Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa akuzunguka kwenye vitengo vyote kwenye msiba huo pichani akitinga makaburini kukagua zoezi la uchimbaji kaburi sambamba na kuwapelekea maji ya kunywa wachimbaji hao kama inayovyoonekana kwenye Pikipiki ya kazi ya ya Mwandishi huyo 'Ez Come Ez Go'
Wajukuu wa marehemu wakimuaga bibi yao
Elizabeth ambaye ni mtoto wa mwisho wa marehemu akimuaga kwa kilio Mpendwa mama yake,
Elisante Peter Shekidele aliyefunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kuja kumzika Mama yake Mdogo akisoma wasifu wa Marehemu
Mzee Togolai Shekidele akiweka udongo kwenye kaburi
Mgane wa Marehemu Mzee Togolai Shekidele akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mpendwa mke wake
Elizabeth na Mumewe wakiweka shada la Mau kwenye kaburi la Mpendwa mama yao
Gasper ambaye ni mmoja wawatoto wa kiume akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mpendwa Mama yake
lnauma sana
Mmoja wa wajukuu wa marehemu akiweka shada la mau kwenye kaburi la mpendwa bibi
yake
TANZIA.
KWA takribani siku 3 Mtandao Pendwa wa Shekidele haukuposti habari yoyoye.
Hali hiyo imetokana na Mwandishi wa Mtandao huo kufiwa na Mama yake Mdogo Marehemu Agnes Togolai Shekidele aliyefariki dunia Desemba 16 hospital ya Mkoa wa Morogoro alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu’Presh’na kuzikwa Desemba 18 katika makaburi ya Kolla Manispaa ya Morogoro.
Mwandishi wa Mtandao huu ambaye Marehemu Agnes ni Mke wa baba yake Mdogo Mzee Togolai Zakaria Shekidele anayezaliwa tumbo moja na baba Mzazi wa Mwandishi huyo Hayati Peter Zakaria Shekidele ndiye aliyekuwa msimamizi Mkuu wa Msiba huo uliokuwa nyumbani kwa Marehemu Mtaa wa Mji Mwema Kata ya Tungi nyuma ya shule ya Sekodani ya Alfa inayomilikiwa na Padri Ricado Maria Maarufu Padri Pekupeku.
Hivyo kutokana na hali hiyo Mwandishi huyo hakufanya kazi yoyote kwa siku zote tatu zaidi ya shughuri hizo za Msiba wa Mpendwa Mama yake mdogo.
Tangulia Mpendwa wetu tutaonana baadae. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Katika mziba huo Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Mji Mwema kwenye mahubiri yake aliwashukia watoto wasiowatunza wazazi wao akishauri sheria itungwe kuwadhibiti watoto wanaowatelekeza wazazi wao.
kama kawaidi stori hiyo itaruka hewani jumapili kwenye kipindi cha ujumbe wa neno la Mungu kinacholuka kila siku za jumapili kwenye Mtandao huu hivyo usikose kusoma hahuburi hayo ya kusisimu yaliwagusa waombolezaji wengi wa dini mbali mbali waliofulika kwenye msiba huo.
CAPTION.
Mgane wa Marehemu Mzee Togolai Shekidele akimuaga kwa uchungu mkubwa Mpendwa Mke wake aliyefunga naye ndoa takribani miaka 50 hadi kifo kilipowatenganisha juzi.
Agalia picha zaidi za mziba huo hapo chini au fungua Profaili la Mtandao huu.
No comments:
Post a Comment