Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, November 24, 2022

TAJIRI ABOOD AONGOZA MAMIA YA WANANCHI MORO KUMZIKA DEREVA WA MALORI.


Mjane wa marehemu Bi Maimua ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM tawi la Mkundi

Padri Elia akimwagia maji ya baraja jeneza lililobeba mwili wa mpendwa wetu Tonny Ntukula

                      Marehemu Tonny enzi za Uhai wake
...Mh Abood mwenye shati la mistari stari akiwasili eneo la msiba huku akisindikizwa na madaka kibao wa CCM

Mhe Abood kulia akisalimiana na Zamoyoni Mogella waoshuhudia tukio hilo ni babau wa shiza Kichuya Mzee lbrahim Mangwende mwenye bagharashia kichwani na mwenye nguo nyeusi ni mke wa zamoyoni Mogella

Mhe Abood kushoto na Zamoyo Mogella wakipozi mbele ya kamera za Mtandao Pendwa wa Shekidele, kwenye msiba wa Tony Ntukula jana jioni

Mh Diwani wa Kata ya Mkundi ambaye pia Mkurugenzi Mkuu wa Chuo Cha Uandishi wa habari Morogoro Mh Seif Chomoka akishukuru baada ya kutambulishwa kwenye msiba huo.


 

Mh Abood akizungumza kwenye Msiba huo
......

 akimkabidhi rambimbi baba mdogo wa marehem


Mwenyekiti wa tawi kuu la Yanga Mkoani Morogoro lssa Kitukwa maarufu lssa Chabala alikabidhiwa kitengo cha kijiko akitabasamu baada ya kuiona kamera ya Mtandao huu


Sophia Ntukula ambaye pia ni Mjumbe wa serikali ya Mtaa wa River Side akipokea rambi rambi kutoka kwa watu mbali mbali

Mchezaji nyota wa zamani wa Simba Reli na timu ya Taifa Zamoyoni Mogella mwenye miwani akisalimiana na Mzee lbrahim Mangwende ambaye ni babu wa shiza Kichuya. aliyeketi chini ni mke wa Mogella  

Mchezaji wa Shujaa Mbaraka Denis akimsarimia Mzee lbrahim Mangwende ambaye ni babu mzaa mama wa mchezaji wa zamani wa Simba Shiza Kichuya ambaye kwa sasa anakipiga Namungo wa Lindi

Baadhi ya wachezaji wa zamani walishiriki mziba huo beki wa zamani wa Reli ya Morogoro Ally Kaliati Kidevu[mwenye shati nyeusi.

Winga wa zamani wa Reli ya Julius Ngawambala
Gari lililobeba viongozi wa Chadema Jimbo la Morogoro
                Katibu wa CCM Kata ya Mkundi akizungumza
...Baada ya katibu huyo kuzungumza wasaidizi wake walimkabidhi bahasha ya Pole mwenye kiti wao wa tawi la Mkundi Bi Maimuna


Nauma sana wanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Mkundi wamejichangisha na kupata kiasi cha shilingi elfu 40 walizomkabidhi dent mwenzao aliyefiwa na mpendwa baba yake.

Dent huyo baada ya kupokea pesa hizo aliangua kilio huku akiwakumbatia wanafunzi wenzake kwa kumfariji kwenye kindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzazi wake.

 

Baadhi ya waombolezaji walishindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio kwa sauti ya juu baada ya kushuhdia tukio hilo.


...Bint wa kwanza wa marehemu anayesoma kidato cha kwanza shule ya sekondari kata ya Mkundi
Baadhi ya wanafunzi wakimuaga baba mzazi wa mwanafunzi mwenzao
,,,,,Ndugu wa Mareheme akisaidia kwenda kutoka heshima zake za mwisho kwenye mwili wa mpendwa wao

.....Baada ya ibada kwisha mwili uliingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea makaburini

Mh Abood akiongoza msululu wa magari kuelekea makaburini

 

 

         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

TAJIRI anayetajwa kuwa namba moja mkoani Morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini  Mh Aziz Abood jana ameongoza Mamia ya wananchi kumzika  dereva Maarufu wa Magari Makubwa Mkoa wa Morogoro Marehemu Tony Agustino Ntukula[42].

