Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, December 31, 2022

SEHEMU YA 3 MAKALA MAALUMU MANISPAA YA MORO KUWA JIJI. MKURUGENZI NA RPC WAFUNGUKA.

  

Mwandishi wa Mtandao huu akizungumza na RPC Muslimu.



 Kulia Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Ally Machelle.


 

Na Dunstan Shekidele, Morogoro.

 

KWA takribani wiki moja sasa Mwandishi wa Mtandao huu amejikita kufanya uchunguzi Maalumu wa kuelekea Manispaa ya Morogoro kuwa Jiji.

 

 Mengi yameelezewa kwenye Stori za nyuma ambazo bado ziko kwenye Mtandao huu Pendwa nchini na kwamba stori ya Mwisho Mwandishi  aliahadi kuwatafuta Mkurugenzi wa Manispaa na Kamanda wa Polisi;RPC’ kwa lengo la kuwahoji vigogo hao ili watupatie majawabu ya baadhi ya kero zinazoendelea kwenye Manispaa hiyo.

 

Jana Mwandishi huyo wa habari xa kiuchunguzi aliwasaka Vigogo hao na kufanikiwa kuwapata wa kwanza kupatikana alikuwa RPC Fortunatus Musilim  alipoelezwa kero ya Bajaj kupakia na kushusha abiri maeneo ya sio lasimi ikiweno ndani ya kituo cha Mafuta.

 

Big boss huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro alisema, “ Ni kweli  hali hiyo ilitokea siku za nyuma tukazungumza na madereva hao wa Bajaj kuhusiana na kushusha na kipakia abiria walitueleza kwamba pale kituo cha mafuta wanaingia kujaza mafuta tu na sio kushusha na kupakia abiri.

 

 Kamanda huyo alipoulizwa kama sheria inaruhusu chombo cha Moto kujaza mafuta abiria wakiwa ndani RPC Musilim alijibu” Hiyo hairuhusiwi nikuombe shekidele uniachie swala hili nitalifanyia kazi”alijibu Kamanda huyo.

 

Baada ya kutoka kwa RPC Mtandao huu ulitinga kwa Mkurugenzi wa Manispaa Ally Machela na mahojianoi yalikuwa hivi.

 

Mwandishi- Pole na majukumu ya kujenga taifa letu bosi.

Mkurugenzi. Asante sana Mwandishi pole na wewe kwa majukumu ya kutuhabarisha.

 

Mwandishi. Asante sasa bosi sasa Mwaka umekwisha ule mpango wetu wa Manispaa ya Morogoro kuwa Jiji umefikia eneo gain?

 

Mkurugenzi. Unaelekea Vizuri na kwa sasa kama ulivyoona tumebandika Vipepelushi vya kuhamasisha ushaji ili Mji wetu uwe safi.

Mwandishi. Unahakika kazi hiyo ya usafi inafanyika vizuri?.

 

Mkurugenzi.lnafanyika vizuri.

 

Mwandishi. Sio kweli Mkuu haifanyiki vizuri ni kweli vijana wako wako kazini kufanya usafi ikiwemo kusafisha mitaro ya barabarani kazi hiyo haifanywi vizuri naweza kusema ndio kwanza hali hiyo inachafua Mji.

 

Mkurugenzi. Kwa nini unasema hivyo.

 

Mwandishi. Nasema hivyo kwa sababu Vijana wako wanatoa tope zito kwenye mifereji hiyo na kulitupia katikati ya barabara tena eneo la maduka ya watu wakiwemo kina Mama Ntilie jambo ambalo ni hatari kwa afya za wateja wao.

 

Mkurugenzi. Eneo lile la barabara za Nane Nane na Kola ziko chini ya wenzetu wa TARURA na Picha zile niliziona tumewasiliana na wenzetu wa TARURA nadhani siku mbili hizi watakwenda kuzoa tope lile pale barabarani. 

 

Mwandishi. Sasa kama hali ndio hii nyinyi wahusika mnatoa tope kwenye mifereji na kulitelekea barabarani ndoto zetu za Manispaa wetu kuwa jiji zitatimia kwa uzoaji taka huu wa kizamani?. Mkurugenzi. Nimekwambia eneo lile ni la TARURA. Mwandishi. Any way tutoke huko je kuelekea Manispaa kuwa Jiji inapaswa wafanyabiashara ndogo ndogo’Machinga’ watengewe maeneo maalum wasizagae hovyo Mjini.

 

Nyakati za  Jioni wamachinga wengi wanapanga bidhaa  barabarani hasa barabara za  Madaraka eneo la Lunna na ile ya Boma jirani na Msikiti Mkuu.

 

 Mkurugenzi. Ni kweli inashangaza asilimia 75 ya hao wamachinga tumewapa Vibanda soko Kuu la Kingalu na Soko la Faya lakini wametoka kule na kurejea barabarani kwa sababu ni wananchi wetu tunaendelea kuwapa elimu ili waondoke kiastaarabu.

