Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, January 31, 2023

MAAJABU YA MJI KASORO BAHARI MGOMBA WAZAA MIKUNGU 2 YA NDIZI.


 

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 

 Ukistaajabu ya Musa hutoyaona ya Filahuni, Mgomba uliombandwa ndani ya uzio wa nyumba ya Mzee Mongi iliyopo Kihonda Maghorofani umezaa Mikungu miwili ya ndizi kwa mpigo.

 

Baada ya kuona hali hiyo Mmiliki wa nyumba hiyo Mzee Mongi alimtwangia simu Mwandishi wa Mtandao huu kumwalika nyumbani kwake kuchukua tukio hilo adhimu kutokea kwenye Jamii yetu.

 

Kwenye mahojiano Maalumu Mzee Mongi Mchaga wa Moshi Mkoani Kilimanjaro alipoulizwa kama ndizo hizo zikikomaa atazivuna na kuzila na familia yake au atazipiga bei? Jibu lake lilikua hili.

 

” Shekidele ndizi hizi zimekuwa kivutio hapa nyumbani kila siku watu wanakuja kwa wingi kuzishangaa hivyo zitabaki kuwa kivutio mpaka zitakapokomaa na kuivia mtini”.


 

Monday, January 30, 2023

WITO KWA WATANZANIA WENZANGU.




 


 

Tujitokeze kwa wingu kuchangia damu kwenye kituo chochote cha afya kwa lengo la kuimalisha Bank ya damu inayotumika kusambaza damu kwa ndugu zetu wagonjwa wenye uhitaji wa kuongezewa damu.

 

Tunafundishwa na Viongozi wetu wa dini kwamba tufanye matendo mema na ya huruma kwa ndugu zeru wenye uhitaji.

 

Kwamba kama unaviwili mgawie kimoja mtu mwenye uhitaji wa kituo hicho.Mwenyezi MUNGU Mwingi wa Rehema atufanyie wepesi tuwe na mioyo hiyo ya huruma na atuondolee ubinfsi na mioyo ya choyo.  .

 

 Kutoa kwako damu kutasaidia kuokoa maisha ya ndugu zetu hasa Wazazi na Majeruhi wa ajari mbali mbali zikiwemo za barabarani.

 

Kutoa ni moyo sio utajiri,nashukuru uongozi wa hospital umethamini mchango wangu huo baada ya kumalizi kugemwa damu hiyo iliyojaa kifuko cha kilo 2 wamenipa  zawadi ya Mirinda nyeusi na kadi  Maalumu ya damu salama.

 

Kwa mujibu wa maelezo yao kadi hii ni kitambulisho cha kuwa na hisa ya damu kwenye bank hiyo.

 

 Hivyo ikitokea mimi au ndugu yangu tukihitaji huduma hiyo nikionyesha kadi hii napatiwa huduma hiyo bure kutoka kwenye bank hiyo ya damu salama kwa uwekezaji wangu huo ilioufanya zaidi ya mara mbili kwa miaka miwili mfurulizo. .

Sunday, January 29, 2023

BARAKA ZA MUNGU NYUMBANI.






 

UJUMBE WA NENO LA MUNGU

SOMO KUTOKA.

 

ZABURI. 127.1-5

 


 

BWANA asipoijenga nyumba waijengao wafanyakazi bure.

 

Bwana asipoulinda Mji yeye aulindaye akesha bure.

 

Kazi yenu ni bure Mnaoamka mapema na kukawia kwenda kulala na kula chakula cha taabu,yeye humpa Mpenzi wake usingizi,

 

Tazama wana ndio Urithi wa Bwana Uzao wa tumbo ni dhawabu.

 

Kama Mishale Mkononi mwa Shujaa ndivyo walivyo wana wa Ujanani.

 

Heri mtu yule aliyelijaza podo lake hivyo.

 

Naam,hawataona aibu wanaosema na adui langoni” Hilo ndilo leno la MUNGU Jumapili ya leo January 29.

 UCHAMBUZI WA NENO HILO UNALETWA KWAKO NA DUSTAN SHEKIDELE.

Soma hapo juu linasema Bwana asipoijenga nyumba wajengao wafanyakazi bure.

 

 Somo hilo pia linasema Bwana asipoulinda mji waulindao wakesha bure.

 

Tumeshuhudia baadhi ya watu wakijenga nyumba zao nzuri kwa kujaliwa kipato na Mwenyezi Mungu.

