Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, January 29, 2023

BARAKA ZA MUNGU NYUMBANI.






 

UJUMBE WA NENO LA MUNGU

SOMO KUTOKA.

 

ZABURI. 127.1-5

 


 

BWANA asipoijenga nyumba waijengao wafanyakazi bure.

 

Bwana asipoulinda Mji yeye aulindaye akesha bure.

 

Kazi yenu ni bure Mnaoamka mapema na kukawia kwenda kulala na kula chakula cha taabu,yeye humpa Mpenzi wake usingizi,

 

Tazama wana ndio Urithi wa Bwana Uzao wa tumbo ni dhawabu.

 

Kama Mishale Mkononi mwa Shujaa ndivyo walivyo wana wa Ujanani.

 

Heri mtu yule aliyelijaza podo lake hivyo.

 

Naam,hawataona aibu wanaosema na adui langoni” Hilo ndilo leno la MUNGU Jumapili ya leo January 29.

 UCHAMBUZI WA NENO HILO UNALETWA KWAKO NA DUSTAN SHEKIDELE.

Soma hapo juu linasema Bwana asipoijenga nyumba wajengao wafanyakazi bure.

 

 Somo hilo pia linasema Bwana asipoulinda mji waulindao wakesha bure.

 

Tumeshuhudia baadhi ya watu wakijenga nyumba zao nzuri kwa kujaliwa kipato na Mwenyezi Mungu.

 

Chakushangaza baada ya kuhamia kwenye nyumba hizo wanafanya sherehe za watu kuywa pombe usiku kucha na baadae wanafukia mapembe kama zindiko la nyumba hiyo.

 

Jambo hilo ni chukizo kubwa Mbele za Mungu.

 

Kuna baadhi ya watu wenye ufahamu wanapopata Neema ya kujenga nyumba wanapohamia  humwalika Kiongozi wa dini kuja kufanya maombi au dua hiyo baada ya maombi na dui hiyo kukamilika mmiliki wa nyumba hiyo hutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu kwa kumjalia kupata nyumba hiyo.

 

Wengine wameamua kufanya matendo mema zaidi kwa kuruhusu nyumba ya lbada kujengwa  nje ya nyumba zao  kama alivyofanya Mwandishi wa Mtandao huu.

 

Kama hiyo haitoshi Mungu anasema yeye asipokaribishwa na mwenye nyumba kulinda mji  walinzi aliowaajiri wamlinde wana kesha bure.

 

Tumeshuhudia baadhi ya nyumba za matajiri zinalindwa na walinzi wenye silaha nzito,ndani ya uzi kuna Mbwa wenye mafunzo wa kijeshi,  kwenye uzio kuna nyaya za umeme za kuzuia waharifu kuluka ukuta, kwenye nyumba hiyo hiyo kuna kamera za ulinzi ‘CCTV Camera’

 

 Licha ya ulinzi wote huo utastaajabu kukicha unaambiwa mmiliki wa nyumba hiyo amefariki dunia  chumbani  akiwa kwenye uzingizini mzito na chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa shinikizo la damu’Presha’

 

Hapo ndipo kauli ya Mungu inapodhihirisha kwamba usipomwalika yeye kuulinda Mji wako  waulindao wakesha bure.

 

Nilichojifunza mimi kwenye somo hili tusijivunie na haya Maboma[Nyumba]tukamsahamu Mungu au  yakatupa kiburi cha kuwanyanyasa na kuwadharau watu wengine wakiwemo wapangaji wetu.

 

 Tukumbuke tutakufa tutayaacha haya Maboma hata yawe mazuri kisiasi gani hatutakwenda nayo kaburini.

 

 Kwa Wakristo tutakwenda kaburini na sanduku la pembe nne na watu wa dini nyingine watakwenda kaburini na vipande vitatu vya sanda.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...