Mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba Mkoani Morogoro Said Mkwindapkulia] ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tawi la Shujaa akimpokea Mkombe wa nafasi ya Uwenyekiti wa Simba Mkao Makuu Wakili Moses Kaluwa
Mwenyekiti Mstaaru wa Simba Mzee Hassan Dalali akimpigia kampeni Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti Wakili Moses Kaluwa 5 Mgombea nafasi ya uwenyekiti wa timu ya Simba Wakili Moses Kaluwa akimwaga sera zake kwa wanachama wa tawi la simba Morogoro
Mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Hamis Maarufu Don King akihojiwa na Mtandao huu mara baada ya kukamilika kwa mkutano huo wa Kampeni.
Msafara huo ukiondoka baada ya mgombea kumwaga sera kwenye tawi la Shujaa
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Kauli hiyo imetolewa na Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti Wakili Msomi Moses Kaluwa wakati akinadi sera zake kwa wanachama wa Simba tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro Maarufu tawi la Shujaa.
Mbali na kauli Mgombea huyo aliyetinga kwenye tawi hiyo na wapambe wake waliojaa kwenye Coaster mbili wakiongozwa na Mwenyekiti Mstaafu wa timu hiyo Mzee Hassan Dalali na Mwenyekiti wa Matawi yote ya Mkoa wa Dar Ramadhan Hamis Maarufu ‘Don King’amewashukia watu watu wanamzushia Uongo kwamba kwenye uongozi wake hamtaki Mwekezaji tajiri Mohamed Dewji ‘MO.’
” Hizo ni Propaganda nyeusi ahadi yangu kwa wanasimba wakinipa ridhaa ya kuingoza timu yetu ahadi yangu kwenu nitamlinda Mwekezaji wetu mpaka dakika ya mwisho”alisema kwa Jazba Mwanasheria huyo na kuongeza kudadavua uzushi huo.
“ Nahisi kuna baadhi ya watu wamenielewa vibaya ninaposema timu nitaerejesha kwa wanachama, ninamaana kwamba kwa sasa inaonekana timu iko mbali na wanachama wa matawi hivyo kwenye uongozi wangu nitairejesha timu kwenye matawi kama ilivyokuwa nyuma kwenye uongozi wa Mzee Dalali.
Mfano timu yetu inakuja kucheza hapa Morogoro nitahakikisha inakuwa mikononi mwenu nyingi wanachama wa Morogoro ambao mnajua utamaduni wa Mkoa huu sisi wa Dar hatujui utamaduni wa Morogoro hilo ndilo lengo langu la kusema timu nitairejesha wa wanachama”alisemsa Wakili huyo na kupokea zawadi ya makofi mengi kutoka kwa wanachama wa tawi hilo la Shujaa. lfahamike kaika uchujo uliofanyw ana kamati ya uchaguzi kwenye nafasi ya Uonyekiti yamerejea majina mawili Wakili Moses Kaluwa na Murtaza Magugu anayeshikilia nafasi hiyo aliyoinyakua kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika baada ya aliyekuwa mwenyekiti Sud Mkwabi kujiudhuru nafasi hiyo
Baada ya kumwaga sera zake nzuri Wakili Kaluwa aliruhusu maswali ambapo wanachama wengi walijitokeza kumuliza maswali magumu na mapesi.
Maswali na majibu hayo yataruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment