Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, November 26, 2022

UDAKUZI SPESHO.   MWANAUME AVUNJA BANDA LA MAMA NTILIE BAADA YA KUMFUMANIA.


Mdakuzi wa Mtandao huu[kulia] akipakia mbao hizo huku wakiangua vicheko wakati akisimuliwa tukio hilo na TOT.
Mbao hizo zikiwasili nyumbani wa Mdakuzi


 Mwandishi wa Mtandao huu akiwa Mikuni ba usafiri wake wa Pikipiki ya Mwendo kasi

 

Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro

 

AMANI ya Mwenyezi Mungu na iwe juu yenu.

 

Ama baada ya salamu Mdakuzi wa Mtandao Pendwa wa Shekidele anakurambisha Udakuzi wa Mwanaume mmoja [jina kapuni] akidaiwa kubomoa banda la chakula alilomjengea Mchepuko wake baada ya kumfumani akiibanjua amari ya 6 na dereva wa boda boda  ndani la banda hilo lililojengwa wiki iliyopita kwa gharama kubwa.

 

 Mara baada ya kutoke kwa valangati hilo lililojaza Nzi kibao mtaani hapo baadhi ya Nzi hao walimjuliza Mtakuzi ambaye alitinga eneo la tukio na kukuta tayari banda hilo la Mama Ntilie limeshavunjwa.

 

“Shekidele umechelewa  Jamaa baada ya kumfumania mpenzi wake ndani ya banda hili kamua kulivunja ambapo mabati mapya na mbao mpya kaenda kuziuza bei ya kutupa kwa yule jamaa anayefanya biashara ya kuuza vifaa ya ujenzi vilivyotumika pale Mji Mpya jirani na kituo cha Polisi ukifika pale yule jamaa ambaye alishiriki kubomoa banda hili atakupa habari kamili ya tukio hili”alisema shuhuza mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake lisitaje popote.

 

 Baada ya kurambishwa Ubuyu huo Mbichi kabisaa uliokolea rangi  Mdakuzi wa Mtandao huu alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendo kasi hadi kwa muuza vifaa hivyo vya ujenzi aliyefahamika kwa jina la TOT.

 

Alipotakiwa kuelezea tukio hilo awari TOT alionekana kukwepa kulizungumzia, baada ya kuligundua hilo Mdakuzi wa Mtandao huu aliyehitimu shahada ya Udakuzi nchini Kiuba alitumia mbinu za kishushu na TOT akifunguka kila kitu msikie akisimulia A-Z fumanizi hilo.

”Shekidele ni kwetu tukio hilo limetokea jana hawa wanawake zetu baadhi yao ni washenzi kuna jamaa yangua anafamilia yake lakini kama unavyojua tena alikuw ana mahusiano ya kimapenzi na mchepuku wake ambao unafanya biashara ya chakula’Mama Ntile’ hivyo kama unavyojua msimu wa mvua umeanza na lile banda lilikuw abovu bovu limeelezwa na maboksi.

 

Hivyo Jamaa uangu kaamua kusambaza upendo kwa kuvunja banda hilo bovu na kujenga banda lingine imara akinunua mabati mabya na mbao za kenchi mpya zilizopakwa dawa ya kuzuia kuliwa na wadudu.

 

 Chaajabu baada ya banda hilo kukamilika baadhi ya wambea walimtonya jamaa kwamba kila siku Mama Ntilie huyo akimaliza chakula hujifungia ndani ya banda hilo na dereva mmoja wa boda boda.

 

Jamaa yangu juzi usiku katoloka kwa mkewe kaenda kwenye banda hilo na kukuta boda boda iko nje huku mlango wa banda hilo ukiwa umefungwa kwa ndani”alisema TOT na kuendelea kumwaga utamu wa tukio hilo.

 “Jamaa aligonga mlango mwanamke huyo bila kujua kwamba anayegoma ni Bwana’ke kwa vile alishazoe kwamba kwa muda huo Kichwa chake hicho kinakuwa kwa mkewe alifungua mlanga na machoyake yakukutana na sura ya Bwana’ke huyo ambaye alimuliza swali moja tu kwamba nilikujengea banda hili ili ilifanye gest ya kuingiza mabwana nazo?.

 

 Mbona awari lilivyokuwa wazi hukufanya ushenzi huu ndani ya banda hivyo kesho nalivunja banda hili nachukua vifaa vyangu huyu boda boda wako akujenge banda lingine muendelee kufanya usheni wenu kwa uhuru.

 

 Kweli kesho yake jamaa kaita wale wale mafunzi waliojenga wakalivunja banda lile na kuja kuniuzia mabati na mbao mabati yote nimeshayauza asubuhi zimebaki hizi mbao tu”alimalizia kusema TOT

 

Mdakuzi wa Mtandao huu alizinunua mbao hizo kwa bei chipa  kazipakia kwenye Kitoyo na kuzipeleka nyumbani wake kuzitumia kuezekea banda la kuku.

Nilipofika nyumbani wakati naendelea kushusha mbao hizo nikawasha Luninga nikachomeka Frash yenye wimbo wa taarabu ulioimbwa na Marehemu lssa Kijoti unaosema ‘kanunua simu kampa demu walivyoachana kamnyang’anya.’

 

 Mara nyingi napendelea kusikiliza wimbo huo nikiwa na hudhuni kubwa kwani kifo cha Kijoti nilikishuhu ambapo wakati kundi lao la  Five Star Morden Taarabu likitokea jijini Mbeya kwenye shoo walipofika ndani ya Mbugha ya wanyama ya Mikumi usiku mnene kuna Lori lililobeba mbao liliharibika eneo la barabara.

 

Huku Kijito akiwa ameketi siti ya Mbele kwenye basi ndogo aina ya Coaster ililigonga Lori hilo kwa nyuma na mbao hizo zilimtoboa tumbo Kijito na kutenganisha mwili wake kiwili wili na semu ya miguu.

 

Wasanii wengi wengi walikuga kwenye ajari hilo lakini kwa mapenzi ya Mungu rafiki yangu Ally Juma Mgona Maarufu Ally J aliyeketi siti ya nyuma ya basi hilo ni miongoni mwa watu wachache walionusurika kwenye ajari hiyo. Mara baada ya kutoka ajari hiyo Mwandishi wa Mtandao huu alipigia gia Pikipiki yake ya Mwendo kasi hadi eneo la tukio kwenye kukusanya habari alipofika alishuhudia  ajari hiyo Mwanzo mwisho huku baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Doma walidaiwa kukwapua baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani ya basi hilo.

                            


 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...