Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MTANGAZAJI Maarufu wa Kituo Maarufu cha Luninga Afrika Mashariki na Kati Cha lndependent Television Maarufu I.T.V ‘Super Bland’,Juma kapalatu amevunjika Mguu mmoja baada ya Pikipiki aliyokuwa akiendesha akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi jijini Dar es salaam kupata ajari.
Baada ya kupata ajari hiyo alipata matibabu kwenye hospital mbali mbali za jijini Dar kabla ya hivi karibuni kuja mkoani hapa kwenye kituo cha Tiba asili cha Dr Kisome kilichopo Kihonda Mkoani hapa.
Kituo hicho kinachoongozwa na Dr bingwa wa Mifupa nchini Dr Kisome aliyewahi kupiga kazi hospital ya Tumbi Kibana kimejizolea umaarufu mkubwa nchini ambapo baadhi ya wachezaji nyota wa timu kubwa zikiwemo Simba na Yanga wanapovunjika Miguu hutibiwa kwenye kituo hicho na Dr Kisome ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mafisa kwa leseni ya CCM.
lfahamikea Kapalatu kabla ya kutimikia ITV na Radio One alikuwa akipiga kazi Abood Media inayobeba Luninga ya Abood Televison’ATV’ na Abood Radio Abood Fm, Kapalatu pia ni Mwanachama hai wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro.
Hivyo juzi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya alifunga safari hadi kwenye kituo hicho na kumjulia hali Mwanachama wake kama wanavyoonekana wakiwa kwenye Picha ya pamoja nnje ya kituo hicho Mkilanya Kulia akimpa Pole Kapalatu.
Leo asubuhi Mwandishi wa habari hizi alimpiga simu Kapalatu kwa lengo la kumjulia hali sambamba na kumhoji juu ya tukio hilo ambapo alipotakiwa kueleza ajari hiyo alisema.
“Miezi miwili iliyopita nikiwa kwenye Pikipiki yangu kwenye majukumu yangu ya kikazi nilipata ajari Buguruni eneo la makutano ya barabara nikavunjika mguu mmoja nilipata matibabu kwenye hospital kadhaa jijini Dar lakini baadae nikaona nije hapa nyumbani Morogoro kwenye Kituo cha Dr Kisome ambapo nashukuru baada ya kufika hapa na kupata matibabu naendelea vizuri sana tofauti na awari kabla sijafika hapa”alisema Kapalatu.
Mtandao huu unamuomba Mungu azidi kumponya ndugu yetu Kapalatu ili arejea kwenye majukumu yake ya mbali mbali yakiwemo hayo ya utangazaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya alipohojiwa na Mtandao huu alisema.
” Ni kweli Shekidele juzi nilikwenda kumjulia hali mwenzetu Kapalatu namshukuru Mungu kwa sasa anaendelea Vizuri baada ya kupata tiba pale kwa Dr Kisome” alisema Mkilanya
Baadhi ya watangazaji wengine Maarufu waliotokea Abood Media na kutimkia Vyombo mbali mbali vya habari vya Jijini Dar ni pamoja na Tumie Omar Radio One, Salum Mkambara Chanel Ten, Henry MabumoTBC’na Juma Kapalatu ITV.
No comments:
Post a Comment