Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, October 31, 2022

MATANGAZAJI MAARUFU 1TV NA RADIO ONE AMEVUNJIKA MGUU BAADA YA KUPATA AJARI YA PIKIPIKI.

                           Mkilanya kulia akimjulia hali Kapalatu
 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

MTANGAZAJI Maarufu wa Kituo  Maarufu cha Luninga Afrika Mashariki na Kati Cha lndependent Television Maarufu I.T.V ‘Super Bland’,Juma kapalatu amevunjika Mguu mmoja baada ya Pikipiki  aliyokuwa akiendesha akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi  jijini Dar es salaam kupata ajari.

 

  Baada ya kupata ajari hiyo alipata matibabu kwenye hospital mbali mbali za jijini Dar kabla ya hivi karibuni kuja mkoani hapa kwenye kituo cha Tiba asili cha Dr Kisome kilichopo Kihonda  Mkoani hapa. 

 

Kituo hicho kinachoongozwa na Dr bingwa wa Mifupa nchini Dr Kisome aliyewahi kupiga kazi hospital ya Tumbi Kibana kimejizolea umaarufu mkubwa nchini ambapo baadhi ya wachezaji nyota wa timu kubwa zikiwemo Simba na Yanga wanapovunjika Miguu hutibiwa kwenye kituo hicho na Dr Kisome ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mafisa kwa leseni ya CCM.

 

 lfahamikea Kapalatu kabla ya kutimikia ITV na Radio One alikuwa akipiga kazi Abood Media inayobeba Luninga ya  Abood Televison’ATV’ na  Abood Radio Abood Fm, Kapalatu pia ni Mwanachama hai wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro.

 

Hivyo juzi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya alifunga safari hadi kwenye kituo hicho na kumjulia hali Mwanachama wake kama wanavyoonekana wakiwa kwenye Picha ya pamoja nnje ya kituo hicho Mkilanya Kulia akimpa Pole  Kapalatu.

 

Leo asubuhi Mwandishi wa habari hizi alimpiga simu Kapalatu kwa lengo la kumjulia hali sambamba na kumhoji juu ya tukio hilo ambapo alipotakiwa kueleza ajari hiyo alisema.

 

 “Miezi miwili iliyopita nikiwa kwenye Pikipiki yangu kwenye majukumu yangu ya kikazi nilipata ajari Buguruni eneo la makutano ya barabara nikavunjika mguu mmoja  nilipata matibabu kwenye hospital kadhaa jijini Dar lakini baadae nikaona nije hapa nyumbani Morogoro kwenye Kituo cha Dr Kisome ambapo nashukuru baada ya kufika hapa na kupata matibabu naendelea vizuri sana tofauti na awari kabla sijafika hapa”alisema Kapalatu.

 

Mtandao huu unamuomba Mungu azidi kumponya ndugu yetu Kapalatu ili arejea kwenye majukumu yake ya mbali mbali yakiwemo hayo ya utangazaji.

 

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya alipohojiwa na Mtandao huu alisema.

 

” Ni kweli Shekidele juzi nilikwenda kumjulia hali mwenzetu Kapalatu  namshukuru Mungu kwa sasa anaendelea Vizuri baada ya kupata tiba pale kwa Dr Kisome” alisema Mkilanya  

 

Baadhi ya watangazaji wengine Maarufu waliotokea Abood Media na kutimkia Vyombo mbali mbali vya habari vya Jijini Dar ni  pamoja na Tumie Omar Radio One, Salum Mkambara Chanel Ten, Henry MabumoTBC’na Juma Kapalatu ITV.

 

Sunday, October 30, 2022

UJUMBE MZITO WA NENO LA MUNGU

Siku niliyompeleka hospital Mama Yangu Mpendwa niliyekaa tumboni mwake miezi 9 Bi. Tumain Samwel Juma ‘Mrs Shekidele’ kupima Typhoid.


 Nikiwa na bibi yangu Mzaa Mama Bi Kete Abdallah hii ni Mwaka 2017 kwenye sherehe yake ya kuzaliwa \Happy Birthday' iliyofanyika nyumbani kwake Gongola Mboto Banana Moshi Baa Jijini Dar es salaam alipotimiza miaka 101.

 Pichani mpendwa mke wangu wangu kipenzi my Number One bibi yangu akinipa wosia kwa Lugha ya Kisambaa. Mpendwa bibi yangu mwaka 2019 alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 103

ZABURI 71-6

 “ Nimekutegea wewe tangu kuzaliwa,ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,

Ninakusifu wewe daima.nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi na wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.

