Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
PADRI wa kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Padri Elia, katikati ya wiki hii amewapa Makavu baadhi ya watu wenye tabia ya kutoa mamilia ya pesa kwa marehemu huku wakikacha kutoa msaada wa matibabu akiwa mgonjwa.
Padri huyo ‘Janki’ alitoa kalipio hilo kwenye sehemu ya mahubiri yake aliyoyatoa kwenye msiba wa Marehemu Tonny Ntukula aliyeanza kuugua ugonjwa wa figo toka Mwaka 2021 hadi alipofariki dunia kwa ugonjwa huo juzikati Novemba 21-2022.
“Jambo jema na lenye faraja kwa Jamii na mbele za Mungu ni yule mtu anayetoa msaada wa Matibabu kwa Mgonjwa, kuna baadhi ya watu Mgonjwa anapohitaji Msaada wao wa pesa za kununua dawa wanakwepa lakini mgonjwa huyo huyo akifariki watu hao wanajitokeza kwa wingi wakishindano kutoa pesa nyingi za rambi rambi nahisi hizo pesa hazina msaada mkubwa kwa marehemu huyo zingekuwa na msaada pale alipokuwa akiupigania uhai wake pale kitandani ”alisema Padri huyo na kupigiwa makofi na baadhi ya waombolezaji waliofulika kwa wingi kwenye msiba wa Mpendwa wetu Tonny ‘Bonge’.Ntukula.
Katika kukadhia kalipi hilo Mwenyekiti wa Kigango cha Mji Mpya Mzee Cosmas Damiani alipigia Msumari kwa kutoa ushahidi wa kweli wa tukio hilo.
“Padri umesema kweli mimi ninaushahidi wa kweli wa jambo hilo,siku za nyuma nilikuwa na uguza mgonjwa wangu na pesa za matibabu zilihitaji laki mbili ili tuokoa maisha yake lakini kwa bahati mbaya pesa hizo zikuzipata kwa wakati hivyo mgonjwa wangu akafariki dunia.
Chaajabu kwenye msiba huo watu mbali mbali wakiwemo waliokuwa na taarifa za ugongwa huo walijitokea na kunipa rambi ramba za pesa kiasi cha milioni 2 na nusu sasa nikajiuliza pesa hizo wangenipa wakati ule wa ugonjwa zingesaidi kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha ya Mgonjwa wangu.
Hakuna shaka yoyote kwamba baadhi ya watu wanakufa kwa kukosa msaada wa pesa za matibabu”alisema Mzee Damiani ambaye ni mmoja wa Vigogo wa kanisa Kuu la Mt Patrick Jimbo la Morogoro.
No comments:
Post a Comment