Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, February 14, 2022

MORO KIDS WA UBINGWA WA MDFA CUP.

Makamo Mwenyekiti wa MDFA Masoud  Gumbwa akikabidhi Kombe na Jezi Nahodha wa Moro Kids Geofrey Mmasi.

               Wachezaji wa Moro Kids wakishangilia Ubingwa.

  Nahodha wa Chamwino Youth Felix Sekwini akipokea zawadi ya Mipita 2 Kinyonge


                           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Moro Kids’Watoto wa Moro’ juzi ilifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Michuano ya MDFA iliyoandaliwa na Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’. 

 

Moro Kids’ walitwaa ubingwa huo baada ya kuichapa timu ngumu ya Chamwino Youth’Vijana wa Chamwino’ kwa Pelnat 5-4 baada ya Miamba hiyo kutoka sale ya bao 1-1  dakika 90 za mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Saba saba  Mkoani hapa.

Chamwino walijipatia bao lao Mapema dakika za 11 huku Moro wakichumoa dao hilo dakika za lala buriani,dakika ya 84  walipoingia kwenye changamoto ya Mikwaju ya Pelnat Chamwino walikosa Pelnat Moja iliyopanguliwa na Kipa wa Moro Geofrey Mmasi huku Moro  wakifunga Pelnat zote tano.

Fainali hiyo iliyolala zaidi ya miezi 4 ilipigwa juzi huku kiporo hicho cha fainali kikitajwa pia kama kiashiria cha Uzinduzi wa Ligi ya Taifa daraja la nne Wilaya ya Morogoro, Bigwa ya Fainali hiyo alikabidhiwa swti ya Jezi na Kikombe huku mshindi wa Pili Chamwino akiambulia zawadi ya Mipira 2.

               


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...