 

Kinywa changu kitajazwa sifa zako na heshima yako mchana kutwa”.Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya Octobar 30

           

 

Friday, October 28, 2022

TAARIFA

Never'Kamwe' Penzi la Mama haliishi nimevutiwa na maandishi ya Khanga hii hivyo moja ya zawadi nilizombebea Bi mkubwa ni pamoja na Khanga hii yenye ujumbe mzuri
Mwandishi wa Mtandao huu muda huu akiwa kituo cha Mafuta Chalinze Mkoa wa Pwani

 

TAARIFA.

Wadau wa Mtandao Pendwa wa Shekidele, takribani siku tatu sijaposti habari yoyote kwenye ukurasa huu,jambo ambalo sio kawaida.

 

Hii nimetokana na Mimi kwenda Dar es salaam juzi kumjulia hali Bi Mkubwa wangu aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi mbali mbali ikiwemo Malaria.

 

Mungu ni Mwema kwa sasa Mpendwa Mama yangu kipenzi aliyenileta hapa duniani amepata nafuu,muda huu niko hapa Chalinze naongeza Mafuta niendelee na safari ya kurejea Morogoro.

 

Hivyo maombi yenu yanahitajika ili niweze kufika salama niendelee na majukumu yangu ya kuwahabarisha wadau wa Mtandao Pendwa wa Shekidele.

 

Kuna watu walivyoniona na gari hiki jipya Dar na Moro walinipongeza wakihisi ni Mali yangu ukweli ni mwamba gari hili si Mali yangu  ni mali ya rafiki yangu aliyenisaidia kwani kwenye safari hii niko na ndugu yangu Mlemavu wa Miguu ambaye kupanda kwenye ngazi ndefu za basi kwake ni changamoto kubwa.

Naamini bila ufafanuzi huu  hapa humu kwenye Mtandao watu wengi wangeamini kwamba chombo hii ni mali yangu jambo ambalo sio kweli.

Nafurahi Mali sina lakini nimejaliwa kuwa na rasilimali watu, naamini hii ni mali kubwa kuliko mali nyingine.si dhani kama inafaida kuwa na mali za duniani huku hunamahusiano mazuri na watu wakiwemo majirani zako.

 

 

 

Tuesday, October 25, 2022

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI. WANENGUAJI WATIMULIWA KWENYE BAND KWA UTORO KAZINI.

Sabrina akitamburishwa kwenye band ya Maisha Mapya akitokea band ya Waluguru.



 Sabrina akiwajibika  wiki iliyopita baada ya kureja band yake ya Waluguru


Mourine V.A.R akiwasha Moto kwenye Jukwaa la Maisha Mapya. kabl ya kutimuliwa kwenye band hiyo kwa sababu za Utoro kazini.

Wanenguaji wa band ya Waluguru wakiuwasha Moto  nyuma yao ni Sabrina akishriki kwenye shoo hiyo


Rap Mahiri wa band ya Waluguru Og Mudizo akiwakoreza wanenguaji wa band Wanengauji wa band ya Waluguru wakiwajibika Jukwaani

Safu ya Waimbaji wa band ya Waluguru wakiwajibika Jukwaani



Mnenguaji nyota wa band ya Waluguru Og Sinyorita akifanya yake wiki end iliyopita





 

 

Na Mlala Nnje Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

HII Kali Wanenguaji wawiki nyota wa kike wa band ya Maisha Mapya, Sabrina Danger na Mourine V.A.R wamefukuzwa kwenye band hiyo kwa sababu za utoro kazini.

 

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mlala Nnje akiwa kwenye Pilika pilika  za kusaka matukio usiku mnene kwenye kumbi mbali mbali za Starehe alikatiza kwenye shoo ya band ya Waluguru Origanal katikati ya Mji wa Morogoro na kumshuhudia Mnenguaji Sabrina Danger akiuwasha Moto na Waluguru hao.

 

lfahamike hivi karibuni Sabrina aliikacha band hiyo ya Waluguru na kutimkia band Pendwa ya Maisha Mapya, wadau wa Mtandao  Pendwa wa Shekidele watakumbuka siku alipotambulishwa takribani Miezi 2 iliyopita Mlala Nnje aliripoti habari hiyo.

 

Sabrina alivyoshuka Jukwaani Mlala nje alimfuta na kumuliza kulikoni ameikacha band ya Maisha Mapya na kurejea band yake ya zamani ya Maisha Mapya?alicheka kisha akajibu kwa mkato “Nimerejea nyumbani wale Jamaa zako hawanaishu”.

