Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, February 17, 2022

TANZIA. MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA

Marehemu Adam Selemani enzi za Uhai wake akipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu akiwa na jezi yake ya Moro Veterani
Marehemu Adam akiwa na Mtoto wake wa mwisho Miraj wakati huo dogo huyo akiitumikia Simba.

 Amin Adam Maarufu Minah Munasiry msemaji wa familia aliyeongeza na Mwandishi wa habari hizi.

.
                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
BEKI kisiki wa zamani wa timu ya Simba Adam Seleman’TATA’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
 
Marehemu Adam ambaye hadi mauti inamkuta alikuwa Mwanachama na Mchezaji wa timu ya Morogoro Veterani.
Alifikwa na umauti akiwa nyumbani Tanga akiendelea na matibabu baada ya kuugua kwa miezi kadhaa mkoa hapa na ndugu zake kuamua kumchua na kumpeleka kwa Tanga. 
 
Jana Majira ya Saa 10 usiku Amina Adam Selema ambaye ni mtoto wa pili kutoka mwisho wa Marehemu aliyeacha watoto 6 alimpigia simu Mwandishi wa Mtandao huu na kumjuza taarifa za kifo cha Mpendwa baba yake.
 
” Shekidele juzi nilipotoka nyumbani Tabora kuja huku Tanga kumuona baba nililala hapo Moro nikakuomba namba za Viongozi wenu wa Moro Veterani nashukuru niliwapigia wakanipa ushirikiano mzuri lakini nasigitika kukueleza kwamba Mzee wangu amefariki usiku huu”alisema Amina na kuangua Kilio.
 
Kulipokucha Mwandishi wa habari hizi alimpigia tena Amina ambapo alipotakiwa kuelezea taratibu za mazishi alisema
” Baba amefia Tanga Mjini leo tunasafirisha mwili kuelekea kijijini Kwetu Muheza na mazishi yatafanyika Kesho baada ya Swala ya ljumaa”alisema Amin.
 
            WASIFU WA MAREHEMU KIMICHEZO
 
. Marehemu Adamu alisajiriwa na Reli ya Morogoro ikiwa ligi kuu akitokea timu ya Muheza Shooting Stars ya Muheza, baadae Simba nao wakavutiwa na Kiwango chake wakamsajiri na mara kadhaa aliitumikia timu ya Taifa ya Tanzania. 
 
Marehemu adam alipoacha kuitumikia Simba alireja Mkoani Morogoro akishi maeneo ya Mji Mpya na kujiunga na timu ya wachezaji vyota wa zamani Moro Veterani aliyoitumikia mpaka kifo kinamkuta Mwandishi wa Mtandao habari hizi pia ni mchezaji wa Moro Veterani. 
 
Marehemu ameacha watoto 6 wakike 5 na wa Kiume 1.
Mwanaye huyo pekee wa kiume ambaye ni kitinda Mimba’Wa mwisho Kumzaa’alifuata nyayo za baba yake za kutandaza kabumbu. 
 
Miraji Adam alianza Moro Kids baadae akajiunga na Simba akiwa beki wa kutumainiwa kwenye gemu ya Simba na JKT Mgambo uwanja wa Mkapa alivunjika Mguu kwenye hemu hiyo iliyotamatika kwa ‘Wanajeshi hao kutoka Tanga walipokea kichapo cha bao 6-0.
Mchezaji huyo aliuguza jeraha hilo kwa muda Mrefu,hali iliyopelekea Simba kumtema kwenye kikosi chao.
 
Mungu ni mwema Miraji alipopona akajiunga na Coastal Union ya Tanga.akaitumikia kwa misimu miwili kabla ya kutimkia Singida United wakati huo ikiwa ya Moto timu hiyo alivyosambaratika Miraj naye akapoteza mwerekeo wa Soka na Mara kadhaa Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia kwenye Michezo ya Ndondo Cup uwanja wa Saba saba Morogoro.
 
" Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 'tangulia kamanda tutaonana baadaye'



No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...