Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, February 28, 2022

KUMBUKIZI. HABARI YA KIJAMII


 


Bw Athuman Rajab akishika tama kwa uchungu akiwa nje ya nyumba yake baada ya mkewe kufariki dunia akidaiwa kuteleza na kutumbukia kwenye kisima cha Maji Kijiji cha Dakawa Wilaya ya Mvomero Mkoa Morogoro. 
 
Baada ya kutokea kwa tukio hilo Mwaka 2012 Mwandishi wa habari hizi alipiga gia Pikipiki yake aina ya Honda 110[Pichani] na kutinga kwenye kijijini hicho na kufanikiwa kuzungumza na Mume Marehemu ambaye alifunguka Mazito.

Saturday, February 26, 2022

KUMBUKIZI.KAMPENI ZA UCHAGUZI 2015 MORO.



 


Wagombea  Uras  John Pombe Magufuli wa CCM na Edward Lowassa wa UKAWA walipotinga Mkoa Morogoro kwa nyakati tofauti kwenye  Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kuomba Kura.

  Lowassa[kulia] akisoma gazeti na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Mkoani Morogoro Muda mfupi kabla ya mkutano wa kampeni kuanza.

 

Mawaziri hao Wakuu wastaafu kwa sasa Wamerejea CCM.

 

Picha no 2 Rais  Mstaafu Jakaya Kikwete akiteta jambo na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM  Mzee Yusuf Makamba’Mgosi’ kwenye Mkutano wa Kampenzi uliofanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro, Vigogo hao wa CCM walitinga kwenye Mkutano huo kumnada Mgombea wao wa Urais Marehemu John Pombe  Josef Magufuri’JPM.’

Katika uchaguzi huo Marehemu Magufuri aliibuka kidedea huku Lowassa akiambulia nafasi ya Pili. Picha na Dunstan Shekidele,

Thursday, February 24, 2022

KUMBUKIZI.BAHATI BUKUKU AMPAGAWISHA MLEMAVU

Mlemavu akienda kumtunza Bahati Bukuku baada ya kuguswa na mahudhui ya wimbo wa Dunia haina hurumam uliotungwana na kuimbwa na Msanii huyo wa Muziki wa lnjiri nchini
Bahati Bukuku akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu
 


Mwimbaji nyota wa muziki wa lnjiri nchini Bahati Bukuku.amempagawisha Mlemavu na wimbo wake wa ‘Dunia haina huruma.

’ Mara baa ya kuimba wimbo huo kwenye tamasha la lnjri lililofanyika mwaka 2013 Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mlemavu huyo alishindwa kujizuia na kupanda jukwaa na kumtunza Pesa Bahati Bukuku’Double B’

Tuesday, February 22, 2022

KUMBIKIZI. PAPARAZI AMGARAGAZA BINGWA WA DISCO AFRIKA MASHARIKI NA KATI





 


Na Mwandishi Wetu Morogoro.
Mwandishi wa mtandao huu Dustan Shekidele'Mkude Simba' Kulia' amefanikiwa kutwaa ubingwa wa kucheza disko baada ya kumshinda bingwa wa kucheza disko Afrika Mashariki na Kati Maneno Ngedere'Super Ngedere'
 
Mpamabo huo ulioandaliwa na Ukumbi wa Air Port Classic uliopewa jina la ‘Nani Mkali’ ulioshuhudia na umati mkubwa wawatu kilele cha sikuu ya Wapendanao Duniani ‘Valentine’ Mwaka 2017.kwenye ukumbi wa Air Port uliopo Pande za Mazimbu Jirani na uwanja wa Ndege wa Morogoro. 
 
Wawili hao waligongewa Sebene kavu kavu na Band ya Waluguru Original ambapo kila mmoja alisaka maksi kwa Style mbali mbali za uchezaji.
 
lkumbukwe Super Ngedere ni kaka wa damu wa Asha Ngedere aliyekuwa akiigizwa na kundi la Original Komedy ambapo Asha alikuwepo kwenye ukumbi huo alishuhudia kaka yake aligaragazwa na Paparazi wa Mtandao. 
 
Mara baada ya kutwaa Ubingwa huo Shekidele alikabidhiwa katoni ya Soda na Jaji Mkuu wa Mpambano huo lbrahim ldd ambaye pia ni Mc Maarufu Mkoani Morogoro akitumia jina la Mc Mluguru Mweupe’

Sunday, February 20, 2022

KWELI NIMEAMINI MAMA NI MLEZI WA WOTE.

 Rais Samia Suluhu Hassan Kulia akizungumza na Tundu Lissu

 


 Na Dunstan Shekidele,Morogoro

Rais  Samia Suluhu Hassan ‘Maarufu Mama Samia’ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi’CCM’  February 12 amemtembelea na kumjulia hali Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzania Tanzania Chedema Mh Tundu Lissu  Jijini Brussels nchini Ubelgiji.

Kwa  miaka kadhaa sasa Mh Lissu  yuko nchini Ubelgiji alikokwenda kupatiwa matibabu baada ya kupigwa Risasi nyingi mwili na watu wasiojulikani wakati akitoka Bungeni Dodoma akirejea nyumbani kwake. 

 

Kwa siku kadhaa Mama Samia alikuwa kwenye Ziara ya kikazi barani Ulaya, hivyo alitumia fursa hiyo kukutana na watanzania wanaoishi kwenye nchini alizotembelea akiwemo Mh Lissu.

Nani Kama Mama?

Saturday, February 19, 2022

UJUMBE WA LEO JUMAPILI


 

YEREMIA 1-19
:"Nao watapigana nawe lakini hawatakushinda.Maana mimi nipo pamoja nawe, Asema BWANA ili nikuokoe".
Hilo ndio neno letu la leo Jumapili

Thursday, February 17, 2022

KIKOSI CHA SIMBA CHA MWAKA 1989


 

Marehemu Adama Selemani'TATA' wanne kutoka kushoto waliochuchumaa akiwa na kikosi cha Simba 
.
Hiki ni kikosi cha Simba cha Mwaka 1989. 
 
Picha kwa hisani ya mchezaji mmoja wa Simba aliyecheza na Marehemu Adam.

TANZIA. MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA

Marehemu Adam Selemani enzi za Uhai wake akipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu akiwa na jezi yake ya Moro Veterani
Marehemu Adam akiwa na Mtoto wake wa mwisho Miraj wakati huo dogo huyo akiitumikia Simba.

 Amin Adam Maarufu Minah Munasiry msemaji wa familia aliyeongeza na Mwandishi wa habari hizi.

.
                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
BEKI kisiki wa zamani wa timu ya Simba Adam Seleman’TATA’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
 
Marehemu Adam ambaye hadi mauti inamkuta alikuwa Mwanachama na Mchezaji wa timu ya Morogoro Veterani.
Alifikwa na umauti akiwa nyumbani Tanga akiendelea na matibabu baada ya kuugua kwa miezi kadhaa mkoa hapa na ndugu zake kuamua kumchua na kumpeleka kwa Tanga. 
 
Jana Majira ya Saa 10 usiku Amina Adam Selema ambaye ni mtoto wa pili kutoka mwisho wa Marehemu aliyeacha watoto 6 alimpigia simu Mwandishi wa Mtandao huu na kumjuza taarifa za kifo cha Mpendwa baba yake.
 
” Shekidele juzi nilipotoka nyumbani Tabora kuja huku Tanga kumuona baba nililala hapo Moro nikakuomba namba za Viongozi wenu wa Moro Veterani nashukuru niliwapigia wakanipa ushirikiano mzuri lakini nasigitika kukueleza kwamba Mzee wangu amefariki usiku huu”alisema Amina na kuangua Kilio.
 
Kulipokucha Mwandishi wa habari hizi alimpigia tena Amina ambapo alipotakiwa kuelezea taratibu za mazishi alisema
” Baba amefia Tanga Mjini leo tunasafirisha mwili kuelekea kijijini Kwetu Muheza na mazishi yatafanyika Kesho baada ya Swala ya ljumaa”alisema Amin.
 
            WASIFU WA MAREHEMU KIMICHEZO
 
. Marehemu Adamu alisajiriwa na Reli ya Morogoro ikiwa ligi kuu akitokea timu ya Muheza Shooting Stars ya Muheza, baadae Simba nao wakavutiwa na Kiwango chake wakamsajiri na mara kadhaa aliitumikia timu ya Taifa ya Tanzania. 
 
Marehemu adam alipoacha kuitumikia Simba alireja Mkoani Morogoro akishi maeneo ya Mji Mpya na kujiunga na timu ya wachezaji vyota wa zamani Moro Veterani aliyoitumikia mpaka kifo kinamkuta Mwandishi wa Mtandao habari hizi pia ni mchezaji wa Moro Veterani. 
 
Marehemu ameacha watoto 6 wakike 5 na wa Kiume 1.
Mwanaye huyo pekee wa kiume ambaye ni kitinda Mimba’Wa mwisho Kumzaa’alifuata nyayo za baba yake za kutandaza kabumbu. 
 
