Mchezaji wa zamani wa Reli Julius Ngawambala akiongoza wenzake kubeba jeneza lenye Mwili wa Steven Mdachi
....Jeneza hilo limewasili nyumbani kwa Marehemu
Marehemu Mdachi enzi za Uhai wake
Umati wawatu walioshiriki msiba huo
Beki wa zamani wa Reli Mohamed Mtono[kushoto] akiweka mambo sawa na Seleman Kido
Wachezaji nyota wa zamani kutoka kulia aliyevaa miwani ni mchezaji wa Simba Zamaoyon Mogelle'Golden Boy' Jonasan Mwaluko[Reli]Ally Jangalu' mchezaji wa zamani wa Reli, Pan na Coastal Union' Ally Kidevu [Reli] Mwenye flana ya Mistari ni Kaka wa Marehemu Charles MdachiSeleman Kidogo[Meneja wa timu ya Reli aalaiyeshika Mikoni ni Dotot Mokili[Yanga] na wamwishi kushoto ni Hamis Malifedha Reli
Doto Mokili kushoto akiteta jambo na Jonasa MwalukoWachezaji wa zamani wa Reli ya Moro kutoka Kulia ni Peter Mjata[Kati]Thabiti Mgalula na Kushoto ni Peter Lemmy huyo alikuw aMuumbe wa kamati ya Utendajiw a timu ya Reli.
Picha no 2 Hussein Ngurungu[kulia] akiteta Jambo ba Bakafu Fungo ambaye ni Mechi Kamishiwa wa michuano ya Ligi Kuu na Mchezji wa Moro Vetera
Fundi wa Mpira Ally Bushiri ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Morogoro Veterani
Wacheaji wa zamani wa Reli Juma salumu Msawila kushoto akipozi mbele ya Kamera na zMtandao huu na Julius Ngawambala
Wachezaji nyota wa zamanai wa Reli Moro kutoka Kulia ni Beki Yohana Semkiya. Hamisi Machupa, Juma Salum Msawila, Hamis Ramadhan Kidingile huyu ni baba Mazazi wa beki wa timu ya Dodoma Jijini Hassa Ramadhan Kessy, Julius Kawambala, Peter Mjana na Kipa wa zamani wa Sandalend[[ kwa sasa Simba] Mlapakolo na wa mwisho kushoto ni Ally Bushiri mchezaji nyota wa zamani wa Pamba ya Mwanza.
Mafundi wa zamani wa Reli Kiboko wa Vigogo kutoka Kushoto ni beki kisiki Salum Pembe. Willy Mfundo[mwenye kapeso Kipa Mohamed Mtenda na wamiwsho kulia ni Salum Dossa mchezaji wa mzani wa Jenolotaya ya Arusha
Mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa zamni nchini UMSOTA Tanzania Husseina Ngurungu akizungumza kwa niaba ya chama hicho juu ya kifo cha Katibu Mkuu wa UMSOTAMwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Meya wa Mji huo akitoa salam kwa niaba ya chama hicho
Diwani wa Kaya Mwembesongo akizungumza kwenye Msiba huo
Diwani wa Kaya Kichangani akitoa salama za kata hiyo
Rafiki mkubwa wa Marehmu Mrisho akizungumza huku akitokw ana Machozi kw auchungu
Seleman Kido akizungumza
Mwanasiasa Maarrufu mkoa wa Morogoro Abed Mlapako akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kufanya hivyo
Rafiki Mkubwa wa Marehemu Jonasan Mwaluko aliyefunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kuja kumzika rafiki yake akizungumza kabla ya safari ya kuelekea Dodoma kuanza
Seleman Kido akiteta jambo na Mtoto wa Marehemu
Viongozi wa dini wakiwa pamoja na Mstahiki Meya
Sister akimfariji Mjane wa Marehemu
...Askofu Mstaafu wa kanisa la Anglikana Jimbo la Morogoro Askofu Mgeni akizungumza kwenye lbada hiyo
Sheke wa wa Msikiti wa Mji Mpya Shehe Kassimu akifuatilia kwa lmakini lbada hiyo
Mchungaji Kiongozoi wa kanisa kuu la Anglikana Morogoro akihubiri kwenye lbada hiyo
Msemaji wa familia ambaye pia ni kaka wa Marehemu Charles Mdachi akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu
Mjane wa Marehemu akiwa na hudhuni kubwa ya kuondokewa na Mpendwa wake
Diwani wa Kaya Kichangani akimuaga Mpiga kula wake
Shaban Chillo akimuaga jirani yake
Mchezaji wa zamani wa Reli Wille Mfundo akimuga Mdachi
Mchezaji wa zamana wa Re.li Ally Jangalu'Mwananguuuu' akimuaga mchezaji wmenzake
Mwanasheria Petet Kimath anaye akitoa heshima zake za mwisho
Mjane wa Mareheme Bi Victoria Mdachi akiangua kilia wakati Mwnaye akisoma wasimu wa Mpendwa baba yake
Jeneza likiingizwe kwenye gari yatari kwa safari ya Dodoma
Coaster Mayai wa Bakari Maarufu Maga akiwa yatari kwa safari
Mstahiki Meya Pascal Kihanga[Kulia] akimpa Pole Mtoto wa kwanza wa Marehemu Fred Vteven Mdach
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Wachezaji nyota wa zamani wa timu mbali mbali nchini zikiwemo Simba na Yanga wakiongozwa na Mkongwe Zamani Mogella’Golden Boy’ juzi wameshiriki kwenye Msiba wa mchezaji mwenzao wa zamani Marehemu Steven Mdachi alifariki dunia jumapili iliyopita.