 

Chakushangaza baada ya kuhamia kwenye nyumba hizo wanafanya sherehe za watu kuywa pombe usiku kucha na baadae wanafukia mapembe kama zindiko la nyumba hiyo.

 

Jambo hilo ni chukizo kubwa Mbele za Mungu.

 

Kuna baadhi ya watu wenye ufahamu wanapopata Neema ya kujenga nyumba wanapohamia  humwalika Kiongozi wa dini kuja kufanya maombi au dua hiyo baada ya maombi na dui hiyo kukamilika mmiliki wa nyumba hiyo hutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu kwa kumjalia kupata nyumba hiyo.

 

Wengine wameamua kufanya matendo mema zaidi kwa kuruhusu nyumba ya lbada kujengwa  nje ya nyumba zao  kama alivyofanya Mwandishi wa Mtandao huu.

 

Kama hiyo haitoshi Mungu anasema yeye asipokaribishwa na mwenye nyumba kulinda mji  walinzi aliowaajiri wamlinde wana kesha bure.

 

Tumeshuhudia baadhi ya nyumba za matajiri zinalindwa na walinzi wenye silaha nzito,ndani ya uzi kuna Mbwa wenye mafunzo wa kijeshi,  kwenye uzio kuna nyaya za umeme za kuzuia waharifu kuluka ukuta, kwenye nyumba hiyo hiyo kuna kamera za ulinzi ‘CCTV Camera’

 

 Licha ya ulinzi wote huo utastaajabu kukicha unaambiwa mmiliki wa nyumba hiyo amefariki dunia  chumbani  akiwa kwenye uzingizini mzito na chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa shinikizo la damu’Presha’

 

Hapo ndipo kauli ya Mungu inapodhihirisha kwamba usipomwalika yeye kuulinda Mji wako  waulindao wakesha bure.

 

Nilichojifunza mimi kwenye somo hili tusijivunie na haya Maboma[Nyumba]tukamsahamu Mungu au  yakatupa kiburi cha kuwanyanyasa na kuwadharau watu wengine wakiwemo wapangaji wetu.

 

 Tukumbuke tutakufa tutayaacha haya Maboma hata yawe mazuri kisiasi gani hatutakwenda nayo kaburini.

 

 Kwa Wakristo tutakwenda kaburini na sanduku la pembe nne na watu wa dini nyingine watakwenda kaburini na vipande vitatu vya sanda.

 

Friday, January 27, 2023

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA









 

Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.

Kama kawaida mtumishi wako kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.

Miongoni mwa jumbe jizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU.

Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.

Shekidele Mkude Simba hana hatia.

 

Thursday, January 26, 2023

MWANDISHI MORO PRESS CLUB ATEULIWA NA RAIS KUWA MKUU WA WILAYA YA SAME


 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Hongera sana Mwandishi wa habari mwenzangu hongera sana Mwanachama Mwenzangu wa Cha Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’Mh Kasilda Mgeni Mlimila kwa kuteuliwa Jana na Rais  Dkt  Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Same.

 

 lfahamike Mh Kasilda kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Tawala[DAS] takribani miaka 6 iliyopita alikuwa Mtangazaji wa Star Tv na Radio Free Afrika  Mkoa wa Morogoro, tukihangaika wote mtaani kusaka habari.

 

Nakumbuka baada ya kuteuliwa kuwa [DAS]nafasi hiyo ya uwakilishi wa Star Tv Mkoa wa Morogoro ulimkabidhi Nickson Mkilanya ambaye aliitumikia nafasi hiyo ya utangazaji kabla na yeye kuiacha ofisi hiyo ya Star Tv na kumwachia kijiti Mtangazaji wa sasa wa Star Tv Omary Hussein.

 

Kwa sasa Mkilanya ndiye Mwanyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro ambaye ndiye aliyesaini barua hii ya Pongezi kwa Mwanachama wake na Mfanyakazi mwenzie wa Star Tv.

 

Mh Kaslda mara nyingi huwa napita hapo Same kwenda Moshi na Arusha kwa ndugu zangu hivyo hapana shaka yoyote nikipita hapo nitakupigia simu tuonane uso kwa macho nikupe pongezi zangu Live a.k.a Mubashara kwa sasa pokea Pongezi hizi kupitia kwenye Mtandao huu pendwa wa Shekidele ambapo wewe pia ni mdau mkubwa wa Mtandao huu.