 

 Wewe Mwandishi unakumbuka ile barabara ya Boma pale jirani na Msikiti ilitokea ajari gari imeacha njia imewavamia kina mama waliokuwa wakiuza bidhaa zao barabarani tulitumia Mgambo kuwaondoa baada ya wiki wamerejea tena.

 

 Mwandishi. Swala la kupanga biashara barabarani ni kosa kisheria sasa tukienda kwa mfumo huyo kuwabembeleza wamachinga kutoka barabarani Manispaa yetu itachelewa sana kuwa Jiji. Mimi kama Mwandishi naona kama kweli tunadhamira ya dhati Manispaa yetu kuwa Jiji tuache Siasa tusimamie sheria Mtu katupa takataka faini elfu 50. Mmachinga katoka kwenye eneo alilopangia kaja barabara anakamatwa faini elfu 50 ndio Majiji ya wenzetu wanavyofanya.

 

Mkurugenzi. Sawa. Mwandishi. Asante kwa ushirikiano wako.

 

Makalla yetu ya Kuelekea Manispaa ya Morogoro kuwa jiji inaishia hapa. Shekidele hana hatia ametimiza Majukumu yake Kama Mwana Morogoro na Mwandishi wa habari kuwakumbusha Viongozi na wananchi wenzake.

                             

Thursday, December 29, 2022

SEHEMU YA TATU MAKALA YA MWELEKEO WA MANISPAA YA MORO KUWA JIJI CHEKI PICHA ZA VULUGU BARABANI.

                                       Kibao cha zuio






Vulugu tupu licha ya soko kuu la Manispaa Maarufu soko la Kingalu kuwa jirani na eneo hili kama umba wa nusu ya kiwanja cha Mpira wafanya biashra hawa wa bidhaa za sokoni wakifanya biashara eneo hili la barabara mbele ya madua ya watu. wenye magari licha ya kibao cha kuwazuiA Kuegesha magari wameegesha na kununu bidhaa eneo hili kama Jamaa akuludi na fenesi lake baada ya kushindwana bei na mmoja wawateja aliyeegesga gari eneo hili

Hatari sana jamaa akichoma mahindi katikati ya barabara ya Makongoro makutano la barabara 4 zenye mzongamano mkubwa wa magari. kufuatia hali hiyo baadhi ya wananchi waliomba eneo hilo kufungwa taa za kuongozea magari licha ya hari hiyo wafanyabiasha hawa wameketi kabisa kwenye kona

 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Takribani siku tatu mfurulizo Mwandishi wa Mtandao huu amejikita kwenye habari ya uchunguzi wa Manispaa ya Morogoro kuwa jiji.

 

Jana Mwandishi huyo aliahadi kutupia picha za wafanyabiashara ndogo ndongo’Wamachinga’ wakiwemo kina mama wauza mboga mboga pamoja na madereva wa Bajaj kwa pamoja wakijazana katikati ya Mji wakivunja  sheria na kuufanya mji huo  kukosa mpangilio hivyo kupoteza baadhi ya Vigezo vya kuwa jiji.

 

Wafanyabiashara hao walipanga biashara zao barabani hali iliyopelekea usumbufu kwa vyombo vya Moto na watu wanaotembea kwa miguu wakiwemo Walemavu,kwa upande wa madereva wa Bajaji nao wanavunja sheria kwa kushusha na kupakia abiria ndani ya kituo cha Mafuta, kama hiyo haitoshi Bajaj hizo pia hushusha na kupakia abiria ndani ya kivuko cha watembea kwa Miguu’Bums ya stend ya zamani ya Daladala.

 

 Vile vile baadhi ya Bajaj hizo hushusha na kupakia abiri ndani ya Mzunguko wa barabara za Madaraka inayoelekea SUA. Barabara ya Boma, inayoelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, barabara ya Korogwe inayoelekea Msamvu na barabara ya zamani ya Dar es salaam inayoelekea Bigwa.

 

Cha kushangaza licha ya Mamlaka husika kuweka kibao cha zuio la Bajaj kupitia eneo hilo kuwepo kwenye  mzunguko huo wa barabara bado madereva hao wa Bajaj wameonegaka kukaidi  amari hiyo.

 

 Leo jioni  Mwandishi huyo wa habari za kichunguzi aliwanasa madereva hao wakishuka kwenye Bajaj zao na kugombea abiria ndani ya Mzunguko huo wa barabara jirani  kabisa  na kibao hicho cha zuio  bila wasiwasi wowote.

 

 Bajaj nyingine zikionekana zikishusha na kupakia abiria ndani ya kituo cha Mafuta jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiri na vyombo vyao.

 

 Sheria za usafirishaji zinazuia Vyombo vya Moto kuingia kituo cha mafuta kujaza mafuta huku kikiwa na abiri.

