Mjane wa marehemu Bi Maimua ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM tawi la MkundiPadri Elia akimwagia maji ya baraja jeneza lililobeba
mwili wa mpendwa wetu Tonny Ntukula
Marehemu Tonny enzi za Uhai wake...Mh Abood mwenye shati la mistari stari akiwasili eneo la msiba huku akisindikizwa na madaka kibao wa CCMMhe Abood kulia akisalimiana na Zamoyoni Mogella
waoshuhudia tukio hilo
ni babau wa shiza Kichuya Mzee lbrahim Mangwende mwenye bagharashia kichwani na
mwenye nguo nyeusi ni mke wa zamoyoni Mogella
Mhe Abood kushoto na Zamoyo Mogella wakipozi mbele ya
kamera za Mtandao Pendwa wa Shekidele, kwenye msiba wa Tony Ntukula jana jioni
Mh Diwani wa Kata ya Mkundi ambaye pia Mkurugenzi Mkuu
wa Chuo Cha Uandishi wa habari Morogoro Mh Seif Chomoka akishukuru baada ya
kutambulishwa kwenye msiba huo.
Mh Abood akizungumza kwenye Msiba huo ......
akimkabidhi
rambimbi baba mdogo wa marehem
Mwenyekiti wa tawi kuu la Yanga Mkoani Morogoro lssa
Kitukwa maarufu lssa Chabala alikabidhiwa kitengo cha kijiko akitabasamu baada
ya kuiona kamera ya Mtandao huu
Sophia Ntukula ambaye pia ni Mjumbe wa serikali ya
Mtaa wa River Side akipokea rambi rambi kutoka kwa watu mbali mbali
Mchezaji nyota wa zamani wa Simba Reli na timu ya
Taifa Zamoyoni Mogella mwenye miwani akisalimiana na Mzee lbrahim Mangwende
ambaye ni babu wa shiza Kichuya. aliyeketi chini ni mke wa Mogella
Mchezaji wa Shujaa Mbaraka Denis akimsarimia Mzee
lbrahim Mangwende ambaye ni babu mzaa mama wa mchezaji wa zamani wa Simba Shiza
Kichuya ambaye kwa sasa anakipiga Namungo wa Lindi
Baadhi ya wachezaji wa zamani walishiriki mziba huo beki wa zamani wa Reli ya Morogoro Ally Kaliati Kidevu[mwenye shati nyeusi.
Winga wa zamani wa Reli ya Julius NgawambalaGari lililobeba viongozi wa Chadema Jimbo la Morogoro Katibu wa CCM Kata ya Mkundi akizungumza ...Baada ya katibu huyo kuzungumza wasaidizi wake walimkabidhi bahasha ya Pole mwenye kiti wao wa tawi la Mkundi Bi Maimuna
Nauma sana wanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya
sekondari Mkundi wamejichangisha na kupata kiasi cha shilingi elfu 40
walizomkabidhi dent mwenzao aliyefiwa na mpendwa baba yake.
Dent huyo baada ya kupokea
pesa hizo aliangua kilio huku akiwakumbatia wanafunzi wenzake kwa kumfariji
kwenye kindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzazi wake.
Baadhi ya waombolezaji
walishindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio kwa sauti ya juu baada ya
kushuhdia tukio hilo.
...Bint wa kwanza wa marehemu anayesoma kidato cha kwanza shule ya sekondari kata ya MkundiBaadhi ya wanafunzi wakimuaga baba mzazi wa mwanafunzi mwenzao,,,,,Ndugu wa Mareheme akisaidia kwenda kutoka heshima zake za mwisho kwenye mwili wa mpendwa wao.....Baada ya ibada kwisha mwili uliingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea makaburiniMh Abood akiongoza msululu wa magari kuelekea makaburini
Na Dunstan
Shekidele,Morogoro.
TAJIRI anayetajwa kuwa namba
moja mkoani Morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood jana ameongoza Mamia ya
wananchi kumzika dereva Maarufu wa
Magari Makubwa Mkoa wa Morogoro Marehemu Tony Agustino Ntukula[42].
Marehemu Tony aliyewahi
kuendesha Malori kwenye Kampuni kubwa ya Ujenzi wa barabara ya NCC na kampuni
ya Ujenzi wa Reli ya Mwendo Kasi ya Bam Enteboton Yapi Markezi alifariki dunia Novemba 21 na
kuzikwa kwenye Makaburi ya familia yao
yaliyopo Bingwa Manispaa ya Morogoro.
