wa Mtaa huu akiwa juu ya Milima ya Uluguru eneo la Mgeta Wilaya ya Movome
KATAZO HILO LINATOKA KUMBUKUMBU YA TORATI SURA 18 -9-14.
”Utakapokwenda kuingia katika nchini,akupayo Bwana Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya Mataifa yale.
Asionekane kwako mtu ampitishaye Mwanawe au binti yake kati ya Moto, wala asionekane mtu atazamaye bao,wala mtu atazamaye nyakati mbaya,wala mwenye kubashiri wala msihiri.
Wala mtu alogaye kwa kupiga Mafundo,wala mtu awaombeaye wafu.
Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana Mungu wako anawafukuza mbele yako.
Uwe mkamilifu kwa Bwana Mungu wako.Maana Mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao,bali wewe Bwana Mungu wako hakukupa ruhusa kutenda hayo” Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya Agost 21.
UCHAMBUZI.
Nakumbuka kuna siku nilikwenda kushiriki msiba wa Mzee mmoja Maarufu mkoani Morogoro ambaye ni Mluguru, kwenye lbada ya msiba huo uliofanyika nyumbani kwa marehemu Kigurunyembe Mizambarauni Padre aliyeongoza lbada hiyo alikuwa pia ni Mluguru na alipotupa jicho kwa waombolezaji alibaini wengi wao ni Waluguru.hivyo Kwenye mahubiri yake kuna sehemu aliweka msisitizo kwa kutumia lugha ya Kiluguru.
” Kwa sasa kuna baadhi ya familia mtu akifariki hata kwa ajari ya gari wao hawaamini kama kafa kwa agizo la Mungu kwa kina nafsi itaonja umauti, wao wana kwenda kupiga bao kuangalia nini kimemuua ndugu yao.
Baadhi ya Waluguru wenzangu tabia hiyo tunayo utasikia familia iliyofiwa ikisema kwa Kiluguru [Chimkomile Choni?] Yaani nini kimemuua? Basi hapo familia itachanga pesa kwenda kwa Mganga kupiga bao kupata majibu la kichomuua ndugu yao.
Majibu hayo ni uchonganishi Mtupu, utaambiwa marehemu wenu amerogwa na yule mzee mwenyekipata pale mtaani kwenu.
Mnajifunga kibwembwe kwenda kugombana na huyo mzee wa watu mwisho wa siku mnajikuta mkiongeza matatizo kwa kukamatwa na Polisi”alisema Padre huyo na kupokea zawadi ya makofi mawili matatu kutoka kwa waombolezaji.
Naamini Padre huyo aliyasema hayo akinukua maneno haya kutoka kwenye Biblia, Somo hili linakemea uchowi na ushirikina na kutegemea nguvu za binadamu huku ukimpa kisogo Mungu.
Baadhi ya mambo ya kuliyokatazwa na Mungu kwenye neno hilo ni Pamoja na kupiga Ramli, kuvaa hirizi’hapo wamesema fundo na kubashiri wale mashabiki wa soka wanao Bet mjuwe kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu. Kwa leo mtumishi wako naishi hapa Mungu akipenda tukutane Jumapili ijayo endelea kuwa jirani na Mtandao huu siku zote.
No comments:
Post a Comment