Hayati Mdachi aliyewahi kuzitumikia timu za CDA ya Dodoma, Reli ya Morogoro,Simba na timu ya taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ alifariki dunia jumapili majira ya saa 7 mchana kwenye hospital ya rufaa ya Mkoani wa Morogoro.
Juzi Jumanne ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Kichangani Mtaa wa Reli Estate eneo la Kota za Reli Jirani na Kalakala Kuu ya Shirika la Reli Tanzania ikiongozwa na Mchugaji Kiongozi wa kanisa Kuu la Aglikana Morogoro Mch. Willison Mafunusi.
Baada ya lbada hiyo Mwili wa Marehemu uliingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea nyumbani kwao kijiji cha Kikuyu kilichopo kando kando ya barabara ya lringa Mkoani Dodoma ambapo jana jumatano alipunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Msemaji wa familia Charles Mdachi ambaye ni Kaka wa Marehemu alisema.
“ Jumapili majira ya asubuhi mdogo wangu alilalamika kusumbuliwa na shinikizo la damu’Presha ya kushuka.’
Akapelekwa hospital ya Mkoa madaktari walipomcheki walibaini ana Malaria 7 na Presha ya kushuka wakati wakiendelea na matibabu majira ya saa 7 mchana siku hiyo hiyo ya Jumapili mpendwa wetu alifariki dunia”alimalizia kusema na kuangua kilio ambapo Mwandishi wa Mtandao huu akaradhimika kubeba jukumu la kumbembeleza.
Enzi za uhai wake Marehemu alishika nyadhifa mbali mbali kwenye Jamii hadi umauti unamkuta Hayati Mdachi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha wachezaji Nyota wa zamani hapa Tanzania wenye makao yake Makuu jijini Dar unajulikana kwa jina la [UMSOTA Tananzia].
Marehemu Mdachi pia alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Uchaguzi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro.na Kiongozi wa timu ya Reli Family Veterani inayafanya mazoezi yake kila siku uwanja wa Shule ya Msingi Mwere.
Kama hiyo haitoshi Hayati Mdachi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mtaa wa Reli Estate na Mshauri wa Kanisa la Anglikana Mtaa wa Area Five Kichangani.
Baadhi ya watu mashuhuri walioshuhudiwa na Mwandishi wa habari hizi kwenye Msibani huo ni pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh Pascal Kihanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro.
Diwani wa Kata ya Mwembesongo Mh Ally Nyau,Diwani wa kata ya Kichangani Mh Gilbert Mtafani na Mwanasiasa Maarufu Mkoani wa Morogoro Abed Mlapakolo aliyewahi kumbea Ubunge Jimbo la Morogoro kwa leseni ya Chama cha CUF kwa awamu mbili ambapo awamu zote mbili kwenye boksi lake kula hazikutosha.
Wengine ni Askofu Mstaafu wa Anglikana Jimbo la Morogoro Baba Askofu Mageni, Shehe wa Msikiti wa Mji Mpya Sheke Kassimu na Mwanasheria Maarufu Mkoa wa Morogoro Peter Kimath ambaye Kitaaluma ni Mwandishi wa habari na Mwanachama wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya wachezaji wa zamani walioshuhudiwa na Mtandao huu kwenye Msiba huo ni pamoja na Amri lbrahim na Zamayoni Mogelle[Simba] Dotto Mokili [Yanga] Hussein Ngurungu[Pan Afrika] na Ally Bushiri Pamba ya Mwanza] na kundi kubwa la wachezaji nyota wa mzani wa Reli walizifunga Simba na Yanga Popote walipokutana nazo iwe Moro au kwao Dar walizipiga kama Ngoma na kupachikwa jina la Reli‘Kiboko ya Vigogo’.
Marehemu ameacha Mjane Mmoja Bi, Victoria Mdachi na watoto wawili Fred na Frida.
Katika Msiba huo Mwandishi wa Mtandao huu amenasa stori kubwa 2 moja ni kaka wa Marehemu kafunguka jinsi alivyofanya umanya mwaka 78 kuvamia kambi ya timu ya Reli akiwa na mashushu wa Simba wakamwiba Mdogo wake Hayati Mdachi na kumpeleka Simba akacheza mchezo wa Kimataifa dhidi ya AC Vita ya Congo.
Stori ya Pili ambayo itaruka kwenye ujumbe wa neno la Mungu Jumapili ijayo ni sehemu ya Mahubiri Mazuri ya Mchungaji Mafunusi Somo hilo likibeba ujumbe wa kusahau akiwashukia wanawake wanaotembea mitaani nusu uchi akikadhia hilo kwa kutaja wimbo wa Msanii Hussein Machozi.
Kwa habari hizo na nyingine moto moto endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment