Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, February 22, 2022

KUMBIKIZI. PAPARAZI AMGARAGAZA BINGWA WA DISCO AFRIKA MASHARIKI NA KATI





 


Na Mwandishi Wetu Morogoro.
Mwandishi wa mtandao huu Dustan Shekidele'Mkude Simba' Kulia' amefanikiwa kutwaa ubingwa wa kucheza disko baada ya kumshinda bingwa wa kucheza disko Afrika Mashariki na Kati Maneno Ngedere'Super Ngedere'
 
Mpamabo huo ulioandaliwa na Ukumbi wa Air Port Classic uliopewa jina la ‘Nani Mkali’ ulioshuhudia na umati mkubwa wawatu kilele cha sikuu ya Wapendanao Duniani ‘Valentine’ Mwaka 2017.kwenye ukumbi wa Air Port uliopo Pande za Mazimbu Jirani na uwanja wa Ndege wa Morogoro. 
 
Wawili hao waligongewa Sebene kavu kavu na Band ya Waluguru Original ambapo kila mmoja alisaka maksi kwa Style mbali mbali za uchezaji.
 
lkumbukwe Super Ngedere ni kaka wa damu wa Asha Ngedere aliyekuwa akiigizwa na kundi la Original Komedy ambapo Asha alikuwepo kwenye ukumbi huo alishuhudia kaka yake aligaragazwa na Paparazi wa Mtandao. 
 
Mara baada ya kutwaa Ubingwa huo Shekidele alikabidhiwa katoni ya Soda na Jaji Mkuu wa Mpambano huo lbrahim ldd ambaye pia ni Mc Maarufu Mkoani Morogoro akitumia jina la Mc Mluguru Mweupe’

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...