 

Masikini ya Mungu wakati Shushu huyo wa habari  za kichunguzi anayetumia kamera za kisasa zenye uwezo wa kupiga Picha usambali Mrefu ambazo pia hazito Mwanga alimshuhudia Mlinzi wa Kituo hicho cha Mafuta akipuuzwa na madereva hao wa Bajaj.

 

 

Shushu huyo akiwa umbali wa zaidi ya Mita 200 akipiga Picha Bajaj hizo zikiwa ndani ya kituo hicho cha Mafuta alimshuhudia Mlinzi huyo akihangaika kuzifukuza Bajaj hizo bila Mafanikio.

 

 Licha ya Mlinzi huyo kuwafukuza Madera hao walimpuuza na kuendelea kushusha na kubakia abiri kama Picha zinavyoonyesha Mlinzi huyo akiwafukuza bila mafanikio.

 

Baada ya kupiga Picha hizo za kishushu akiwa umbari mrefu,Mwandishi huyo aliludisha Kamera kwenye begi na kutinga kwenye kituo hicho cha Mafuta na kuzungumza na Mlinzi huyo ambapo alipotakiwa kueleza hali hiyo alisema.

” Bora Mwandishi wa habari nisaidie hawa madereva wa Bajaj wanataka kunifukuzisha kazi bosi wa Kituo hiki kapiga marufuku Bajaj kushusha na kupakia abiria ndani ya kituo chake akitupa agizo sisi walinzi  kuhakikisha Bajaj hazifanya hivyo”alisema Mlinzi huyo na kuongeza kudadavua.

 

Kama unavyoona wanafukuza hawasikii wanaendelea kushusha na kupakia abiria eneo hili”alisema Mlinzi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa sababu yeye  si msemaji wa kituo hicho.

 

Mwandishi huyo alipotaka kuzungumza na bosi wa kituo hicho Mlinzi huyo alidai kwa muda huo wa saa 12 jioni ameshatoka ofisini hivyo.juhudi hizo za kumtafuta zinaendelea.

 

Mara baada ya kuzungumza na bosi huyo Mwanahabari huyo  pia atatinga Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro’RPC’kuzungumza naye kuhusiana na vulugu hizo za Bajaj  ambazo nyingi hazina namba ya Usajiri nyuma kama zinavyonekana Pichani.

 

Mwandishu huyo pia atatinga ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa kwa lengo la kupata maelezo ya Wamachinga hao kuzagaa barabarani huku baadhi wakiwasha Moto na kuchoma mahindi katikati ya barabara.

Tuesday, December 27, 2022

SEHEMU YA PILI ISHU YA MORO KUWA JIJI.

Mwananchi akitembea katikati ya barabara baada ya eneo lao la watembea kwa miguu kuzibwa na Vifusi vya tope
...Baadhi ya wafanyabishara nao waliemau kujaza takatata kwenye Viroba na kuzitupa barabarani wakifuata nyazo zilizofanywa na wafanyakazi wa Manispaa

 Lundo la tope likitelekezwa barabara ya Nane nane kuelekea Makaburi ya Kolla


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kuelekea Manispaa ya Morogoro kuwa jiji Maoni ya Mwandishi  wa Mtandao huu aliyoanza kuyatoa jana yanaendelea tena leo.

 

 Baada ya kutoa Maoni hayo kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inavyoelekeza kwamba kila Mtanzania anahaki ya kutoa Maoni  yake kwenye jambo lolote Pasina kuvunja sheria za nchi hivyo Mwandishi huyo anaishi kwenye kifungu hicho.

 

 Kama hiyo haitoa Mwandishi huyo anakofia ya Pili ya kufanya hivyo ambapo kazi ya Mwandishi wa habari ni Kuelemisha, Kuburudisha, Kuhabarisha na kukosoa. Sasa hapa anapembea na  kipengele cha kukosoa

 

Kwenye maoni hayo aliyoyatoa alidadavua mengi huku akiahidi kukatiza kwenye barabara Mpya za kiwango cha Lami zilizopo eneo la Nane nane Area Five  Kata ya Kichangani zilizojazwa uchafu wa vifusi vya tope na watumishi wa Manispaa.

 

Jana majira ya asubuhi Mwandishi huyo alikatiza kwenye barabara hizo mbili ile inayotoka Nane nane kuelekea Makaburi ya Kola na ile inayotoka Nane nane eneo la maegesho ya Malori kuelekea Kichangani na kushuhudia uchafu huo.

 Baada ya kufika kwenye barabara hizo zilizojengwa miaka 2 iliyopita Mwanahabari huyo alishuhudia lundo la tope zilizotolewa kwenye mifereje na kutelekezwa kwenye barabara hizo eneo la watembea kwa Miguu hali iliyopelekea wananchi kupita katikati ya barabara jambo ambalo ni hatari kiusalama.