Kabla ya kwenda kumpunzisha
kwenye nyumba yake ya Milele Umati Mkubwa wawatu ukiongozwa na Makada wa CCM na
wachezaji Maarufu wa zamani wa soka akiwemo Zamoyoni Mogella walishiriki ibada
ya kumuombea Marehemu ilitofanyika nyumbani kwao Mtaa wa River Side Kata ya
Mwembesongo.
lfahamike Mke wa Marehemu Bi
Maimuna Semandua ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mkundi, dada wa Marehemu Bi
Sophia Ntukula ni Mjumbe wa Seriali ya Mtaa wa River Side kwa leseni ya CCM na
baba wa Marehemu Hayati Agustino Ntukula enzi za Uhai wake alikuwa mchezaji
mahiri wa timu ya Shujaa ambayo inaundugu na timu ya Simba ya Jijini Dar.
Kwa sasa tawi kuu la Simba la
Mkoani Morogoro linajulikana kwa jina la tawi la Shujaa.
Hivyo Mwandishi wa Mtandao huu aliwashuhudia
baadhi ya wachezaji nyota wa zamani kwenye msibani huo baadhi yao ni
Zamayoni Mogella aliyewahi kuzitumikia timu za Reli Moro, na Simba,
Julius Ngawambala, Ally Kidevu[Reli] na Mbaraka Dens aliyeitumikia Shujaa. Watu
wengine mashuhuri walioshuhudia na Mwandishi wa Mtandao huu ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro’MSJ’kilichopo Mkundi Seif Chomoka ambaye pia ni Mh diwani wa Kata
ya Mkundi aliyeutumia Ustahiki Meya kwa takribani wiki Moja kabla ya uondolewa
kwa sababu zinazodai za kikanuzi za Uchaguzi. Akizungumza na Mwandishi wa
habari hizi Mh Chomoka alisema amesigitishwa sana na kifo hicho cha Mume wa kiongozi wake
wa Chama kwenye Kata hiyo ya Mkundi.
”Shekidele Mke wa Marehemu ni
Mwenyekiti wangu wa tawi la CCM Mkundi hivyo Msiba huu ni wetu sote”alisema Big
Boss huyo wa Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro.
Watu wengine mashuhuli
walionaswa na Mwandishi wa habari hizi ni Viongoiz wa Chadema Jimbo la Morogoro
Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye
Msiba huo ikiwemo tukio la Mh Abood kuwashukia watuwanaowatapeli wananchi
kwenye msaadawake wa mabasi ya kuziki.na tukio la Pili la Padri kuwa makavu
watu wanatoa pesa nyingi kwenye msiba ili hali kabla ya marehemu kufariki dunia
hawakujitokea kutoa pesa za matibabu wakati taarifa za ugonjwa walikuwa nazo.
WASIFU
WA MAREHEMU.
Wasifu wa marehemu uliosomwa
na baba mdogo wa marehemu ulidai kwamba Marehemu Tonny alizaliwa Septemba
17-1980 Mtaa wa River Side.
Baada ya kuhitimu shule ya msingi na Sekondari Mwaka 1996
alijiunga na Chuo cha Ufundi Stand VETA katika fani ya udereva wa Magari
Makubwa na kuhitimu mafunzio hayo 1999.
Wasifu huo umezidi kubainisha
kwamba Marehemu ameanza kuugua ugongwa wa Figo toka Mwaka 2021 hadi alipokutwa
na umauti kwa ugongwa huo Novembe 21-2022.
Marehemu ameacha Mjane mmoja
na watoto wawili. Katika kupokea rambi rambi wanafunzi wa Kidato cha Kwanza
Shule ya Sekondari Mkundi wanaosoma darasa moja na mtoto wa kwanza wa marehmu
waliliza watu wengi baada ya kutangaza kujichangia kiasi cha shilingi elefu 40
na kumkabidhi dent mwenzao kama pole kwa
kufiwa na Mpendwa baba yake.
Baada ya kupokea pesa hizo
mtoto huyo aliangua kilio na wawakumbatia wanafunzi hao waliovaa sale za shule
ambali tukio hilo
kwenye picha hapo chini.
Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe.
Tangulia kamanda Tony Bonge tutaonana baadae nafarijika
nilifika mara kwa mara kukujua hali wakati ukiwa kitandani ukiendelea kupigania
uhai wako.