 

Usiku huo huo Mlala Nnje kapiga Gia Pikipiki yake ya Mwendokasi hadi kwenye shoo ya band ya Maisha Mapya maeneo ya Mazindu na kuzungumza na Kiongozi wa band hiyo Joshua Malekela ambapo alipoulizwa juu ya mnenguaji huyo alijibu kwa Jazba.

 

”Tumewafukuza wanenguaji  Sabrina na Mourine kwa sababu ni watoro kazini eti Sabrina akiwa na matatizo Mourine haji kazini wiki inayofuta Mourine akiomba ruhusu, Sabrina naye hajikazini sasa hatuwezi kuwavumilia wanamuziki wa sampuli hiyo wanaoleta utani kwenye kazi”alisema Malekea.

 Mourine V.A.R naye alijiunga na band hiyo hivi karibuni akitokea band ya Afrikan Stars’Twanga Pepeta’ ya Jijini Dar.

Sunday, October 23, 2022

MSIBA WA MCHEZAJI WA SIMBA MCHUNGAJI AWASHUKIA WANAWAKE WANAOTEMBEA NUSU UCHI MTAANI.


 


            Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

AMANI ya Bwana na iwe Juu yenu,nawasalimu tena kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Kwa Majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tunamshukuru tena kwa kuendelea kutupa zawadi ya Uhai na afya njema tukitambua  kuna wenzetu walitamani hayo lakini Mungu amewatwaa na wengine Muda huu wako Mahospitali na Majumbani wakisumbuliwa na Maradhi Mbali mbali wakipigania Uhai wao.

 

 Mtandao huu unamuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema awaponye  na awape kauli thabiti wote waliofariki dunia akiwemo Mpendwa wetu Mchezaji wa zamani wa Reli Moro, Simba na timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ Marehemu Steven Mdachi aliyeiaga dunia Jumapili iliyopita.

 

Akihubiri kwenye lbada ya kumuombea Marehemu Mdachi iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Mtaa wa Reli Estate Kata ya Kichangani Mkoani hapa, Mchungaji Kiongozi wa kanisa Kuu la Anglikana Morogoro Mchungaji Willison Mafunusi aliwaonya watu wenye tabia ya kusahau majukumu yao ya msingi.

 

“Hapa Msibani tuko watu wa dini mbali mbali kuna baadhi ya watu hawaendi kwenye nyumba za lbada kumuomba  Mungu wanategenea kupana Mawaidha,Mahubiri au mafundisho ya Mungu kwenye lbada za Misibani.

 

Hivyo niwe Muwazi  kwenye mahubiri yangu hapa msibani sitafundisha neno la Mungu kwani Marehemu Mdachi faili lake limeshafungwa hata nikihubiri vipi sitaweza kuongeza chochote kwenye faili lake.

 

Sisi tuliokuwa hai ndio wenyenafasi ya kubadili maisha yetu kuna baadhi ya watu hawaendi kwenye nyumba za lbada kumuungamia Mungu wao wako bize na mambo ya dunia wanasubiri kusikia Mawaidha au Mahubiri  yanayotolewa na Viongozi wa dini kwenye lbada za Misibani.

 

Mawaidha hayo au Mahubiri hayo ya Msibani hayatakusaidi chochote naamini Mungu anaweza kukusaidia na kukusamehe makosa yako ukiacha kazi zako ukafunga safari kwenye Kanisani au Msikitini kumuungamia kwa dhati amanini wote tulokuwa hapa hatukuja kwenye ibada tumekuja kwenye msiba”alisema Mchungaji huyo na kuendelea kusema.

 

 “Nitakachowahubiria leo ni lshu ya watu kusahau Majukumu yao na somo hilo linatoka.

Kumbukumbu la Torati 8 -11 “Jihadharini Usije Ukamsahau Bwana Mungu wako,kwa kutozishika amri zake na hukumu zake,na Sheria zake, zinazokuamuru leo.”

 

Somo mmelisikia linatukumbusha kwamba pamoja na ubize wetu wa kutafuta maisha na sterehe za dunia hii lakini tusimsahu Bwana Mungu wetu, tujisisahau kwenda kwenye lbada kanisani na Misikitini tusisubiri mpaka utokee msibani kama hivi  viongozi wa dini waje kutufundisha maneno ya Mungu hapana.

 

Tayari hapa hapa msibani watu wanajisahau mimi naendelea na lbada wao wanazungumza habari za Simba na Yanga, tunasahau sana utakuta mwanamke anajisahau anafanya mambo ya hovyo kama vile sio mke wa mtu hajiheshimu.