 

Kama hiyo haitoshi baadhi ya wafanyabiashara wanao fanyabiashara kando kando ya barabara hizo eneo la Maegesho ya Malori  hasa kina Mama Ntili baada ya kuona watumishi hao wa manispaa wametelekeza uchafuo huo kwenye maeneo yao nao wameamua kutupa viroba vya takatika kwenye eneo hilo hilo kama inavyoonekana Pichani.

 

Wakizungumza na Mtandao huu baadhi ya wafanyabiashara hao wamewatupia lawama wafanyakazi hao wa Manispaa kwa kujaza tope kwenye biashara zao” Angefanya hivi mwananchi wa kawaida Maafisa Afya wa Manispaa wangempifa faini sasa wao wametoa tope zito kwenye mitalo zaidi ya wiki bila kuzoa kama hawana gari la kubeba uchafuo huo kwa nini wameutoa kwenye mifereji?,alisema Mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Tunaelewa kuelekea Msimu huu wa Mvua Wafanyakazi wa Manispaa wanafanya kazi ya kuzibua Mifereji ili maji yapite bila kuzalisha mafuriko, lakini pia sio busara kutoa tope hilo chafu na kulitelekeza kwenye barabara mpya mbaya zaidi kwenye makazi ya wananchi wanaofanya biashara za vyakula.

 

  Japo sijasoma vizuri Mwongozo wa Taifa wa Vigezo kupandisha hadhi Maeneo waishio watu,lakini Mwandishi anaamini moja ya Vigezo hivyo ni mpangilio mzuri wa Mji sambamba na usafi wa Mji husika.

 

Tujiulize Maswali Mepesi tu Je kwa hali hii ya Muonekano wa Picha hizi za uchafu juhuzi zetu la kuifanya Manispaa yetu ya Morogoro kuwa jiji zitaza matunda?

 

 Panapo majaliwa ya mwenyezi Mungu kesho stori hii itaendelea kwa kurusha hewani picha za wafanyabiashara ndogo ndogo’Wamachinga’ wakizagaa hovyo katikati ya Mji huo huku baadhi yao wakipanga bidhaa zao barabarani ikiwa ni kinye cha sheria.

Monday, December 26, 2022

HAPA SIO ULAYA NI MJI KASORO BAHARI.



 


 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu ni kweli Mijengo hiyo haiko Ulaya bali iko Maeneo la Msamvu Mkoani Morogoro.

 

 Maghorofa hayo ni hotel za kisasa ambapo Mwandishi wa Mtandao huu si kama anatoka kula bata kwenye hotel hizo hapana  anatoka  kufanya kazi yake ya Uandishia wa habari.

 

Kwa sasa Mji wa Morogoro unazidi kukua kwa kwa kasi ambapo aliyekuwa rais wa awamu ya 5 hayati John Pombe Magufuli’JPM’ wakati akizindua Soko kuu la Kisasa la Morogoro Maarufu Soko la Chief Kingalu.

 

Alishangazwa Manispaa ya Morogoro mpaka sasa kutokizi Vigezo vya kupewa hadhi ya Jiji ili hali mikoa inayolingana na Manispaa hiyo kama Mkoa wa Tanga na Dodoma kukidhi Vigezo vya Jiji huku Morogoro ikishindwa kufanya hivyo.  Kwa Miaka Mingi kufuatia ukubwa wa Mji wao wenyeji wa Mkoa wa Morogoro’Waluguru’wanakausemi kao kanakosema ”Mweee Morogoro Mji Kasoro Bahati Tu” Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi umebaini baadhi ya vigezo vinavyopelekea Mji huo kukosa Vigezo vya Manispaa ni Pamoja na Chafu wa Mji  wamachinga kuzagaa hovyo katikati ya Mji.

 

 Kuhusu Uchafu Mfano Juzi  Mwandishi wa Mtandao huu alikatiza  barabara mpya za kisasa za Viwango vya lami chaajabu baadhi ya wafanyakazi wa Manispaa kwa sasa wanaendelea kutoa tope zito kwenye mifereji na kutupa katikati ya barabara ya lami.

 

 Tope hilo lipo zaidi ya siku 4  bila kuzolewa na hivyo barabara hio 2 ile inayotoka Nane nane kuelekea Makaburi ya Kolla na ile inayotoka Nane nane eneo la Maegesho la Malori inayoelekea Kichangani kugeuka kuwa ya vumbi ili hali chini kuna lami.

 

 Muda huu napita tena kwenye eneo hilo kama nikikuta tope hilo bado halijazolewa nitapiga Picha na kurusha hewani kwa lengo la kuwakumbusha Vigogo wa Manispaa.

Saturday, December 24, 2022

KUMBUKIZI YA KUZALIWA,MWANDISHI AOMBA RADHI.