 

Vigogo wengine niliowahi kufanya nao kazi ya Uandishi wa habari Mkoani Morogoro waliotimkia kwenye siasa na sasa ni Mastaa nchini Tanzania ni pamoja na  Mtangazaji wa ITV na Radio One Mkoa wa Morogoro Devotha Minja aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa leseni ya Chadema ambaye pia ni Mwanachama hai wa Morogoro Press Club.

 

Mwingine Mwandishi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalengo Mkoa wa Morogoro Esther Bulaya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM kabla ya kutimkia Chadema na kufanikiwa kumbwaga  aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Bunda  Mzee Wasira kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

 

Kwa sasa Esther na wenzake 18 wanaounda timu ya wabunge 19 wa Viti Maalumu walivyovinyakua kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka 2020 kupitia Chadema wakiongozwa na Madam Halima Mdee wako kwenye kesi Mahakamani na chama chao cha Chadema huhusiana na ubunge wao huo wa kuteuliwa.

Tuesday, January 24, 2023

STEND IPI KALI KATI YA STEN YA DAR NA MORO

                              Stend ya Magufuli
Rais wa awanu ya tano Hayati John Pombe Magufuri enzi za Uhai wake
                    Stend ya Mabasi ya Msamvu Morogoro

 


 

Kwa sasa stend bora za mabasi Tanzania na ukanda wa Afrikari Mashariki na Kati ni mbili.

 

 Stend ya Mabasi ya Msamvu iliyopo eneo la Msamvu Morogoro yenye Muonekana kama Meli na Stend ya Magufuri iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam yenye Muonekano wa Kipekee.

 

 Pichani zaidi ya mabasi 20 Mapya ya kampuni Pendwa ya Abood yenye makao yake Makuu Mkoani Morogoro yakiingia  Stend ya Magufuri yakitokea Bandarini.

 

Watanzania tunabahati ya kupata vitu vizuri lakini changamoto yetu ni kuvitunza vitu hivyo nakumbuka Mwaka jana baadhi ya wafanyakazi wa kampuni moja ya mabasi walinipigia simu wakidai Vyoo vya Stend hiyo Mpya ya Msamvu vimefungwa kufuatia baadhi ya watu kuiba koki za bomba ndani ya vyoo hivyo hali iliyopelekea vyoo hivyo kukosa Maji.

 

Swali kwa Mdau wa Mtandao wa Shekidele kati ya Stend hizo mbili ili kali zaidi ya nyingine ya Moro au ya Dar?

 

Baada ya siku chache wahusika waliweka koki nyingine na kuvifungua Vyoo hivyo vya kisasa.

Sunday, January 22, 2023

KAULI YA YA SHEKIDELE MKUDE SIMBA.

                    Shekidele Mkude Simba Arsenal lia lia

 


“Nidhambi kubwa kukata tamaa kwa Jambo ambalo hujui mwisho wake utakuwaje.”

 

Kuna Mtu anabisha kuhusu timu bora ya Arsenal Kutwaa Ubingwa wa England Msimu huu?”

 

Usiku huu Arsenal Washika bunduki wa Jiji  la Maraha la London imeinyuka bila huruma timu inayoshikiliwa na  Madalali  kwa sasa baada ya kutangazwa kuuzwa naizungumzia  Manchester United Kwa bao 3-2 na kukata ngebe za mashetani hao wekundu.

Saturday, January 21, 2023

TANZIA.DENT WA KIDATO CHA 6 AFARIKI DUNIA


 


Taarifa kwa hisani ya Radio Ukweli inayomilikliwa na kanisa Katoliki Jimbo na Morogoro ambapo pia shule hiyo ya Kigurunyembe inamilikiwa na kanisani hilo Taarifa hiyo inasomeka hivi.
"Mwanafunzi mmoja wa kidato cha sita Shule ya Sekondari Kigurunyembe mkoani Morogoro Namith Jackob Sayore amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Nanguji mkoani humo.
Akizungumza na Radio Ukweli Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Daniel Lameck Chipindula amesema kuwa afya ya Mwanafunzi huyo ilianza kutetereka siku za karibuni na umauti umemkuta usiku wa Januari 19 mwaka huu wakati yupo katika matibabu Hospitalini hapo.
Naye Mzazi wa Mwanafunzi huyo Jackob Sayore Mmbaga amesema ameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa
Kwa upande wao baadhi ya Wanafunzi Shuleni hapo wamebainisha kuwa Msiba huo ni mkubwa kwao kwani alikuwa ni Mwanafunzi ambaye Rafiki kwa kila mmoja Shuleni hapo hivyo watamkumbuka kwa mengi.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI....... AMINAA.

UKAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU SIMBA MGOMBEA APANGUA MASWALI YA WANACHAMA.

Mbombea nafasi ya Uwenyekiti wa Klabu ya Simba  Wakili Moses Kaluwa akimwaga sera zake kwa wanachma wa timu hiyo tawi la Shujaa Morogoro juzi jioni
...Mgombea huyo akijibu Maswali ya wanachama hao



 


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mgombea nafasi ya Uwenyekiti wa timu ya Simba Wakili Moses Kaluwa juzi alipangua kiufasaha Maswali  ya wanachama wa tawi kuu la Simba la Mkoani Morogoro kwenye mkutano wa kampeni.

 

Wakili Kaluwa aliyeasindikizwa na wapambe wake waliojaa Coaster Mbili walipotoka Dar walipita Moro Mjini wakaelekea tawi la Simba la Dumila baadae wakageuka wakarejea Moro Mjini kwenye tawi kuu la Simba Maarufu tawi la Shujaa waliwasili kwenye tawi hilo lililopo pande za Mji Mpya majira ya saa 11 jioni.

 

Mara baada ya kunadi sera zake kwa wanachama hao Wakili Kaluwa aliruhusu wanachama hao kuuliza Maswali.

 

Mwanachama. Mgombea tumesikia sera zako maswali yangu ni mawili la kwanza ukifanikiwa kupata nafasi hiyo kubwa utaifanyia nini timu yetu? Swali langu la  Pili.

 

Wewe ni Wakili Muda mwingi uko Mahakamani utajigawa vipi kuitumikia Simba?.

 

Majibu ya Mgombea.

 

Kuhusu swali lako la kwanza kwamba nitaifanyia nini Simba nimeshajibu kwenye maelezo yangu ya awari nimetaja mambo ambayo nitaifanyia timu yetu.

 

Kuhusu swali la Pili kwamba nitajigawa vipi kweli mimi ni Wakili na umri wangu umeshasogea ninamiaka 55 naelekea 56 kwenye kazi ya uwakili ninamiaka 24 hivyo kwenye kazi hiyo ninauzowefu mkubwa hivyo najua nitajigawa vipi, pia kumbuka mimi sio mtendaji mkuu wa Klabu wako wasaidizi wangu wengi ambao kwa pamoja tutashirikiana kuijenga Simba yetu.

 

Swali la pili kutoka kwa Mwanachama Samora Mwarabu ambaye pia ni Makam mwenyekiti wa tawi hilo la Shujaa.

 

“Mgombea umemwaga sera zako nzuri zimenivutia sana nikuahidi tarehe 29 utapata kura yangu wasi wasi wangu ni kwamba mara nyingi kipindi hiki cha kampeni wagombea mnakuja hapa kutupa maneno matamu tukiwachagua mnapotea  mpaka kipindi cha uchaguzi mnakuja tena mbaya zaidi uongozi uliopita sisi wanachama tukiwapigia simu hawapokei  swali langu kwako utakuwa kiongozi wa namnagani?

 

Majibu ya Mgombea Kaluwa.

 

Kama ambavyo nimetangulia kusema kwenye maelezo yangu ya awari kwamba timu hii nitaejesha kwa wanachama pia nitatenga muda wa kutembelea matawi kujua kero zenu.

 

Mwanachama mwingine alipata nafasi ya kuliza Swali.

 

”Kwa sasa hatupati taarifa za timu yetu kwa wakati hali hiyo inapelekea kupata taarifa kwenye vyanzo vingine ambapo nyingi sio sahihi je ukipata ridhaa ya kutuongoza utakabiliana vipi na kero yetu hii.?

 

Majibu ya Mgombea Wakali

 Kaluwa.”Nitaboresha kitengo hicho cha habari na Mawasiliano ili wanachama mpate habari sahihi na kwa wakati.

 

Baada ya kujibu maswali hayo kiufasaha  Mgombea huyo aliketi na kumpa nafasi mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba ya Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Hamis’Don King’ alifunguka haya.

