Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, November 27, 2022

CHEDEMA, CCM WASHIRIKI MAZISHI YA DEREVA WA MALORI.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Morogoro Moses akifunguka kikao cha Mafunzo ya Mawakala wa Chadema Digital mOctoba 16 mwaka huu
Gari lililobeba viongozi wa Chedema Jimbo la Morogoro likiwa eneo la Msibani
Mwenyekiti kiti  wa Chadema wilaya ya Morogoro [Mwenye koti na jezi ya Simba ndani akitoa heshima zake kwa marehemu kaka yake
Mjane wa marehemu Bi Maimuna ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mkundi
MNec Aziz Abood[mwenye shati la mistari stari] akiwasili kwenye msiba huo huku akisindikizwa na kundi la Makada wa CCM.

 Mwenye gauni la kitenge aliyeweka mikono tumboni ni Bi Geloda Kimilila ambaye ni Mama mzazi wa Mwenyekiti  huyo wa Chadema akiwa mbele ya jeneza la Mpendwa Mwanaye ambaye ni mtoto Pekee wa kiume wa Marehemu kaka yake


 

            Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

VIONGOZI Wakuu wa  Vyama Vikuu vya Siasa nchini Chama Cha Mapinduzi’CCM’ na Chama Cha Demokrasia na Maendele ‘Chadema’ Jimbo la Morogoro wiki iliyopita waliweka kando itikadi zao na kushirikiana kwa pamoja kumzika dereva Maarufu wa malori nchini Marehemu Tonny Ntukula.

 

Viongozi hao wa CCM na Chadema wameunganisha na Familia hiyo ya marehemu ambapo baadhi ya wanafamilia hao wamegawanyika wengine ni Viongozi wa CCM na wengine ni Viongozi wa Chadema.

 

Mdogo wa Marehemu Moses Kimilila ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Morogoro huku Mke wa Marehemu Bi Maimua Semambua ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mkundu huku dada wa Marehemu Sophia Ntukula pia akiwa Mjumbe wa serikali ya Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo kwa leseni ya CCM.

 

Baadhi ya Vigogo wengine wa CCM walioshuhudiwa na Mwandishi wa Mtandao huu kwenye msiba huo ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ‘M -NEC’ Aziz Abood Katibu wa CCM Kata ya Mkundi na Diwani wa Kata ya Mkundi kwa leseni wa CCM Seif Chomoka.

 

Binafsi nahifahamu vizuri familia hiyo ya Ntukula niliyoishi nayo kwa miaka mingi Mtaa mmoja wa Makaburi B Kata ya Mji Mpya, Mama wa Mwenyekiti huyo wa Chadema  Bi Geloda  Kimilila  anazaliwa tumbo moja na Marehemu Agustino Ntukula baba mzazi wa Marehemu Tony.

 

 lfahamike pia familia hiyo akiwemo Mwenyekiti wa chadema na Sophia Ntukula na Magreth Ntukula wote ni wadau wakubwa wa Mitandao Pendwa  ya shekidele www.shekideletz.blogspot.com. lnstagran facebook ya Shekidelemkudesimba na Dustan shekidele.

 

Hivyo baada ya kusoma habari hizo kwenye Mitandao hiyo yenye wasoma wengi pande zote za dunia, Mwenyekiti huyo wa Chadema Kamanda Moses ni niongoni mwa wanafamilia waliompigia simu Mwandishi wa Mtandao huu akimpa shukrani kwa kushiriki mazishi ya mpendwa wao sambamba na kutumia mitandao yake kuripoti matukio yote ambapo watu waliokuwa mbali walipata taarifa za msiba huo A-Z kupitia Mtandao huo wa shekidele.

        

 


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...