Mesia Yesu Kristo akizaliwa katika Zizi la Ng'ombe Desemba 25
Dunstan Peter Shekidele alizaliwa hospital ya  ya Rufaa ya Bombo Jijini Tanga Desemba 25

 


                 Na Mwana Birthday Dunstan Shekidele.

Leo Desemba 25 Wakristo duniani kote wanasheherekea siku kuu ya kuzaliwa Mesiha Yesu Kristo ambaye Mungu alimtoa kama sadaka kwa wanadamu, aliluhusu Mtume huyo aliyekuja kuukomboa Ulimwengu azaliwe katika zizi la kufungia Ng’ombe kama picha ya mfano inavyoonyesha Mtoto Yesu akizaliwa katika Zizi hilo la Ng’ombe.

Leo Pia Decemba 25 ni kukumbizi ya Kuzaliwa kwa Mwandishi wa Mtandao huu ambaye yeye hakuzaliwa Katika Zizi la Ng’ombe bali amezaliwa katika Hospital ya Rufaa ya Bombo iliyopo kando kando ya Bahati  Jijini Tanga.

 

              SHUKRAN.

Kipekee na Msukulu Mungu kwa kuendelea kunipa zawadi ya Uhai na leo hii kwa Neema zake ameniongezea Mwaka Mwingine.

Pili nawashukuru wazazi wangu Marehemu Baba yangu Mzee Peter Zakari Shekidele Mungu amepe punziko   la Aman.

Tatu. Mama yangu Kipenzi Tumaini Samwel Juma ‘Mrs Shekidele’ anayeendelea na Matibabu jijini Dar es salaam na Muombea kwa Mungu amponye upesi.

Nne nawashukuru Viongozi wote wa dini zote kwa kuendelea kutupa mahubiri na Mawaidha yenye lengo la kutuweka karibu na Mwenyezi Mungu.

 

 Tano. Nawashukuru Viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kuenzi na kudumia Amani inayopelekea mimi na wananchi wengine kuishi kwa amani.  

Sita. Nawashukuru ndugu zangu Marafiki zangu na wadau wote wa Mitandao yangu ya Kijamii hasa Facebook.                        MSAMAHA.

Kupitia siku yangu hii ya kuzaliwa naomba Msahama wa dhati toka ndani ya sakafu ya Moyo wangu kwa mtu yoyote niliyemkosea kwa kujua ama kwa kutoa kujua naomba anisamehe kwani mimi ni kiumbe dhaifu si Mkamilifu.  

 

Pia kupita siku hii nimewasamehe kwa dhati  wote walionikosema kwa namna yoyote ile.

Happy Birthday Yesu Kristo, Happy Birthday Dunstan Shekidele, Happy Birthday watu wote waliozaliwa siku  ya leo Desemba 25.

               UJUMBE KWA WOTE.

Kumcha  Bwana’Mola’ ndio chanzo cha Maarifa. Hapa duniani tunapitia kuna maisha mengine tena mazuri zaidi ya maisha haya ya duniani yaliyojaa damu na shida nyingi.

 

UDAKUZ SPESHO. DUME LA NYAKUA PESA ZA MCHEZO NA KWENDA KUFUNGA NDAO MWACHIA MSALE KIONGOZI WAKE.


 

 

Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro.

 Udakuzi huu ni wakufunga Mwaka 2022 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2023.ambapo Kijana mmoja ‘Jina Kapuni’ anadaiwa kuchukua pesa za Mchezo na kwenda kijijini kwao kuoa.

 

Kama kawaida kila Jumamosi Mtandao Pendwa wa Shekidele hurusha habari ya kidakuzi, Kwa Jumamosi iliyopita hilo halikufanyika  kufuatia Udakuzi huu kutokamilika kwa baadhi ya wahusika kutopatikana.

 

 Hata hivyo wahusika hao walipotakika walikwepa kutoa ushirikiano.

 

 Licha ya wahusika kukwepa kutoa ushirikiano hawazuia udakuzi huo kwenda hewani, Mwandishi wa habari ni kama hakimu  hutoa nafasi kwa mshitakiwa kujitetea Mbele ya Mahakama hivyo  Mshitakiwa akigoma kutoa  utetezi  haimzui hakimu kufanya kazi yake ya kutoa hukumu.

 

Hali kazarika  Kanuni za Uandishi wa habari zinaelekeza kabla ya kurusha habari lazima ubalance Story pande zote mbili kwa Maana ya Upande wa Mlalamikaji na ule wa Mlalamikiwa.

 

Hivyo Mlalamikiwa akikwepa kukupa maelezo  haizui habari hiyo kuruka hewani,Mwandishi atakapoandika habari hiyo ataueleza uma kwamba  Mlalamikiwa alipofuatwa ili azungumzie tuhuma hizo zinazomkabiri aligoma kuzungumza.

 

Nimelazimika kutoa ufafanuzi huo wa kisheria na kikanuni kufuatia wahusika  kugoma kutoa ushirikiano kwa Mdakuzi, Jumamosi iliyopita udakuzi huu ulishindwa kwenda hewani baada ya wahusika kutopatikana.