 

Tunajisahau sana utakuwa mwanaume anasahu kutimiza majukumu yake nyumbani kama baba wa familia pesa zote anamalizi kwenye anasa  Pombe na uzinzi watoto wake nyumbani wanakufa njaa.

 

Tunatembea mtaani unamuona mwanamke amaevaa nusu uchi tunasema huyu naye amesahau kuvaa nguo anatembea nusu uchi mtaani.

 

Mimi sio mtaalamu sana wa kusikiliza nyimbo lakini ule wimbo wa Msanii Hussein Machozi unaokwenda kwa jina la natamani kuludi Jela unamaana kubwa sana.

 

Ule wimbo ulibeba ujumbe wa mtu aliyekuwa jela siku nyingi alivyotoka Ulaiani na kukutana na mambo ya ajabu ya kiwemo ya kina dada kutembea nusu uchi Mtaani akasema  bora arejea huko huko ndani ili asione uchafu huo, hivyo naomba tusijisahau”alimalizia kusema mchungaji huyo ambapo muda wote watu walikuwa wakishangilia kwa vicheko kama vile hawako msibani ambapo alipohitimisha mahurini yake hayo alipokea zawadi ya makofi mengi kutoka kwa waombelezaji hao wakitamani aendelea kuwapa dozi hiyo nzito.

 

Saturday, October 22, 2022

BEKI ASIMULIA MCHEZAJI MWENZAKE ALIVYOTOROSHWA NA VIONGOZI WA SIMBA WAKIWA KAMBI YA JESHI MORO.


 

      Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Beki kisiki wa zamani wa timu ya Reli ya Morogoro’Kiboko ya Vigogo’ Jonasa Mwaluko amefunguka jinsi Viongozi wa Simba walivyovamia kimafya kambi ya timu hiyo iliyokuwa  Jeshi la  Magereza Kingolwira Manispaa ya Morogoro na kumtorosha Mshambuliaji hatari wa Reli Steven Mdachi.

 

 Akihojiwa na Mtanda huu kwenye Msiba wa Hayati Steven Mdachi aliyefariki Jumapili iliyopita Mkoani hapa na kuzikwa Jumatano nyumbani kwao eneo la Kikuyu Mkoani Dodoma, rafiki Mkubwa wa Marehemu Mdachi Bw Mwaluko alipotakiwa kueleza tukio hilo alifunguka yafuatayo.

 

“Marehemu Mdachi ni rafiki yangu Mkubwa na juzi alivyoanza kuugua alinijulisha hivyo wakati najianda kutoka Dodoma kuja hapa Moro nikapata taarifa zilizolarua moyo wangu kwamba rafiki yangu kipenzi amefariki dunia”alisema Mzee Mwaluko na kuongeza.

 

 “Kuhusu tukio la Simba kuvamia kambi yetu na kumwiba Mdachi ilikuwa Mwaka 78 Reli tuliweka kambi eneo la Jeshi la Magereza Kingolwira  rafiki Mdachi aliniambia anatoroka kambini amefuatwa na wachezaji wa Simba akaitumikie timu hiyo dhidi ya timu ya AS Vita [Association Sportive Vita  Club] yenye Maskani yake Kinshasa nchini Congo.

 

Siku hiyo jioni Mdachi hakuonekana kambini Viongozi wakaniuliza Rafiki yako yuko wapi nikawaficha nikawaambia sijui alipo kwani hakuniaga siku iliyofuta tunamsikia kwenye Matangazo ya Redio Tanzania’RTD’ akiitumikia timu ya Simba kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Vita.

 

 Nakumbuka kabla ya Mdachi kutimkia samba siku 3 nyuma Reli tulicheza mchezo wa Ligi uwanja wa Jamhuri na kikosi kilichocheza mchezo huo mpaka leo nakikumbuka”alisema Mwaluko. Pichani aliyeshika Mic’

Alipotakiwa kukitaja kikosi hicho Mzee Mwaluko alianza kukidadavua kila kusita hata kidogo kama lfuatavyo.

 

“ Nakumbuka Kocha wetu alikuwa Hatiko tukiwa kambini muda mchache kabla ya kuelekea uwanja alitaja kikosi

[1]Hamed Mussa ‘Fujo’

[2]Jonasa Mwaluko[Mimi hapa]

[3]Ally Kidevu’Kaliati’huyu hapa

[4] Muhando Mdeve

[5] Hassan Sengo

[6] Meck Ndomba

[7]Wille Mfundo’Yule pale’

[8]Abdul Bakari

[9] Steven Mdachi huyu amelala kwenye jeneza’

[11] Matata Mdeve.