Miraji Adam alianza Moro Kids baadae akajiunga na Simba akiwa beki wa kutumainiwa kwenye gemu ya Simba na JKT Mgambo uwanja wa Mkapa alivunjika Mguu kwenye hemu hiyo iliyotamatika kwa ‘Wanajeshi hao kutoka Tanga walipokea kichapo cha bao 6-0.
Mchezaji huyo aliuguza jeraha hilo kwa muda Mrefu,hali iliyopelekea Simba kumtema kwenye kikosi chao.
 
Mungu ni mwema Miraji alipopona akajiunga na Coastal Union ya Tanga.akaitumikia kwa misimu miwili kabla ya kutimkia Singida United wakati huo ikiwa ya Moto timu hiyo alivyosambaratika Miraj naye akapoteza mwerekeo wa Soka na Mara kadhaa Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia kwenye Michezo ya Ndondo Cup uwanja wa Saba saba Morogoro.
 
" Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 'tangulia kamanda tutaonana baadaye'



Tuesday, February 15, 2022

KUMBIKIZI. TAJIRI SHABIBY AZUNGUKWA NA MAPAPARAZI


 


Waandishi nguri wa habari Mkoa Morogoro, Ratifa Ganzeri[Kulia]anayeandikia gazeti ya Uhuru na Liliani Lucas Kasenene Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi[Kati] wakiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mh Ahmed Shabiby. 
 
Mastaa hao walinaswa na Kamera za Mtandao huu Mwaka 2012 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro’lkuru Ndogo’ kwenye shughuri ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wilaya wapya wa Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete. 
 
Kwa sasa Ratifa ni Diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM na Lili ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa habari Tanzania. 
 
Kwa Upande wa Shabiby kama kawa yeye ni Mmiliki wa Kampuni ya Mabasi ya Shabiby Line akimiliki pia Hotel kubwa katika Mikoa ya Dodoma na Morogoro pia ni Mbunge wa Jimbo la Gairo kwa Vipindi 4 mfururizo toka Mwaka 2005 Mpaka sasa.
 
Hii ni kwa sababu ya kukubarika kwake na wananchi wa Jimbo hilo waliompachika jina la Rais wa Gairo.
Wakati huo Lili na Ratifa walikuwa bado hawajaanza heka heka zao za kuseti Nywele kama wanavyooneka Kichwania 'simpo' ukibahatika kuwaona sasa hivi wawili hao ni Warembo haswaa kama Malaika

Monday, February 14, 2022

ISHU YA MAITI KUZIKKWA MARAMBI MKE WA MAREHEMU AFUNGUKA


 

EXCLUSIVE
ISHU ya Maiti kudaiwa kuchanganywa chumba na kuhifadhi Maiti hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyopelekea kaburi kufukuriwa na Maiti kuzikwa mara ya pili,mke wa Marehemu afunguka Mazito.
 
Jana Mtandao huu umefanikiwa kuzungumza na Bi Patricia Marck ‘Mrs Mkude’.huku akidai baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti tufauti tukio la Mpendwa Mume wake kuzikwa mara mbili hivyo kupitia Mtandao huu amejariku kuweka sawa jambo hilo. 
 
Nini amesema endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote

MORO KIDS WA UBINGWA WA MDFA CUP.

Makamo Mwenyekiti wa MDFA Masoud  Gumbwa akikabidhi Kombe na Jezi Nahodha wa Moro Kids Geofrey Mmasi.

               Wachezaji wa Moro Kids wakishangilia Ubingwa.

  Nahodha wa Chamwino Youth Felix Sekwini akipokea zawadi ya Mipita 2 Kinyonge


                           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Moro Kids’Watoto wa Moro’ juzi ilifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Michuano ya MDFA iliyoandaliwa na Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’. 

 

Moro Kids’ walitwaa ubingwa huo baada ya kuichapa timu ngumu ya Chamwino Youth’Vijana wa Chamwino’ kwa Pelnat 5-4 baada ya Miamba hiyo kutoka sale ya bao 1-1  dakika 90 za mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Saba saba  Mkoani hapa.

Chamwino walijipatia bao lao Mapema dakika za 11 huku Moro wakichumoa dao hilo dakika za lala buriani,dakika ya 84  walipoingia kwenye changamoto ya Mikwaju ya Pelnat Chamwino walikosa Pelnat Moja iliyopanguliwa na Kipa wa Moro Geofrey Mmasi huku Moro  wakifunga Pelnat zote tano.

Fainali hiyo iliyolala zaidi ya miezi 4 ilipigwa juzi huku kiporo hicho cha fainali kikitajwa pia kama kiashiria cha Uzinduzi wa Ligi ya Taifa daraja la nne Wilaya ya Morogoro, Bigwa ya Fainali hiyo alikabidhiwa swti ya Jezi na Kikombe huku mshindi wa Pili Chamwino akiambulia zawadi ya Mipira 2.

               


MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...