 

Wiki hii Mdakuzi  alifanya jitihada za dhati na kufanikiwa kuwapata wahusika lakini  waliposomewa tuhuma zao waligoma kutoa maelezo.

 

Hivyo Udakuzi huo unakwenda hewani Live bila chenga baada ya kutimiza kanuni za Uandishi wa habari ingawa  sitotaja majina yao hewani.

         UDAKUZ WENYEWE SASA.

Mdakuzi alipokea taarifa sahihi kutoka kwa Mwananchi mmoja akidai kwamba siku za nyuma alicheza mchezo ule wa kimtaa wa kupeana Pesa kwa maana kiongozi anakusanya pesa kila siku za watu zaidi ya 50 kwa kiwango wanachokubaliana mfano kila siku lazima kila mtu awasilishe shiringi elfu 5.

 

Na kwamba baada ya pesa hizo  kukusanywa kiongozi wa mchezo huo humkabidhi mtu mwenye jina la kwanza  hali hiyo inaendelea mpaka majina yote 50 zitakapofika tamati.

 

 Mbaya zaidi michezo hiyo ya kimtaa inakwenda kwa kuaminiana  hakuna kigezo cha mtu kuweka  dhamana yoyote  ikitokea imelaza siku moja siku ya pili unatakiwa  ku Double Pesa ya jana na leo

 

Siku za hivi karibuni uliibuka mzozo mkubwa eneo la Lunna kunawafanyabiasha 50 walianzisha mchezo huo wa kila siku elfu 5 ambapo kila siku mtu alitoka na laki mbili na nusu.

 

  mmoja wawashiriki kaingia majina 3 kwa maana kila siku alihitajika kukabidhi elfu 15 Kijana huyo kawasilisha ombi la majina yake hayo 3 yawe ya kwanza kakubaliwa hivyo ndani ya siku 3 za kwanza kakabidhiwa laki saba na nusu.

 

Kijana huyo baada ya kukusanya Pesa hiyo ndefu kwa sisi walala hoi katinga kijijini kwao kuoa mtoto mkali  katkisa kijijini  kwa kufunga mziki mnene wa Mtaani Maarufu Kigodoro’kama tunavyojua kwa maisha ya kijijini ukiwa na Milioni unafunga ndoa ya kifahari.

 

 Mdakuzi krambishwa Ubuyu kwamba Kijana huyo alikuwa n hakiba yake ya laki 3 hivyo alivyokabidhi laki saba na nusu  mzigo umesoma Milioni na ushee.

 

Kesho yake kareja Mjini na Mwali wake wakaanza maisha ya ndoa ya kila siku kuacha ushuru wa meza, huku akitakiwa  kulipa kila siku elfu 15 kwa siku 47 mfurulizo.

 

huku kodi ya nyumba inamhitaji jamaa majukumu yamempalia maisha  ya awari ya kisela  chai buku kwa mama Ntilie mchaka chakula  Buku na jioni tena cha buku yamebadilika  kwa mkewe hamna hamna kila siku lazima ache elfu 8 pesa ya matumizi.

 

kwenye mchezo kila siku elfu 15 jamaa kajikongoja hivyo kwa wiki 2 wiki ya tatu kaferi kupeleka pesa ya mchezo biashara yake mtaji umekata kamua kuwakimbia wenzake wa mchezo.

 

 Kiongozi wa mchezo  baada ya kufanya uchunguzi kabaini kwamba mwenzao alichukua pesa hizo na kwenda kufunga ndoa wakaamua kwenda kwenye biashara yake hawakumkuta wakapewa maelezo kwamba baada ya kuoa amefunga biashara.

 

Wametinga nyumbani  wakaelezwa na mwenye nyumba kwamba baada ya kuoa hakukaa sana amehama na alipohamia hapajulikani.

 

Mdakuzi baada ya kurambishwa ubuyu huo katinga kwa kiongozi huyo wa mchezo alipotakiwa kuelezea tukio hilo Msimamizi huyo wa mchezo aligoma kutoa ushirikiano.

 

Kwa vile  amegoma  Mwandishi wa habari hizi  analazimika kutoa taarifa zilizopatikana eneo la tukio ambazo zinadai kwamba kiongozi huyo amelazimika kuuza vitu vyake kulipa deni hilo.

 

Pia taarifa nyingine zilizopatikana eneo hilo la tukio zinadai kwamba kiongozi huyo hakuuza vitu vyake bali analipa deni hilo kwa kukatwa posho yake.

 

kwamba kwenye mchezo huo walijiwekea kanuni  kila siku mtu anapokabidhiwa Pesa ni lazima ampe posho ya elfu 10 msimamizi wa mchezo huo.  

