Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
AMANI ya Bwana na iwe Juu yenu,nawasalimu tena kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa Majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tunamshukuru tena kwa kuendelea kutupa zawadi ya Uhai na afya njema tukitambua kuna wenzetu walitamani hayo lakini Mungu amewatwaa na wengine Muda huu wako Mahospitali na Majumbani wakisumbuliwa na Maradhi Mbali mbali wakipigania Uhai wao.
Mtandao huu unamuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema awaponye na awape kauli thabiti wote waliofariki dunia akiwemo Mpendwa wetu Mchezaji wa zamani wa Reli Moro, Simba na timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ Marehemu Steven Mdachi aliyeiaga dunia Jumapili iliyopita.
Akihubiri kwenye lbada ya kumuombea Marehemu Mdachi iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Mtaa wa Reli Estate Kata ya Kichangani Mkoani hapa, Mchungaji Kiongozi wa kanisa Kuu la Anglikana Morogoro Mchungaji Willison Mafunusi aliwaonya watu wenye tabia ya kusahau majukumu yao ya msingi.
“Hapa Msibani tuko watu wa dini mbali mbali kuna baadhi ya watu hawaendi kwenye nyumba za lbada kumuomba Mungu wanategenea kupana Mawaidha,Mahubiri au mafundisho ya Mungu kwenye lbada za Misibani.
Hivyo niwe Muwazi kwenye mahubiri yangu hapa msibani sitafundisha neno la Mungu kwani Marehemu Mdachi faili lake limeshafungwa hata nikihubiri vipi sitaweza kuongeza chochote kwenye faili lake.
Sisi tuliokuwa hai ndio wenyenafasi ya kubadili maisha yetu kuna baadhi ya watu hawaendi kwenye nyumba za lbada kumuungamia Mungu wao wako bize na mambo ya dunia wanasubiri kusikia Mawaidha au Mahubiri yanayotolewa na Viongozi wa dini kwenye lbada za Misibani.
Mawaidha hayo au Mahubiri hayo ya Msibani hayatakusaidi chochote naamini Mungu anaweza kukusaidia na kukusamehe makosa yako ukiacha kazi zako ukafunga safari kwenye Kanisani au Msikitini kumuungamia kwa dhati amanini wote tulokuwa hapa hatukuja kwenye ibada tumekuja kwenye msiba”alisema Mchungaji huyo na kuendelea kusema.
“Nitakachowahubiria leo ni lshu ya watu kusahau Majukumu yao na somo hilo linatoka.
Kumbukumbu la Torati 8 -11 “Jihadharini Usije Ukamsahau Bwana Mungu wako,kwa kutozishika amri zake na hukumu zake,na Sheria zake, zinazokuamuru leo.”
Somo mmelisikia linatukumbusha kwamba pamoja na ubize wetu wa kutafuta maisha na sterehe za dunia hii lakini tusimsahu Bwana Mungu wetu, tujisisahau kwenda kwenye lbada kanisani na Misikitini tusisubiri mpaka utokee msibani kama hivi viongozi wa dini waje kutufundisha maneno ya Mungu hapana.
Tayari hapa hapa msibani watu wanajisahau mimi naendelea na lbada wao wanazungumza habari za Simba na Yanga, tunasahau sana utakuta mwanamke anajisahau anafanya mambo ya hovyo kama vile sio mke wa mtu hajiheshimu.
Tunajisahau sana utakuwa mwanaume anasahu kutimiza majukumu yake nyumbani kama baba wa familia pesa zote anamalizi kwenye anasa Pombe na uzinzi watoto wake nyumbani wanakufa njaa.
Tunatembea mtaani unamuona mwanamke amaevaa nusu uchi tunasema huyu naye amesahau kuvaa nguo anatembea nusu uchi mtaani.
Mimi sio mtaalamu sana wa kusikiliza nyimbo lakini ule wimbo wa Msanii Hussein Machozi unaokwenda kwa jina la natamani kuludi Jela unamaana kubwa sana.
Ule wimbo ulibeba ujumbe wa mtu aliyekuwa jela siku nyingi alivyotoka Ulaiani na kukutana na mambo ya ajabu ya kiwemo ya kina dada kutembea nusu uchi Mtaani akasema bora arejea huko huko ndani ili asione uchafu huo, hivyo naomba tusijisahau”alimalizia kusema mchungaji huyo ambapo muda wote watu walikuwa wakishangilia kwa vicheko kama vile hawako msibani ambapo alipohitimisha mahurini yake hayo alipokea zawadi ya makofi mengi kutoka kwa waombelezaji hao wakitamani aendelea kuwapa dozi hiyo nzito.
No comments:
Post a Comment