Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, January 21, 2023

UKAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU SIMBA MGOMBEA APANGUA MASWALI YA WANACHAMA.

Mbombea nafasi ya Uwenyekiti wa Klabu ya Simba  Wakili Moses Kaluwa akimwaga sera zake kwa wanachma wa timu hiyo tawi la Shujaa Morogoro juzi jioni
...Mgombea huyo akijibu Maswali ya wanachama hao



 


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mgombea nafasi ya Uwenyekiti wa timu ya Simba Wakili Moses Kaluwa juzi alipangua kiufasaha Maswali  ya wanachama wa tawi kuu la Simba la Mkoani Morogoro kwenye mkutano wa kampeni.

 

Wakili Kaluwa aliyeasindikizwa na wapambe wake waliojaa Coaster Mbili walipotoka Dar walipita Moro Mjini wakaelekea tawi la Simba la Dumila baadae wakageuka wakarejea Moro Mjini kwenye tawi kuu la Simba Maarufu tawi la Shujaa waliwasili kwenye tawi hilo lililopo pande za Mji Mpya majira ya saa 11 jioni.

 

Mara baada ya kunadi sera zake kwa wanachama hao Wakili Kaluwa aliruhusu wanachama hao kuuliza Maswali.

 

Mwanachama. Mgombea tumesikia sera zako maswali yangu ni mawili la kwanza ukifanikiwa kupata nafasi hiyo kubwa utaifanyia nini timu yetu? Swali langu la  Pili.

 

Wewe ni Wakili Muda mwingi uko Mahakamani utajigawa vipi kuitumikia Simba?.

 

Majibu ya Mgombea.

 

Kuhusu swali lako la kwanza kwamba nitaifanyia nini Simba nimeshajibu kwenye maelezo yangu ya awari nimetaja mambo ambayo nitaifanyia timu yetu.

 

Kuhusu swali la Pili kwamba nitajigawa vipi kweli mimi ni Wakili na umri wangu umeshasogea ninamiaka 55 naelekea 56 kwenye kazi ya uwakili ninamiaka 24 hivyo kwenye kazi hiyo ninauzowefu mkubwa hivyo najua nitajigawa vipi, pia kumbuka mimi sio mtendaji mkuu wa Klabu wako wasaidizi wangu wengi ambao kwa pamoja tutashirikiana kuijenga Simba yetu.

 

Swali la pili kutoka kwa Mwanachama Samora Mwarabu ambaye pia ni Makam mwenyekiti wa tawi hilo la Shujaa.

 

“Mgombea umemwaga sera zako nzuri zimenivutia sana nikuahidi tarehe 29 utapata kura yangu wasi wasi wangu ni kwamba mara nyingi kipindi hiki cha kampeni wagombea mnakuja hapa kutupa maneno matamu tukiwachagua mnapotea  mpaka kipindi cha uchaguzi mnakuja tena mbaya zaidi uongozi uliopita sisi wanachama tukiwapigia simu hawapokei  swali langu kwako utakuwa kiongozi wa namnagani?

 

Majibu ya Mgombea Kaluwa.

 

Kama ambavyo nimetangulia kusema kwenye maelezo yangu ya awari kwamba timu hii nitaejesha kwa wanachama pia nitatenga muda wa kutembelea matawi kujua kero zenu.

 

Mwanachama mwingine alipata nafasi ya kuliza Swali.

 

”Kwa sasa hatupati taarifa za timu yetu kwa wakati hali hiyo inapelekea kupata taarifa kwenye vyanzo vingine ambapo nyingi sio sahihi je ukipata ridhaa ya kutuongoza utakabiliana vipi na kero yetu hii.?

 

Majibu ya Mgombea Wakali

 Kaluwa.”Nitaboresha kitengo hicho cha habari na Mawasiliano ili wanachama mpate habari sahihi na kwa wakati.

 

Baada ya kujibu maswali hayo kiufasaha  Mgombea huyo aliketi na kumpa nafasi mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba ya Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Hamis’Don King’ alifunguka haya.

 

“Wanachama wenzangu tumchague Wakili kaluwa tuendelea kupata furaha sote ni mashahidi uongozi uliopo ukipiga simu kuliza habari  za timu yetu unapewa majibu ya hovyo unambiwa kachukue fomu  uongozi wewe sasa naomba tumchagua wakili Kaluwa kuondokana na hali hiyo”alisema Mwenyekiti huyo wa Matawi na kumalizi kwa kuwaombea kura wajumbe wengine wanaunda safu yao ya uongozi.

 

“ Kuna mgombea  kutoka hapa Morogoro anaitwa Abdallah Rashid Migomba akaniomba nimuombea kula yeye ni mzaliwa wa hapa hapa Morogoro kwa sasa anaishi Dar anagombea nafasi ya Ujumbe tumchague”alimalizia kusema Don King.

 

Baada ya mkutano huo kutamatika majira ya saa moja kasoro Wakili Kaluwa na wapambe wake waliingia kwenye Coater hizo mbili na kurejea jijini Dar.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...