Kweli ndani ya ndoa kuna siri kubwa mpaka leo bibi harusi huyo yuko ndani akikarangiza hajui maswahiba yanayompaka mumeweke ambaye ili asionekena mnyonge hakumshirikisha mkewe kwenye jambo hilo.

 

 

 

 

 

 

Friday, December 23, 2022

KUMBUKIZI YA KIFO CHA BIBI WA MIAKA 103

Picha no 2 Mwinjilisti wa kanisani la KKKT Usharika wa Kitunda Dar akiongoza lbada fupi ya kumuombea Marehemu ndani ya Hospital ya Amana kabla Mwili wa Mpendwa wetu kusafirishwa kuelekea Lushoto kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele.


Jeneza lililo beba mwili wa bibi Kete likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea kijijini kwake  Tarafa ya Mlalo  Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga. Picha juu ni baadhi ya familia ya bibi Keke inayosihi jijini Dar es salaam wakishiriki lbada fupi iliyofanyika hospitalini hapo
Msafara huo ukikatiza maeneo mbali mbali ya jiji la Dar ukielekea Lushoto ukipitia njia ya Bagamoyo Road ambapo Mpiga Picha wa Mtandao huu aliyeketi siti ya mbele ya moja ya Coaster alifanya kazi ya kupiga Picha matukio yote ya njiani
....Msafara huo ukiwasili daraja la Wami barabara kuu ya Calinze Segera


Msafara huo ukiwasili Stend ya Mkongoloni Jimbo la Mlalo Lushoro
William Peter Shekidele ambaye ni Mjukuu wa kwanza wa bibi kete akizungumza na anko wake David Juma kulia ni Dkt lkunda Riwa kitukuu cha marehemu ambaye pia ni mtoto wa kwanza wa Elice Peter Shekidele

Changamoto mwenzi huo wa Desemba ni mwezi wa msimu wa Mvua ambapo basi lililobeba mwili wa marehemu lilikwama kwenye moja ya barabara za kijijini hapo na kurazimika waombolezaji kutoa msaada wa kulisukuma na kufanikiwa kuvusha eneo hilo korofi
Msafara huo ukiwasilia nyumbani kwa mume wa marehemu Mzee Samwel Juma ambaye pia alitangulia mbele za haki

Kutoka Kulia Dustan Peter Shekidele, Elisante Peter Shekidele Wiliam Peter Shekidele wakiwa na Anko wao David Juma mwenye kofiakati] wa mwisho kushoto ni Mpiga kinanda maarufu wa kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo ambaye pia anaudugu na familia hiyo ya Marehemu.
                     Kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo
David Juma ambaye ni Mtoto pekee wa kiume wa Marehemu akimlilia Mama yake hulia anayembendeleza ni Mke wa David Juma
Mwili wa bibi Kete ukitolewa kanisani baada ya kumilika kwa lbada


Msafara ukitoka kanisani ukielekea nyumbani kwake msafara huo ukiongozwa na matarumbeta ya kanisa la KKKT Usharika wa Mlala ambapo enzi za Uhai wake bibi Kete Abdallah alikuwa Mwana kwaya ya kwaya Kuu ya Usharika huo
;;;Mwili ukiwasi kwenye nyumba yake ya Milele

Anko David Juma akiwa kwenye kaburi la Mpendwa mama yake mara baada ya kumzika kwenye shamba lake Mlalo Lushoto Picha zote na Dunstan Shekidele aliyekuwa Lushoto

...Msafara huo Ukiwa Lushoto Mjini ukirejea Dar es salaam baada ya mazishi
Kutoka Kushoto Dustan Peter Shekidele, William Peter Shekidele na Elisante Peter Shekidele Kwa pamoja wakiwa kwenye kaburi la Mpendwa baba yao hayati Peter Zakaria Shekidele, kaburo hilo liko nje ya kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo Lushoto.
...Hayati Bibi Kete Abdallah103' enzi za uhai wake lfahamike licha ya kuw ana umri huo Mkubwa bibi Kete alikuw aakisumbuliwa na Miguu tu lakini hajawahi kusumbuliw ana ugonjwa wa Pesha kisukari wala ugonjwa wowote na hadi anafariki alikuw aakisoma biblia ba sms kwenye simu bila kutumia miwani
Bibi kete akimpa wosia Mjukuu wake ambaye ni Mwandishi wa Mtandao huu kwa Lugha ya Kisambaa
Vicky David Juma Mjukuu akimsaidia bibi yake kukata keki kwenye moja ya Birthday zake.

KUMBUKIZI.

Leo Desemba 22 Mpendwa wangu. Mke wangu, Kipenzi cha Moyo wangu, barafu wa Moyo wangu, My Number One, Mshauri wangu, Msili wangu.

 

Kette Abdallah umeniacha mpweke baada ya kutwaliwa na Bwana ukiwa usingizini nyumbani kwako Gongolamboto,Mombasa, Mtaa wa Moshi Baa jijini Dar es salaam.