Friday, October 21, 2022

EXCLUSIVE ENTERVIEW. KAKA WA MAREHEMU AFUNGUKA KUMWIBA MDOGO WAKE KAMBINI NA KUMPELEKA KAMBI YA SIMBA.

Charles Mdachi akifunguka alivyofanya umanya kumchomoa mdogo wake Kambi ya timu ya Reli na Kumpeleka kambi ya timu ya Simba

 

Shabiki namba Moja nchini ambaye mpaka sasa pengo lake halijazibwa Hayati  Yamungu akifanya yake uwanja wa Uhuru Dar kwenye gemu ya Yanga na Reli.

 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kwa Mara ya kwanza  Charles Mdachi ambaye ni Kaka wa Marehemu Steven Mdachi amefunguka A-Z ulivyotumia Umafya yeye na Viongozi wa Simba kuvamia kambi ya timu ya Reli ya Morogoro na kumwiba mdogo wake Steven Mdachi na kumpeleka Kambi ya Simba Jijini Dar ili aitumikie timu hiyo kwenye Mchezo wa kimataifa dhidi ya AC Vita ya Congo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

 

Jana Mtandao huu uriripoti habari ya kifo cha Mpendwa wetu  Steven Mdachi na kwenye habari hiyo tuliahidi kurusha hewani habari mbili moja wapo ikiwa hii ya kaka wa Marehemu kueleza alivyovamia kambi ya Reli na kumchomoa mdogo wake.

lfahamike Mwandishi wa habari hizi alisoma shule ya Msingi Kaloleni iliyopo Mji Mpya jirani kabisa na Maghorofa waliokuwa wakiishia wafanyakazi wa Shirika la  Reli Morogoro,nje ya Shule hiyo ulikuwepo uwanja wa mazoezi wa timu ya Reli.

 

Kwa mazingira hayo toka Mwandishi wa habari hizi anaanza darasa la kwanza mpaka kuhitimu la 7 mapenzi yake yalikuwa kwenye timu hiyo na kamwe hajawahi kuzipenda timu za uridhi za Simba na Yanga.

 

 Kuna kipindi Reli ilicheza michezo ya kirafiki kwenye uwanja huo,Mwandishi huyo alikuwa ni miongoni mwa watoto walioteuliwa kuokota Mipira uwanjani ‘Ballboys.’

 

Baada ya kuwa mtu mzima Mwandishi huyo alikabidhi kadi ya Uwanachama wa timu hiyo  na  Mwenyekiti Mzee Sumary.

 

Kama hiyo haitoshi  Uongozi wa Reli uliteuwa watu wawili kuzunguka na timu mikoani kwenye michezo ya ligi kuu ambapo Mpiga Picha wa Mtandao huu aliteuliwa kuwa Mpiga Picha mkuu wa timu na Shabiki namba moja nchini Tanzania hayati Yamungu aliteuliwa kuwa mhamasishaji Mkuu wa timu.

 

Kuna siku tukiwa safarini tukielekea mikoani ikazungumzwa stori  ya Simba kuvamia kambi ya Reli na kumchukua kimafya Steven Mdachi na kumpeleka kambi ya Simba.

 

Stori nyingine ilikuwa Simba hao hao kuvamia kambi ya Reli iliyokuwa Chuo Cha VETA Morogoro na kumvyakua Kimafya Clement Bazo ambaye baada ya kuitumikia Simba kwa miaka kadhaa alireja Moro na kujiunga na timu ya Polisi Moro, baadae Bazo kapata ajira kwenye jeshi hilo kwa sasa ni Askari Polisi wa kituo Kikuu cha Polisi Morogoro.  .

 

Hivyo juzi kwenye Msiba wa Steven Mdachi Mwandishi wa Mtandao huu alijikita kutafuta undani wa tukio hilo ambapo kwenye dodosa ndosa alifanikiwa kuwapata wahusika walioshiriki kwenye tukio hilo ambao ni Kaka wa Marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charles Mdachi na rafiki Mkubwa wa Marehemu Jonasan Mwaluko.

   MSIKIE KAKA WA MAREHEMU.

“Ni kweli tukio hilo limetokea Mwaka 1978  Kwa siku zote hizo mpaka sasa mimi na familia yangu tunaishi Dar, siku ya tukio uongozi wa Simba nakumbuka wakati huo mwenykiti alikuwa Johakim Kimwaga walikuja kwangu kuniomba nifanye linalowezekana nije Morogoro kumchukua Mdogo wangu Steven  nimpeleke timu ya Simba ambao walikuwa na mchezo mgumu wa kimataifa dhidi ya AC ViTA ya Congo.

 

 Kama unavyojua wakati huo Mdogo wangu alikuwa mshambuliaji hatari aliifungia Reli mabao kila alipokutana na timu pinzani zikiwemo Simba na Yanga.kiasi cha timu hiyo kupewa jina la Kiboko ya Vigogo.

 

 Nikakubali ombi la Simba nikaingia kwenye gari yao ndogo aina ya Pijo tukaja Kambi ya Reli Morogoro ilikuwa Magereza Kingolwira nakumbuka wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alikuwa mama yetu Anna Abdallah.

 

 Nilipofika jirani na Kambi nikampigia simu Mdogo wangu nikamueleza kuna matatizo ya kifamilia hivyo atokea nje ya kambi tuzungumze akaja fasta.

 

 Viongozi wa Simba waliokuna na donge nono kwenye begi wakamuonyesha na kumuomba akawasaidi kwenye mchezo huo wa kimataifa, kwa kuniheshimi mimi Mdogo wangu kakubali maombi yetu hivyo hakuludi tena kambini kuaga hata begi hakuchukua kaingia kwenye gari tukaanza safari ya Dar.

 

 Dereva kambikiza gari tulivyofika Mdaula tukapata ajari gari limeingia kwenye Mtalo hakuna aliyeumia tukatafuta Fusso likalivuta tukaendelea na safari.

 

Tunamshukuru Mungu tukafika Dar moja kwa moja tukaelekea nyumbani kwa mwenyekiti wa Simba  Kunduchi tukamueleza  kazi aliotutuma tumeikamilisha na mchezo huyo hapa, akamchukua na kumpekeka kambi ya Simba ambapo siku iliyofuata mdogo wangu alicheza vizuri sana mechi hiyo ingawa Simba alifungwa bao 1-0”alisema Charles Mdachi.

 

 Baadae tutarusha hewani habari ya rafiki wa marehemu Jonasa Mwaluko ambaye naye alifahamu A-Z Picha hilo la kiwashiri lililochezwa na Stelling Charles Mdachi na yeye kuwaficha Viongozi wake wa Reli kwa lengo la kumlinda rafiki yake Steve Mdachi, hivyo endelea kuwajirani na mtandao huu muda wote.

                

                

 

 

Thursday, October 20, 2022

WACHEZAJI WA SIMBA NA YANGA WAKIONGOZWA NA ZAMONI MOGELLA WAMESHIRIKI MSIBA WA MCHEZAJI MWENZAO STEVEN MDACH

Fred Mdachi ambaye ni Mtoto wa kwanza wa Marehgemu Mdachi akiongoza mamia ya wananachi kuingia mwili wa baba yake nyumbani kwao baada ya kutoka Mochwa
Mchezaji wa zamani wa Reli Julius Ngawambala akiongoza wenzake kubeba jeneza lenye Mwili wa Steven Mdachi
....Jeneza hilo limewasili nyumbani kwa Marehemu
Marehemu Mdachi enzi za Uhai wake
Umati wawatu walioshiriki msiba huo
Beki wa zamani wa Reli Mohamed Mtono[kushoto] akiweka mambo sawa na Seleman Kido

Wachezaji nyota wa zamani kutoka kulia aliyevaa miwani ni mchezaji wa Simba Zamaoyon Mogelle'Golden Boy' Jonasan Mwaluko[Reli]Ally Jangalu' mchezaji wa zamani wa Reli, Pan na Coastal Union' Ally Kidevu [Reli] Mwenye flana ya Mistari ni Kaka wa Marehemu Charles MdachiSeleman Kidogo[Meneja wa timu ya Reli aalaiyeshika Mikoni ni Dotot Mokili[Yanga] na wamwishi kushoto ni Hamis Malifedha Reli

Doto Mokili kushoto akiteta jambo na Jonasa Mwaluko

Wachezaji wa zamani wa Reli ya Moro kutoka Kulia ni Peter Mjata[Kati]Thabiti Mgalula na Kushoto ni Peter Lemmy huyo alikuw aMuumbe wa kamati ya Utendajiw a timu ya Reli.