 

“Wanachama wenzangu tumchague Wakili kaluwa tuendelea kupata furaha sote ni mashahidi uongozi uliopo ukipiga simu kuliza habari  za timu yetu unapewa majibu ya hovyo unambiwa kachukue fomu  uongozi wewe sasa naomba tumchagua wakili Kaluwa kuondokana na hali hiyo”alisema Mwenyekiti huyo wa Matawi na kumalizi kwa kuwaombea kura wajumbe wengine wanaunda safu yao ya uongozi.

 

“ Kuna mgombea  kutoka hapa Morogoro anaitwa Abdallah Rashid Migomba akaniomba nimuombea kula yeye ni mzaliwa wa hapa hapa Morogoro kwa sasa anaishi Dar anagombea nafasi ya Ujumbe tumchague”alimalizia kusema Don King.

 

Baada ya mkutano huo kutamatika majira ya saa moja kasoro Wakili Kaluwa na wapambe wake waliingia kwenye Coater hizo mbili na kurejea jijini Dar.

 

Friday, January 20, 2023

MGOMBEA SIMBA ANADI SERA ZAKE AKIDAI SIMBA NI TIMU YA WOTE SIO WANACHAMA WA DAR PEKEE.









Mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba Mkoani Morogoro Said Mkwindapkulia] ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tawi la Shujaa akimpokea Mkombe wa nafasi ya Uwenyekiti wa Simba Mkao Makuu Wakili Moses Kaluwa





Mwenyekiti Mstaaru wa Simba Mzee Hassan Dalali akimpigia kampeni Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti Wakili Moses Kaluwa 5 Mgombea nafasi ya uwenyekiti wa timu ya Simba Wakili Moses Kaluwa akimwaga sera zake kwa wanachama wa tawi la simba Morogoro






Mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Hamis Maarufu Don King akihojiwa na Mtandao huu mara baada ya kukamilika kwa mkutano huo wa Kampeni.


 Msafara huo ukiondoka baada ya mgombea kumwaga sera kwenye tawi la Shujaa


 

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti Wakili Msomi Moses Kaluwa wakati akinadi sera zake kwa wanachama wa Simba  tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro Maarufu tawi la Shujaa.

 

Mbali na kauli  Mgombea huyo aliyetinga kwenye tawi hiyo na wapambe wake waliojaa kwenye Coaster mbili wakiongozwa na Mwenyekiti Mstaafu wa timu hiyo Mzee Hassan Dalali na Mwenyekiti wa Matawi yote ya Mkoa wa Dar Ramadhan Hamis Maarufu ‘Don King’amewashukia watu watu wanamzushia Uongo kwamba kwenye uongozi wake hamtaki Mwekezaji  tajiri Mohamed Dewji ‘MO.’

 

” Hizo ni Propaganda nyeusi ahadi yangu kwa wanasimba wakinipa ridhaa ya kuingoza timu yetu ahadi yangu kwenu nitamlinda Mwekezaji wetu mpaka dakika ya mwisho”alisema kwa Jazba Mwanasheria huyo na kuongeza kudadavua uzushi huo.

 

“ Nahisi kuna baadhi ya watu wamenielewa vibaya ninaposema timu nitaerejesha kwa wanachama, ninamaana kwamba kwa sasa inaonekana timu iko mbali na wanachama wa matawi hivyo kwenye uongozi wangu nitairejesha timu kwenye matawi kama ilivyokuwa nyuma kwenye uongozi wa Mzee Dalali.

 

 Mfano timu yetu inakuja kucheza hapa Morogoro nitahakikisha  inakuwa mikononi mwenu nyingi wanachama wa Morogoro ambao mnajua utamaduni wa Mkoa huu sisi wa Dar hatujui utamaduni wa Morogoro hilo ndilo lengo langu la kusema timu nitairejesha wa wanachama”alisemsa Wakili huyo na kupokea zawadi ya makofi mengi kutoka kwa wanachama wa tawi hilo la Shujaa. lfahamike kaika uchujo uliofanyw ana kamati ya uchaguzi kwenye nafasi ya Uonyekiti yamerejea majina mawili Wakili Moses Kaluwa na  Murtaza Magugu anayeshikilia nafasi hiyo aliyoinyakua kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika baada ya aliyekuwa mwenyekiti Sud Mkwabi kujiudhuru nafasi hiyo

 

Baada ya kumwaga sera zake nzuri Wakili Kaluwa aliruhusu maswali ambapo wanachama wengi walijitokeza kumuliza maswali magumu na mapesi.

Maswali na majibu hayo yataruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...