...Baadhi ya wafanyabishara nao waliemau kujaza takatata kwenye Viroba na kuzitupa barabarani wakifuata nyazo zilizofanywa na wafanyakazi wa Manispaa
Lundo la tope likitelekezwa barabara ya Nane nane kuelekea Makaburi ya Kolla
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Kuelekea Manispaa ya Morogoro kuwa jiji Maoni ya Mwandishi wa Mtandao huu aliyoanza kuyatoa jana yanaendelea tena leo.
Baada ya kutoa Maoni hayo kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inavyoelekeza kwamba kila Mtanzania anahaki ya kutoa Maoni yake kwenye jambo lolote Pasina kuvunja sheria za nchi hivyo Mwandishi huyo anaishi kwenye kifungu hicho.
Kama hiyo haitoa Mwandishi huyo anakofia ya Pili ya kufanya hivyo ambapo kazi ya Mwandishi wa habari ni Kuelemisha, Kuburudisha, Kuhabarisha na kukosoa. Sasa hapa anapembea na kipengele cha kukosoa
Kwenye maoni hayo aliyoyatoa alidadavua mengi huku akiahidi kukatiza kwenye barabara Mpya za kiwango cha Lami zilizopo eneo la Nane nane Area Five Kata ya Kichangani zilizojazwa uchafu wa vifusi vya tope na watumishi wa Manispaa.
Jana majira ya asubuhi Mwandishi huyo alikatiza kwenye barabara hizo mbili ile inayotoka Nane nane kuelekea Makaburi ya Kola na ile inayotoka Nane nane eneo la maegesho ya Malori kuelekea Kichangani na kushuhudia uchafu huo.
Baada ya kufika kwenye barabara hizo zilizojengwa miaka 2 iliyopita Mwanahabari huyo alishuhudia lundo la tope zilizotolewa kwenye mifereje na kutelekezwa kwenye barabara hizo eneo la watembea kwa Miguu hali iliyopelekea wananchi kupita katikati ya barabara jambo ambalo ni hatari kiusalama.
Kama hiyo haitoshi baadhi ya wafanyabiashara wanao fanyabiashara kando kando ya barabara hizo eneo la Maegesho ya Malori hasa kina Mama Ntili baada ya kuona watumishi hao wa manispaa wametelekeza uchafuo huo kwenye maeneo yao nao wameamua kutupa viroba vya takatika kwenye eneo hilo hilo kama inavyoonekana Pichani.
Wakizungumza na Mtandao huu baadhi ya wafanyabiashara hao wamewatupia lawama wafanyakazi hao wa Manispaa kwa kujaza tope kwenye biashara zao” Angefanya hivi mwananchi wa kawaida Maafisa Afya wa Manispaa wangempifa faini sasa wao wametoa tope zito kwenye mitalo zaidi ya wiki bila kuzoa kama hawana gari la kubeba uchafuo huo kwa nini wameutoa kwenye mifereji?,alisema Mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Tunaelewa kuelekea Msimu huu wa Mvua Wafanyakazi wa Manispaa wanafanya kazi ya kuzibua Mifereji ili maji yapite bila kuzalisha mafuriko, lakini pia sio busara kutoa tope hilo chafu na kulitelekeza kwenye barabara mpya mbaya zaidi kwenye makazi ya wananchi wanaofanya biashara za vyakula.
Japo sijasoma vizuri Mwongozo wa Taifa wa Vigezo kupandisha hadhi Maeneo waishio watu,lakini Mwandishi anaamini moja ya Vigezo hivyo ni mpangilio mzuri wa Mji sambamba na usafi wa Mji husika.
Tujiulize Maswali Mepesi tu Je kwa hali hii ya Muonekano wa Picha hizi za uchafu juhuzi zetu la kuifanya Manispaa yetu ya Morogoro kuwa jiji zitaza matunda?
Panapo majaliwa ya mwenyezi Mungu kesho stori hii itaendelea kwa kurusha hewani picha za wafanyabiashara ndogo ndogo’Wamachinga’ wakizagaa hovyo katikati ya Mji huo huku baadhi yao wakipanga bidhaa zao barabarani ikiwa ni kinye cha sheria.
No comments:
Post a Comment