 

Marehemu Kete ambaye ni bibi yangu aliyenizalia Mama yangu Mzazi alifariki dunia Desemba 22 2019 akiwa na umri wa Miaka 103.

Marehemu ameacha watoto watatu Tumaini Samwel Juma, ‘Mrs Shekidele’, David Samwel Juma na Neema Samwel Juma’Mrs Mulokozi’ Wajukuu, Vitukuu na Vilembwe zaidi ya 100.

 

Pichani Bibi Kette akinipa wosia kwa Lugha ya Kisambaa kwenye moja ya sherehe zake za kuzaliwa’Happy Birthday iliyofanyika nyumbani kwake Moshi Baa.

 

Leo Desemba 22 2022 ametimiza miaka 3 toka alivyofariki dunia na kuzikwa kijijini kwake Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Desemba 26.

 

Watu wengi walihoji sababu za kuchelewa kuzikwa na Mpendwa wetu, nami na wajibu kwamba sababu ya msingi ya kuchelewa kumzika Mpendwa wetu ni kwa sababu ya kumsubiri mwanae pekee wa kiume David Juma anayeishi Marekani.

 

Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe.

 

Umetangulia bibi yangu tutaonana baadae.

  

 

 
 

Tuesday, December 20, 2022

TANZIA KIFO CHA BI AGNES CHA LIZA WENGI

Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa akuzunguka kwenye vitengo vyote kwenye msiba huo pichani akitinga makaburini kukagua zoezi la uchimbaji kaburi sambamba na kuwapelekea maji ya kunywa wachimbaji hao kama inayovyoonekana kwenye Pikipiki ya kazi ya ya Mwandishi huyo 'Ez Come Ez Go'




       Wajukuu wa marehemu wakimuaga bibi yao

Elizabeth ambaye ni mtoto wa mwisho wa marehemu akimuaga kwa kilio Mpendwa mama yake,

Elisante Peter Shekidele aliyefunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kuja kumzika Mama yake Mdogo akisoma wasifu wa Marehemu

 

Mzee Togolai Shekidele akiweka udongo kwenye kaburi

Mgane wa Marehemu Mzee Togolai Shekidele akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mpendwa mke wake

Elizabeth na Mumewe wakiweka shada la Mau kwenye kaburi la Mpendwa mama yao

Gasper ambaye ni mmoja wawatoto wa kiume akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mpendwa Mama yake

lnauma sana Mmoja wa wajukuu wa marehemu akiweka shada la mau kwenye kaburi la mpendwa bibi yake
 

TANZIA.

KWA takribani siku 3 Mtandao Pendwa wa Shekidele haukuposti habari yoyoye.

 

Hali hiyo imetokana na Mwandishi wa Mtandao huo kufiwa na Mama yake Mdogo Marehemu Agnes Togolai Shekidele aliyefariki dunia Desemba 16 hospital ya Mkoa wa Morogoro alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu’Presh’na kuzikwa Desemba 18 katika makaburi ya Kolla Manispaa ya Morogoro.

 

Mwandishi wa Mtandao huu ambaye Marehemu Agnes ni Mke wa baba yake Mdogo Mzee Togolai Zakaria Shekidele anayezaliwa tumbo moja na baba Mzazi wa Mwandishi huyo Hayati Peter Zakaria Shekidele ndiye aliyekuwa msimamizi Mkuu wa Msiba huo uliokuwa nyumbani kwa Marehemu Mtaa wa Mji Mwema Kata ya Tungi nyuma ya shule ya Sekodani ya Alfa inayomilikiwa na Padri Ricado Maria Maarufu Padri Pekupeku.

 

 Hivyo kutokana na hali hiyo Mwandishi huyo hakufanya kazi yoyote kwa siku zote tatu zaidi ya shughuri hizo za Msiba wa Mpendwa Mama yake mdogo.

 

Tangulia Mpendwa wetu tutaonana baadae. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

 

Katika mziba huo Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Mji Mwema kwenye mahubiri yake aliwashukia watoto wasiowatunza wazazi wao akishauri sheria itungwe kuwadhibiti watoto wanaowatelekeza wazazi wao.

 

kama kawaidi stori hiyo itaruka hewani jumapili kwenye kipindi  cha ujumbe wa neno la Mungu kinacholuka kila siku za jumapili kwenye Mtandao huu hivyo usikose kusoma hahuburi hayo ya kusisimu yaliwagusa waombolezaji wengi wa dini mbali mbali waliofulika kwenye msiba huo.

                        CAPTION.

 Mgane wa Marehemu  Mzee Togolai Shekidele akimuaga kwa uchungu mkubwa Mpendwa Mke wake aliyefunga naye ndoa takribani miaka 50 hadi kifo kilipowatenganisha juzi.

 

Agalia picha zaidi za mziba huo hapo chini au fungua Profaili la Mtandao huu.

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...