Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Beki kisiki wa zamani wa timu ya Reli ya Morogoro’Kiboko ya Vigogo’ Jonasa Mwaluko amefunguka jinsi Viongozi wa Simba walivyovamia kimafya kambi ya timu hiyo iliyokuwa Jeshi la Magereza Kingolwira Manispaa ya Morogoro na kumtorosha Mshambuliaji hatari wa Reli Steven Mdachi.
Akihojiwa na Mtanda huu kwenye Msiba wa Hayati Steven Mdachi aliyefariki Jumapili iliyopita Mkoani hapa na kuzikwa Jumatano nyumbani kwao eneo la Kikuyu Mkoani Dodoma, rafiki Mkubwa wa Marehemu Mdachi Bw Mwaluko alipotakiwa kueleza tukio hilo alifunguka yafuatayo.
“Marehemu Mdachi ni rafiki yangu Mkubwa na juzi alivyoanza kuugua alinijulisha hivyo wakati najianda kutoka Dodoma kuja hapa Moro nikapata taarifa zilizolarua moyo wangu kwamba rafiki yangu kipenzi amefariki dunia”alisema Mzee Mwaluko na kuongeza.
“Kuhusu tukio la Simba kuvamia kambi yetu na kumwiba Mdachi ilikuwa Mwaka 78 Reli tuliweka kambi eneo la Jeshi la Magereza Kingolwira rafiki Mdachi aliniambia anatoroka kambini amefuatwa na wachezaji wa Simba akaitumikie timu hiyo dhidi ya timu ya AS Vita [Association Sportive Vita Club] yenye Maskani yake Kinshasa nchini Congo.
Siku hiyo jioni Mdachi hakuonekana kambini Viongozi wakaniuliza Rafiki yako yuko wapi nikawaficha nikawaambia sijui alipo kwani hakuniaga siku iliyofuta tunamsikia kwenye Matangazo ya Redio Tanzania’RTD’ akiitumikia timu ya Simba kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Vita.
Nakumbuka kabla ya Mdachi kutimkia samba siku 3 nyuma Reli tulicheza mchezo wa Ligi uwanja wa Jamhuri na kikosi kilichocheza mchezo huo mpaka leo nakikumbuka”alisema Mwaluko. Pichani aliyeshika Mic’
Alipotakiwa kukitaja kikosi hicho Mzee Mwaluko alianza kukidadavua kila kusita hata kidogo kama lfuatavyo.
“ Nakumbuka Kocha wetu alikuwa Hatiko tukiwa kambini muda mchache kabla ya kuelekea uwanja alitaja kikosi
[1]Hamed Mussa ‘Fujo’
[2]Jonasa Mwaluko[Mimi hapa]
[3]Ally Kidevu’Kaliati’huyu hapa
[4] Muhando Mdeve
[5] Hassan Sengo
[6] Meck Ndomba
[7]Wille Mfundo’Yule pale’
[8]Abdul Bakari
[9] Steven Mdachi huyu amelala kwenye jeneza’
[11] Matata Mdeve.
No comments:
Post a Comment