Picha no 2 Hussein Ngurungu[kulia] akiteta Jambo ba Bakafu Fungo ambaye ni Mechi Kamishiwa wa michuano ya Ligi Kuu na Mchezji wa Moro Vetera

 

Fundi wa Mpira Ally Bushiri ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Morogoro Veterani

 Wacheaji wa zamani wa Reli Juma salumu Msawila kushoto akipozi mbele ya Kamera na zMtandao huu na Julius Ngawambala

Wachezaji nyota wa zamanai wa Reli Moro kutoka Kulia ni Beki Yohana Semkiya. Hamisi Machupa, Juma Salum Msawila, Hamis Ramadhan Kidingile huyu ni baba Mazazi wa beki wa timu ya Dodoma Jijini Hassa Ramadhan Kessy, Julius Kawambala, Peter Mjana na Kipa wa zamani wa Sandalend[[ kwa sasa Simba] Mlapakolo na wa mwisho kushoto ni Ally Bushiri mchezaji nyota wa zamani wa Pamba ya Mwanza.

Mafundi wa zamani wa Reli Kiboko wa Vigogo kutoka Kushoto ni beki kisiki Salum Pembe. Willy Mfundo[mwenye kapeso Kipa Mohamed Mtenda na wamiwsho kulia ni Salum Dossa mchezaji wa mzani wa Jenolotaya ya Arusha

Mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa zamni nchini UMSOTA Tanzania Husseina Ngurungu akizungumza kwa niaba ya chama hicho juu ya kifo cha Katibu Mkuu wa UMSOTA
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Meya wa Mji huo akitoa salam kwa niaba ya chama hicho
Diwani wa Kaya Mwembesongo akizungumza kwenye Msiba huo
Diwani wa Kaya Kichangani akitoa salama za kata hiyo
Rafiki mkubwa wa Marehmu Mrisho akizungumza huku akitokw ana Machozi kw auchungu
                       Seleman Kido akizungumza
Mwanasiasa Maarrufu mkoa wa Morogoro Abed Mlapako akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kufanya hivyo
Rafiki Mkubwa  wa Marehemu Jonasan Mwaluko aliyefunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kuja kumzika rafiki yake akizungumza kabla ya safari ya kuelekea Dodoma kuanza
Seleman Kido akiteta jambo na Mtoto wa Marehemu
Viongozi wa dini wakiwa pamoja na Mstahiki Meya
              Sister akimfariji Mjane wa Marehemu
...Askofu Mstaafu wa kanisa la Anglikana Jimbo la Morogoro Askofu Mgeni akizungumza kwenye lbada hiyo
Sheke wa wa Msikiti wa Mji Mpya Shehe Kassimu akifuatilia kwa lmakini lbada hiyo
Mchungaji Kiongozoi wa kanisa kuu la Anglikana Morogoro akihubiri kwenye lbada hiyo
Msemaji wa familia ambaye pia ni kaka wa Marehemu Charles Mdachi akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu
Mjane wa Marehemu akiwa na hudhuni kubwa ya kuondokewa na Mpendwa wake
Diwani wa Kaya Kichangani  akimuaga Mpiga kula wake
                    Shaban Chillo akimuaga jirani yake
Mchezaji wa zamani wa Reli Wille Mfundo akimuga Mdachi

Mchezaji wa zamana wa Re.li Ally Jangalu'Mwananguuuu' akimuaga mchezaji wmenzake
Mwanasheria Petet Kimath anaye akitoa heshima zake za mwisho
Fred Mdachi akisoma wasifu wa Mpendwa baba yake
Mjane wa Mareheme Bi Victoria Mdachi akiangua kilia wakati Mwnaye akisoma wasimu wa Mpendwa baba yake
Jeneza likiingizwe kwenye gari yatari kwa safari ya Dodoma
Coaster Mayai wa Bakari Maarufu Maga akiwa yatari kwa safari
Beki wa Kulia wa zamani wa Reli  Yohana Semkia akimuaga mchezaji mwenzake

 Mstahiki Meya Pascal Kihanga[Kulia] akimpa Pole Mtoto wa kwanza wa Marehemu Fred Vteven Mdach


          Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Wachezaji nyota wa zamani wa timu mbali mbali nchini zikiwemo Simba na Yanga wakiongozwa na Mkongwe Zamani Mogella’Golden Boy’ juzi wameshiriki kwenye Msiba wa mchezaji mwenzao wa zamani Marehemu Steven Mdachi alifariki dunia jumapili iliyopita.

 

Hayati Mdachi aliyewahi kuzitumikia timu za CDA ya Dodoma, Reli ya Morogoro,Simba na timu ya taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ alifariki dunia jumapili majira ya saa 7 mchana kwenye hospital ya rufaa ya Mkoani wa Morogoro.

