Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 28, 2022

BONDIA CHEKA AOPOA DEMU WA KIZUNGU UJERUMANI.

Bondia Cosmas Cheka akiwa na Mchumba'ke wa kizungu

Cheka akiumwagilia Moyo viwanj vya Ujerumani na Mpenzi wake wa kizungu





 


                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

BONDIA Maarufu wa ngumi za kulipwa nchini Cosmas Cheka anayeishi nchini ujerumani kwa sasa amefanikiwa kumiliki  demu wa kizungu zaia wa Ujerumani.

 

Cheka ambaye ni Mdau Mkubwa wa Mtandao Pendwa wa shekidele alimtambulisha Mpenzi wake huyo kwa Watanzania wenzake alipofanya  Mahojiano Maalumu  na Mtandao huu leo asubuhi kupitia Ukurasa wa Facebook  wa Dustan Shekidele.

 

Alipotakiwa kutana jina la Mchumba’ke huyo Cheka alisema Mtarajiwake wake huyo anaitwa Casselin Phil raia wa Ujeruamani aliyeangukia kwenye penzi zito la mtoto wa Kimakonde ‘Chinga kutoka Mtwara aliyekulia Mkoani Morogoro.

 

 Alipoulizwa hapo Ujerumani anaishi Mji gani na kwamba anampango wa kurejea nyumbani au ametekwa mazima na mtoto huyo mzuri wa Kijerumani Cheka alicheka kisha akajibu.

 

“ Shekidele kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutupa habari moto moto watanzani wengi wanaoishi huku Ujerumani ni wadau wakubwa wa Mtandao wako.

 

Binafsi  bila kuingia kwenye Mtandao wako naona kama sijashiba habari kwani napata habari za kusisimua za Tanzania hasa za nyumbani Morogoro kupitia Mitandao yako.

 

Nikijibu Maswali yako hapa Ujerumani naishi Mji wa  Berlin na huyu Shemeji yako, kuhusu kurejea  nyumbani lazima nirejee ingawa si kwa siku za  hivi karibuni kwani bado nipo nipo sana huku”alisema Cosmas ambaye ni mdogo wa damu wa bondia Maarufu nchini Francis Cheka’SMG.’

 

 Mara baada ya mahojiano hayo Cosmas alimtumia Picha kibao Mwandishi wa habari hizi akiwa na mkewe huyo Mteule.

Mtandao huu unamuombea kwa Mungu amfanyie wepesi Mtanzania mwenzetu,Mwana Morogoro mwenzetu kwenye mipango yake mbali mbali ya kimaisha.

 

Angalia Picha mbali mbali za Cosmas Cheka akiwa viwanja mbali mbali vya Ujerumani akiwa na My wake wa kitasha.

 

Akichanganya rangi Black and White.

 

Mitandao Pendwa ya shekidele inawasomaji wengi pande zote za dunia zikiwemo nchi za Ujerumani, Marekani. Blazil. China , Ufaransa Uarabuni. Denmack, Canada Japan.lndia nk

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...