Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, December 24, 2022

UDAKUZ SPESHO. DUME LA NYAKUA PESA ZA MCHEZO NA KWENDA KUFUNGA NDAO MWACHIA MSALE KIONGOZI WAKE.


 

 

Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro.

 Udakuzi huu ni wakufunga Mwaka 2022 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2023.ambapo Kijana mmoja ‘Jina Kapuni’ anadaiwa kuchukua pesa za Mchezo na kwenda kijijini kwao kuoa.

 

Kama kawaida kila Jumamosi Mtandao Pendwa wa Shekidele hurusha habari ya kidakuzi, Kwa Jumamosi iliyopita hilo halikufanyika  kufuatia Udakuzi huu kutokamilika kwa baadhi ya wahusika kutopatikana.

 

 Hata hivyo wahusika hao walipotakika walikwepa kutoa ushirikiano.

 

 Licha ya wahusika kukwepa kutoa ushirikiano hawazuia udakuzi huo kwenda hewani, Mwandishi wa habari ni kama hakimu  hutoa nafasi kwa mshitakiwa kujitetea Mbele ya Mahakama hivyo  Mshitakiwa akigoma kutoa  utetezi  haimzui hakimu kufanya kazi yake ya kutoa hukumu.

 

Hali kazarika  Kanuni za Uandishi wa habari zinaelekeza kabla ya kurusha habari lazima ubalance Story pande zote mbili kwa Maana ya Upande wa Mlalamikaji na ule wa Mlalamikiwa.

 

Hivyo Mlalamikiwa akikwepa kukupa maelezo  haizui habari hiyo kuruka hewani,Mwandishi atakapoandika habari hiyo ataueleza uma kwamba  Mlalamikiwa alipofuatwa ili azungumzie tuhuma hizo zinazomkabiri aligoma kuzungumza.

 

Nimelazimika kutoa ufafanuzi huo wa kisheria na kikanuni kufuatia wahusika  kugoma kutoa ushirikiano kwa Mdakuzi, Jumamosi iliyopita udakuzi huu ulishindwa kwenda hewani baada ya wahusika kutopatikana.

 

Wiki hii Mdakuzi  alifanya jitihada za dhati na kufanikiwa kuwapata wahusika lakini  waliposomewa tuhuma zao waligoma kutoa maelezo.

 

Hivyo Udakuzi huo unakwenda hewani Live bila chenga baada ya kutimiza kanuni za Uandishi wa habari ingawa  sitotaja majina yao hewani.

         UDAKUZ WENYEWE SASA.

Mdakuzi alipokea taarifa sahihi kutoka kwa Mwananchi mmoja akidai kwamba siku za nyuma alicheza mchezo ule wa kimtaa wa kupeana Pesa kwa maana kiongozi anakusanya pesa kila siku za watu zaidi ya 50 kwa kiwango wanachokubaliana mfano kila siku lazima kila mtu awasilishe shiringi elfu 5.

 

Na kwamba baada ya pesa hizo  kukusanywa kiongozi wa mchezo huo humkabidhi mtu mwenye jina la kwanza  hali hiyo inaendelea mpaka majina yote 50 zitakapofika tamati.

 

 Mbaya zaidi michezo hiyo ya kimtaa inakwenda kwa kuaminiana  hakuna kigezo cha mtu kuweka  dhamana yoyote  ikitokea imelaza siku moja siku ya pili unatakiwa  ku Double Pesa ya jana na leo

 

Siku za hivi karibuni uliibuka mzozo mkubwa eneo la Lunna kunawafanyabiasha 50 walianzisha mchezo huo wa kila siku elfu 5 ambapo kila siku mtu alitoka na laki mbili na nusu.

 

  mmoja wawashiriki kaingia majina 3 kwa maana kila siku alihitajika kukabidhi elfu 15 Kijana huyo kawasilisha ombi la majina yake hayo 3 yawe ya kwanza kakubaliwa hivyo ndani ya siku 3 za kwanza kakabidhiwa laki saba na nusu.

 

Kijana huyo baada ya kukusanya Pesa hiyo ndefu kwa sisi walala hoi katinga kijijini kwao kuoa mtoto mkali  katkisa kijijini  kwa kufunga mziki mnene wa Mtaani Maarufu Kigodoro’kama tunavyojua kwa maisha ya kijijini ukiwa na Milioni unafunga ndoa ya kifahari.

 

 Mdakuzi krambishwa Ubuyu kwamba Kijana huyo alikuwa n hakiba yake ya laki 3 hivyo alivyokabidhi laki saba na nusu  mzigo umesoma Milioni na ushee.

 

Kesho yake kareja Mjini na Mwali wake wakaanza maisha ya ndoa ya kila siku kuacha ushuru wa meza, huku akitakiwa  kulipa kila siku elfu 15 kwa siku 47 mfurulizo.

 

huku kodi ya nyumba inamhitaji jamaa majukumu yamempalia maisha  ya awari ya kisela  chai buku kwa mama Ntilie mchaka chakula  Buku na jioni tena cha buku yamebadilika  kwa mkewe hamna hamna kila siku lazima ache elfu 8 pesa ya matumizi.

 

kwenye mchezo kila siku elfu 15 jamaa kajikongoja hivyo kwa wiki 2 wiki ya tatu kaferi kupeleka pesa ya mchezo biashara yake mtaji umekata kamua kuwakimbia wenzake wa mchezo.

 

 Kiongozi wa mchezo  baada ya kufanya uchunguzi kabaini kwamba mwenzao alichukua pesa hizo na kwenda kufunga ndoa wakaamua kwenda kwenye biashara yake hawakumkuta wakapewa maelezo kwamba baada ya kuoa amefunga biashara.

 

Wametinga nyumbani  wakaelezwa na mwenye nyumba kwamba baada ya kuoa hakukaa sana amehama na alipohamia hapajulikani.

 

Mdakuzi baada ya kurambishwa ubuyu huo katinga kwa kiongozi huyo wa mchezo alipotakiwa kuelezea tukio hilo Msimamizi huyo wa mchezo aligoma kutoa ushirikiano.

 

Kwa vile  amegoma  Mwandishi wa habari hizi  analazimika kutoa taarifa zilizopatikana eneo la tukio ambazo zinadai kwamba kiongozi huyo amelazimika kuuza vitu vyake kulipa deni hilo.

 

Pia taarifa nyingine zilizopatikana eneo hilo la tukio zinadai kwamba kiongozi huyo hakuuza vitu vyake bali analipa deni hilo kwa kukatwa posho yake.

 

kwamba kwenye mchezo huo walijiwekea kanuni  kila siku mtu anapokabidhiwa Pesa ni lazima ampe posho ya elfu 10 msimamizi wa mchezo huo.  

Kweli ndani ya ndoa kuna siri kubwa mpaka leo bibi harusi huyo yuko ndani akikarangiza hajui maswahiba yanayompaka mumeweke ambaye ili asionekena mnyonge hakumshirikisha mkewe kwenye jambo hilo.

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...