 

Juzi Jumanne ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Kichangani Mtaa wa Reli Estate eneo la Kota za Reli Jirani na Kalakala Kuu ya Shirika la Reli Tanzania ikiongozwa na Mchugaji Kiongozi wa kanisa Kuu la Aglikana Morogoro Mch. Willison Mafunusi.

 

Baada ya lbada hiyo Mwili wa Marehemu uliingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya  kuelekea nyumbani kwao kijiji cha Kikuyu  kilichopo kando kando ya barabara ya lringa Mkoani Dodoma ambapo jana jumatano alipunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele.

 

 Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Msemaji wa familia  Charles Mdachi ambaye ni Kaka wa Marehemu alisema.

 

 “ Jumapili majira ya asubuhi mdogo wangu alilalamika kusumbuliwa na shinikizo la damu’Presha ya kushuka.’

 

Akapelekwa hospital ya Mkoa madaktari walipomcheki walibaini ana Malaria 7 na Presha ya kushuka wakati wakiendelea na matibabu majira ya saa 7 mchana siku hiyo hiyo ya Jumapili mpendwa wetu alifariki dunia”alimalizia kusema  na kuangua kilio ambapo Mwandishi wa Mtandao huu akaradhimika kubeba jukumu la kumbembeleza.

 

Enzi za uhai wake Marehemu alishika nyadhifa mbali mbali kwenye Jamii hadi umauti unamkuta Hayati Mdachi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha wachezaji  Nyota wa zamani hapa Tanzania  wenye makao yake Makuu jijini Dar unajulikana kwa jina la [UMSOTA Tananzia].

 

 Marehemu Mdachi pia alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Uchaguzi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro.na Kiongozi wa timu ya Reli Family Veterani inayafanya mazoezi yake kila siku uwanja wa Shule ya Msingi Mwere.

 

Kama hiyo haitoshi Hayati Mdachi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mtaa wa Reli Estate na Mshauri wa Kanisa la Anglikana Mtaa wa Area Five Kichangani.

 

Baadhi ya watu mashuhuri walioshuhudiwa na Mwandishi wa habari hizi kwenye Msibani huo ni pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro  Mh Pascal Kihanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro.

 

Diwani wa Kata ya Mwembesongo Mh Ally Nyau,Diwani wa kata ya Kichangani Mh Gilbert Mtafani na Mwanasiasa Maarufu Mkoani wa Morogoro Abed Mlapakolo aliyewahi kumbea Ubunge Jimbo la Morogoro kwa leseni ya Chama cha CUF kwa awamu mbili ambapo awamu zote mbili kwenye boksi lake kula hazikutosha.

 

Wengine ni Askofu Mstaafu wa Anglikana Jimbo la Morogoro Baba Askofu Mageni, Shehe wa Msikiti wa Mji Mpya Sheke Kassimu na Mwanasheria Maarufu Mkoa wa Morogoro Peter Kimath ambaye  Kitaaluma ni Mwandishi wa habari na Mwanachama wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro.

 

 Baadhi ya wachezaji wa zamani walioshuhudiwa na Mtandao huu kwenye Msiba huo ni pamoja na Amri lbrahim na Zamayoni Mogelle[Simba] Dotto Mokili [Yanga] Hussein Ngurungu[Pan Afrika] na Ally Bushiri Pamba ya Mwanza] na kundi kubwa la wachezaji nyota wa mzani wa Reli walizifunga Simba na Yanga Popote walipokutana nazo iwe Moro au kwao Dar walizipiga kama Ngoma na kupachikwa jina la Reli‘Kiboko ya Vigogo’.

 

Marehemu ameacha Mjane Mmoja Bi, Victoria Mdachi na watoto wawili Fred na Frida.

 

Katika Msiba huo Mwandishi wa Mtandao huu amenasa stori kubwa 2 moja ni kaka wa Marehemu kafunguka jinsi alivyofanya umanya mwaka 78 kuvamia kambi ya timu ya Reli akiwa na mashushu wa Simba  wakamwiba Mdogo wake Hayati Mdachi na kumpeleka Simba akacheza mchezo wa Kimataifa dhidi ya AC Vita ya Congo.

Stori ya Pili ambayo itaruka kwenye ujumbe wa neno la Mungu Jumapili ijayo ni sehemu ya Mahubiri Mazuri ya Mchungaji Mafunusi Somo hilo likibeba ujumbe wa kusahau akiwashukia wanawake wanaotembea mitaani nusu uchi akikadhia hilo kwa kutaja  wimbo wa  Msanii Hussein Machozi.

Kwa habari hizo na nyingine moto moto endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 

 

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...