Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, November 24, 2022

ABOOD ATOA ONYO KWA MATAPELI WANAOWATAPELI PESA WAFIWA KWENYE MSAADA WA MABASI YAKE YA KUZIKIA.

Moja ya basi la Abood likiwe msibani maeneo ya Mawenzi  Morogoro.
Mh Abood[kulia] akimpa Pole Zamoyoni Mogella alitevaa miwani ya giza.
....Mh Abood na Mogella akipozi mbele ya camera za Mtandao huu mara baada ya tukio hilo
    Mh Abood akitoa onyo hilo Msibani hapo.

 Mzee lbrahim Mangwende ambaye ni babu mzaa mama wa Winga wa Namungu Shiza Kichuya naye akimpa Pole Mogella aliyeketi chini mwenye nguo nyeusi ni mke wa Zamoyoni Mogella.Picha


            Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TAJIRI anayetajwa kuwa namba moja mkoani Morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Abdulaziz  Mohamed Abood ‘Maarufu Aziz Abood’ juzi ametoa onyo kali  kwa matapeli wanaowatapeli pesa wafiwa kwenye  mabasi yake anayoyatoa msaada kwa wafiwa.

 

Mh Abood alitoa Onyo hilo kwenye Msiba wa Mpwa wa Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars Zamoyoni Mogella’Golden Boy’marehemu Tonny Aguston Ntukula aliyefariki Novemba 21 na kuzikwa Novemba 23 kwenye Makaburi ya Bingwa Morogoro.

 

Baada ya kukamilika kwa lbada ya kumuombea Marehemu huyo iliyofanyika nyumbani kwao Mtaa wa River Side  Kata ya Mwembesono Mkoani hapa,baada ya kukamilika kwa lbada hiyo Muongozaji  alimkaribisha Mbunge huyo kuwasalimia wananchi wake sambamba na kutoa rambi rambi zake kwa familia ya marehemu.

 

Mara baada ya kuwapa pole kasha  kukabidhi rambi rambi zake kwa familia Mh Abood alisema.

 

”Naomba nitoe angalizo kwa wananchi wote wa Manispaa ya Morogoro kama mnavyofahamu kwa miaka mingi sasa nimekuwa na utamaduni wa kutoa mabasi yangu bure kwenye misiba.

 

 Nafanya hivi sio kwa sababu ya Ubunge  hapana nafanya hivyo nikitekeleza agizo la Mwenyezi Mungu la kututaka wanadamu tusaidiane kwenye shida na raha.

 

 Nasigitika kusema baadhi ya watu wasio na huruma wanatumia fursa hiyo kuwatapeli wafiwa, siku za hivi karibuni kumeibuka matapeli ukitokea msibani  kuwatapeli wafiwa wakiwataka wachangie elfu hamsini za mafuta”alisema Abood kwa Jazba na kuendelea kusema.

 

”Hao ni matapeli mtu yoyote akikuambia hivyo toa taarifa tumkamate, natoa mabasi bure kwenye misiba yote pia hata ukiwa na shughuri  nyingine inayokusanya watu wengi kutoka eneo moja kwenda lingine pia natoa mabasi bure bila gharama yoyote hata huyo dereva anayekuja analipwa na ofisi yangu ubwabwa wanaokula waombolezaji na yeye mumpe huo huo”alimalizia kusema tajiri huyo na kupewa zawadi ya makofi kutoka kwa umati mkubwa wawatu uliofulika kwenye msiba huo

 

lfahamike Mh Abood Kipenzi cha wanamorogoro anayemilikia Mabasi, Malori, Viwanda na Vyombo vya habari, alianza kutoa msaada huo wa mabasi ya kuzikia zaidi ya miaka 20 kabla  hajawa mbunge ambapo kwa mara ya kwanza alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Morogoro mwaka 2010 akiendelea kutetea kiti hicho mpaka sasa


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...