Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, February 15, 2022

KUMBIKIZI. TAJIRI SHABIBY AZUNGUKWA NA MAPAPARAZI


 


Waandishi nguri wa habari Mkoa Morogoro, Ratifa Ganzeri[Kulia]anayeandikia gazeti ya Uhuru na Liliani Lucas Kasenene Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi[Kati] wakiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mh Ahmed Shabiby. 
 
Mastaa hao walinaswa na Kamera za Mtandao huu Mwaka 2012 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro’lkuru Ndogo’ kwenye shughuri ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wilaya wapya wa Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete. 
 
Kwa sasa Ratifa ni Diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM na Lili ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa habari Tanzania. 
 
Kwa Upande wa Shabiby kama kawa yeye ni Mmiliki wa Kampuni ya Mabasi ya Shabiby Line akimiliki pia Hotel kubwa katika Mikoa ya Dodoma na Morogoro pia ni Mbunge wa Jimbo la Gairo kwa Vipindi 4 mfururizo toka Mwaka 2005 Mpaka sasa.
 
Hii ni kwa sababu ya kukubarika kwake na wananchi wa Jimbo hilo waliompachika jina la Rais wa Gairo.
Wakati huo Lili na Ratifa walikuwa bado hawajaanza heka heka zao za kuseti Nywele kama wanavyooneka Kichwania 'simpo' ukibahatika kuwaona sasa hivi wawili hao ni Warembo haswaa kama Malaika

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...