 

Marehemu Tony aliyewahi kuendesha Malori kwenye Kampuni kubwa ya Ujenzi wa barabara ya NCC na kampuni ya Ujenzi wa Reli ya Mwendo Kasi ya Bam Enteboton  Yapi Markezi alifariki dunia Novemba 21 na kuzikwa kwenye Makaburi ya familia yao yaliyopo Bingwa Manispaa ya Morogoro.

 

Kabla ya kwenda kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele Umati Mkubwa wawatu ukiongozwa na Makada wa CCM na wachezaji Maarufu wa zamani wa soka akiwemo Zamoyoni Mogella walishiriki ibada ya kumuombea Marehemu ilitofanyika nyumbani kwao Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo.

 

lfahamike Mke wa Marehemu Bi Maimuna Semandua ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mkundi, dada wa Marehemu Bi Sophia Ntukula ni Mjumbe wa Seriali ya Mtaa wa River Side kwa leseni ya CCM na baba wa Marehemu Hayati Agustino Ntukula enzi za Uhai wake alikuwa mchezaji mahiri wa timu ya Shujaa ambayo inaundugu na timu ya Simba ya Jijini Dar.

 

Kwa sasa tawi kuu la Simba la Mkoani Morogoro linajulikana kwa jina la tawi la Shujaa.

 

 Hivyo Mwandishi wa Mtandao huu aliwashuhudia baadhi ya wachezaji nyota wa zamani kwenye msibani huo baadhi yao ni  Zamayoni Mogella aliyewahi kuzitumikia timu za Reli Moro, na Simba, Julius Ngawambala, Ally Kidevu[Reli] na Mbaraka Dens aliyeitumikia Shujaa. Watu wengine mashuhuri walioshuhudia na Mwandishi wa Mtandao huu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro’MSJ’kilichopo Mkundi  Seif Chomoka ambaye pia ni Mh diwani wa Kata ya Mkundi aliyeutumia Ustahiki Meya kwa takribani wiki Moja kabla ya uondolewa kwa sababu zinazodai za kikanuzi za Uchaguzi. Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mh Chomoka alisema amesigitishwa sana na kifo hicho cha Mume wa kiongozi wake wa Chama kwenye Kata hiyo ya Mkundi.

 

”Shekidele Mke wa Marehemu ni Mwenyekiti wangu wa tawi la CCM Mkundi hivyo Msiba huu ni wetu sote”alisema Big Boss huyo wa Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro.

 

Watu wengine mashuhuli walionaswa na Mwandishi wa habari hizi ni Viongoiz wa Chadema Jimbo la Morogoro

 

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye Msiba huo ikiwemo tukio la Mh Abood kuwashukia watuwanaowatapeli wananchi kwenye msaadawake wa mabasi ya kuziki.na tukio la Pili la Padri kuwa makavu watu wanatoa pesa nyingi kwenye msiba ili hali kabla ya marehemu kufariki dunia hawakujitokea kutoa pesa za matibabu wakati taarifa za ugonjwa walikuwa nazo.

 

     WASIFU  WA MAREHEMU.

Wasifu wa marehemu uliosomwa na baba mdogo wa marehemu ulidai kwamba Marehemu Tonny alizaliwa Septemba 17-1980 Mtaa wa River Side.

 

 Baada ya kuhitimu  shule ya msingi na Sekondari Mwaka 1996 alijiunga na Chuo cha Ufundi Stand VETA katika fani ya udereva wa Magari Makubwa na kuhitimu mafunzio hayo 1999.

 

Wasifu huo umezidi kubainisha kwamba Marehemu ameanza kuugua ugongwa wa Figo toka Mwaka 2021 hadi alipokutwa na umauti kwa ugongwa huo Novembe 21-2022.

 

Marehemu ameacha Mjane mmoja na watoto wawili. Katika kupokea rambi rambi wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Mkundi wanaosoma darasa moja na mtoto wa kwanza wa marehmu waliliza watu wengi baada ya kutangaza kujichangia kiasi cha shilingi elefu 40 na kumkabidhi dent mwenzao kama pole kwa kufiwa na Mpendwa baba yake.

 

Baada ya kupokea pesa hizo mtoto huyo aliangua kilio na wawakumbatia wanafunzi hao waliovaa sale za shule ambali tukio hilo kwenye picha hapo chini.

  

Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe.

Tangulia kamanda Tony Bonge tutaonana baadae nafarijika nilifika mara kwa mara kukujua hali wakati ukiwa kitandani ukiendelea kupigania uhai wako.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...