Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, January 26, 2023

MWANDISHI MORO PRESS CLUB ATEULIWA NA RAIS KUWA MKUU WA WILAYA YA SAME


 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Hongera sana Mwandishi wa habari mwenzangu hongera sana Mwanachama Mwenzangu wa Cha Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’Mh Kasilda Mgeni Mlimila kwa kuteuliwa Jana na Rais  Dkt  Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Same.

 

 lfahamike Mh Kasilda kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Tawala[DAS] takribani miaka 6 iliyopita alikuwa Mtangazaji wa Star Tv na Radio Free Afrika  Mkoa wa Morogoro, tukihangaika wote mtaani kusaka habari.

 

Nakumbuka baada ya kuteuliwa kuwa [DAS]nafasi hiyo ya uwakilishi wa Star Tv Mkoa wa Morogoro ulimkabidhi Nickson Mkilanya ambaye aliitumikia nafasi hiyo ya utangazaji kabla na yeye kuiacha ofisi hiyo ya Star Tv na kumwachia kijiti Mtangazaji wa sasa wa Star Tv Omary Hussein.

 

Kwa sasa Mkilanya ndiye Mwanyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro ambaye ndiye aliyesaini barua hii ya Pongezi kwa Mwanachama wake na Mfanyakazi mwenzie wa Star Tv.

 

Mh Kaslda mara nyingi huwa napita hapo Same kwenda Moshi na Arusha kwa ndugu zangu hivyo hapana shaka yoyote nikipita hapo nitakupigia simu tuonane uso kwa macho nikupe pongezi zangu Live a.k.a Mubashara kwa sasa pokea Pongezi hizi kupitia kwenye Mtandao huu pendwa wa Shekidele ambapo wewe pia ni mdau mkubwa wa Mtandao huu.

 

Vigogo wengine niliowahi kufanya nao kazi ya Uandishi wa habari Mkoani Morogoro waliotimkia kwenye siasa na sasa ni Mastaa nchini Tanzania ni pamoja na  Mtangazaji wa ITV na Radio One Mkoa wa Morogoro Devotha Minja aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa leseni ya Chadema ambaye pia ni Mwanachama hai wa Morogoro Press Club.

 

Mwingine Mwandishi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalengo Mkoa wa Morogoro Esther Bulaya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM kabla ya kutimkia Chadema na kufanikiwa kumbwaga  aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Bunda  Mzee Wasira kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

 

Kwa sasa Esther na wenzake 18 wanaounda timu ya wabunge 19 wa Viti Maalumu walivyovinyakua kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka 2020 kupitia Chadema wakiongozwa na Madam Halima Mdee wako kwenye kesi Mahakamani na chama chao cha Chadema huhusiana na ubunge wao huo wa kuteuliwa.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...