Shabiki namba Moja nchini ambaye mpaka sasa pengo lake halijazibwa Hayati Yamungu akifanya yake uwanja wa Uhuru Dar kwenye gemu ya Yanga na Reli.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Kwa Mara ya kwanza Charles Mdachi ambaye ni Kaka wa Marehemu Steven Mdachi amefunguka A-Z ulivyotumia Umafya yeye na Viongozi wa Simba kuvamia kambi ya timu ya Reli ya Morogoro na kumwiba mdogo wake Steven Mdachi na kumpeleka Kambi ya Simba Jijini Dar ili aitumikie timu hiyo kwenye Mchezo wa kimataifa dhidi ya AC Vita ya Congo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Jana Mtandao huu uriripoti habari ya kifo cha Mpendwa wetu Steven Mdachi na kwenye habari hiyo tuliahidi kurusha hewani habari mbili moja wapo ikiwa hii ya kaka wa Marehemu kueleza alivyovamia kambi ya Reli na kumchomoa mdogo wake.
lfahamike Mwandishi wa habari hizi alisoma shule ya Msingi Kaloleni iliyopo Mji Mpya jirani kabisa na Maghorofa waliokuwa wakiishia wafanyakazi wa Shirika la Reli Morogoro,nje ya Shule hiyo ulikuwepo uwanja wa mazoezi wa timu ya Reli.
Kwa mazingira hayo toka Mwandishi wa habari hizi anaanza darasa la kwanza mpaka kuhitimu la 7 mapenzi yake yalikuwa kwenye timu hiyo na kamwe hajawahi kuzipenda timu za uridhi za Simba na Yanga.
Kuna kipindi Reli ilicheza michezo ya kirafiki kwenye uwanja huo,Mwandishi huyo alikuwa ni miongoni mwa watoto walioteuliwa kuokota Mipira uwanjani ‘Ballboys.’
Baada ya kuwa mtu mzima Mwandishi huyo alikabidhi kadi ya Uwanachama wa timu hiyo na Mwenyekiti Mzee Sumary.
Kama hiyo haitoshi Uongozi wa Reli uliteuwa watu wawili kuzunguka na timu mikoani kwenye michezo ya ligi kuu ambapo Mpiga Picha wa Mtandao huu aliteuliwa kuwa Mpiga Picha mkuu wa timu na Shabiki namba moja nchini Tanzania hayati Yamungu aliteuliwa kuwa mhamasishaji Mkuu wa timu.
Kuna siku tukiwa safarini tukielekea mikoani ikazungumzwa stori ya Simba kuvamia kambi ya Reli na kumchukua kimafya Steven Mdachi na kumpeleka kambi ya Simba.
Stori nyingine ilikuwa Simba hao hao kuvamia kambi ya Reli iliyokuwa Chuo Cha VETA Morogoro na kumvyakua Kimafya Clement Bazo ambaye baada ya kuitumikia Simba kwa miaka kadhaa alireja Moro na kujiunga na timu ya Polisi Moro, baadae Bazo kapata ajira kwenye jeshi hilo kwa sasa ni Askari Polisi wa kituo Kikuu cha Polisi Morogoro. .
Hivyo juzi kwenye Msiba wa Steven Mdachi Mwandishi wa Mtandao huu alijikita kutafuta undani wa tukio hilo ambapo kwenye dodosa ndosa alifanikiwa kuwapata wahusika walioshiriki kwenye tukio hilo ambao ni Kaka wa Marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charles Mdachi na rafiki Mkubwa wa Marehemu Jonasan Mwaluko.
MSIKIE KAKA WA MAREHEMU.
“Ni kweli tukio hilo limetokea Mwaka 1978 Kwa siku zote hizo mpaka sasa mimi na familia yangu tunaishi Dar, siku ya tukio uongozi wa Simba nakumbuka wakati huo mwenykiti alikuwa Johakim Kimwaga walikuja kwangu kuniomba nifanye linalowezekana nije Morogoro kumchukua Mdogo wangu Steven nimpeleke timu ya Simba ambao walikuwa na mchezo mgumu wa kimataifa dhidi ya AC ViTA ya Congo.
Kama unavyojua wakati huo Mdogo wangu alikuwa mshambuliaji hatari aliifungia Reli mabao kila alipokutana na timu pinzani zikiwemo Simba na Yanga.kiasi cha timu hiyo kupewa jina la Kiboko ya Vigogo.
Nikakubali ombi la Simba nikaingia kwenye gari yao ndogo aina ya Pijo tukaja Kambi ya Reli Morogoro ilikuwa Magereza Kingolwira nakumbuka wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alikuwa mama yetu Anna Abdallah.
Nilipofika jirani na Kambi nikampigia simu Mdogo wangu nikamueleza kuna matatizo ya kifamilia hivyo atokea nje ya kambi tuzungumze akaja fasta.
Viongozi wa Simba waliokuna na donge nono kwenye begi wakamuonyesha na kumuomba akawasaidi kwenye mchezo huo wa kimataifa, kwa kuniheshimi mimi Mdogo wangu kakubali maombi yetu hivyo hakuludi tena kambini kuaga hata begi hakuchukua kaingia kwenye gari tukaanza safari ya Dar.
Dereva kambikiza gari tulivyofika Mdaula tukapata ajari gari limeingia kwenye Mtalo hakuna aliyeumia tukatafuta Fusso likalivuta tukaendelea na safari.
Tunamshukuru Mungu tukafika Dar moja kwa moja tukaelekea nyumbani kwa mwenyekiti wa Simba Kunduchi tukamueleza kazi aliotutuma tumeikamilisha na mchezo huyo hapa, akamchukua na kumpekeka kambi ya Simba ambapo siku iliyofuata mdogo wangu alicheza vizuri sana mechi hiyo ingawa Simba alifungwa bao 1-0”alisema Charles Mdachi.
Baadae tutarusha hewani habari ya rafiki wa marehemu Jonasa Mwaluko ambaye naye alifahamu A-Z Picha hilo la kiwashiri lililochezwa na Stelling Charles Mdachi na yeye kuwaficha Viongozi wake wa Reli kwa lengo la kumlinda rafiki yake Steve Mdachi, hivyo endelea kuwajirani na mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment