Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, November 30, 2022

UDAKUZI SPESHO.   MBOGA MAJI WA IHEFU AIBUKIA MTO JANGWANI DAR.


 

 

Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

KWELI Maisha ya Soka la Tanzania ni kama Gwaride nyuma geuka wa Mwisho anakuwa wa kwanza na wakwanza anakuwa wa Mwisho.

 

Hali hiyo imetimia jana baada ya timu inayoshika mkia kwenye ligi kuu Tanzania Bara lhefu Fc ‘Wana Mbogo Mji’ wenye maskani yao katikati ya Mashamba ya Mpunga Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kuwafunga Wananchi’Yanga’ Wanaoongoza ligi hiyo kwa kuwachapa bao 2-1.

 

Ushindi huo umewatoa Mkiani lhefu na kupanda  nafasi 3 juu kupitia ngazi ya Yanga inayotajwa kuwa na kikosi chenye wachezaji wa dhamani kubwa kuliko timu yoyote nchini.

 

Gemu hiyo iliyomilikiwa na lhefu kwa takribani dakika zote 90 imepigwa  uwanja wa Highland Estate unaomilikiwa na Wana Mbogo Maji hao wanaonolewa na kocha wa zamani wa Yanga Juma Mwambusi’Mnyambara’mzaliwa wa Mbeya.

 

 Kipigo hicho nimevunja mbwembwe za wana yanga hao kupigiwa makofi kila walipocheza mchezo wa ligi kuu wakifurahia rekodi yao ya kutokufungwa mchezo yoyote’Unbeaten 49’ mfurulizo toka ligi ya msimu uliopita na kuweka rekodi mpya kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ikiwa timu pekee iliyocheza michezo  49 bila kufungwa.

 

Kwa masigitika Makubwa  Mbwembwe zao hizo ziliisha jana kwenye msitu wa mashamba ya Mbunga Mbarali,baada ya kufungwa na wakulima hao wa Mpunga  waliokuwa wakiburuza mikia kwenye ligi hiyo.

 

 Matokeo hayo ya kikatili  kwa Yanga yanasindikizwa na msemo wa wahenga unaosema kuna Majira Saa Mbovu nayo inasema Kweli.

 

Jana tetemeko la Mayele lilizimwa na Zoluba kali lililozalishwa na upepo mkali kutoka kwenye Mashamba ya Mpunga ya Mbarali ambapo Mayele alionekana kama joka la kibisa lisilokuwa na sumu mdomoni.

        

Licha ya kuwapa makavu wananchi kwenye Udakuzi hapo juu lakini pia nitakuwa mnafika kama wanafiki wengine kama sita dhamini mafanikio ya timu hiyo ya kunyakua ubingwa wa Ligi kuu, Ngao ya Jamii na F.A Cup.

 

 Kama hiyo haitoshi Yanga hao hao wameshangaza Afrika baada ya kuwafunga Waarabu wa Tunisia nyumbani kwao bao 1-0 na kukata tiketi ya kuingia makundi kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo ratiba ya makundi hayo inatarajiwa kupangwa Desemba 12.

 

lfahamike baadhi ya wachezaji wa Klabu hiyo ya Tunisia iliyofungwana Yanga kwa sasa tunawashuhudia wakiitumikia timu yao ya taifa ya Tunisia kwenye fainali za Kombe la Dunia hivyo yanga sio timu ya kumchezo mchezo imewapiga watu wa viwango vya kombe la dunia sio timu nyingine zimetinga makundi kwa kuzifunga timu vya viwango vya Afrika.

 

 

lkumbukwe  licha ya kufungwa jana timu hiyo yenye Maskani yake Makutano ya barabara za Mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo Dar bado inaongoza ligi hiyo ikiwa na Point 32 huku akiwa na mchezo  mmoja wa Kiporo dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa keshokutwa Novemba 5 Kwa Mkapa Dar.

 

 Baada ya kiporo chao cha Mihogo kuwachachia jana na kulazimika kulishwa viporo vya sahani 2 za Wali kutoka mashamba ya Mpunga Mbarali Mbeya, kwa sasa Yanga wako kwenye mahesabu makali ya kupasha moto kipora chao hicho cha keshokutwa dhidi ya Wajera jera hao wanaopiga pira Gwaride’.

 

Namalizia Udakuzi huu kwa kuwatia moyo Mashabiki wa Yanga siku zote Mwanamke mwenye watoto adui yake namba moja ni yule Mwanamke Mgumba ambaye hafurahi kuona mwanamke mwenzake anawatuma watoto zake dukani  huku yeye hana mtoto hata mmoja wa kumtuma dukani.

 

Shekidele hana hatia nimeamua kuandika Udakuzi huo kufuatia kichapo hicho cha Yanga kufuatia baadhi ya mashabiki timu hiyo walikuwa na ngebe kali kwa mashabiki wa timu nyingine wakijinasibu kwamba watifikisha mechi 100 bila kufungwa.

 

  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...