Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Taa za barabarani Manispaa ya
Morogoro zinazopendezesha Mji zinazidi kutoweka baada ya kukumbwa na hujuma
mbali mbali zikiwemo kuibiwa na kugongwa na magari.
Juzi Mwandishi wa Mtandao huu
Majira ya asubuhi akitokea maeneo ya Nane nane alikatiza barabara Mpya ya Kolla
na kushuhudia taa mbili zikiwa chini
jirani na kituo cha Mafuta.
Mwanahabari huyo alitimiza
majukumu yake ya Uandishi kwa kuzipiga
Picha taa hizo kisha kufanya mahojiano na Majirani wa eneo hilo kwa lengo la kujua taa hizo zimekubwa na
kadhia gani, mashuhuuda hao walifunguka haya.
”Mara nyingi kunapokuwa na
misafara ya Viongozi kwenye barabara ile ya Dar Magari mengi yakiwemo Malori
hutumia njia hii ya Kolla, hivyo juzikati kuna Lori lenye mzigo mkubwa baada ya kupishana na Lori
lingine lilizidi kushoto na Kontena hilo likaziangusha taa hizi mbili”walisema
mashuhuda hao ambao ni madereva wa boda boda wanaoegesha Pikipiki zao nje ya baa
ya Vuga jirani na kituo cha Mafuta.
Walipoulizwa wao kama
wananchi na taa hizo ni Mali
ya wananchi zinazowasaidi kuwamulikia nyakati za usiku wamechukua hatua gani kuhusiana
na tukio hilo
la kihalifu? boda boda hao walijibu.
” Broo sisi tuchukue hatua
gani kweli mwenye Lori baada ya kuzigonga taa hizi mbili alisimama kwa muda
lakini baada ya kuona hakuna mtu yoyote anayemfuta na kumueleza lolote alipiga
gia kaondoka, hatujua kama amekwenda kwenye
mamlaka kulipa taa hizo au amekimbia”
Chaajabu siku iliyofutaa
Majira hayo hayo ya asubuhi Mwanahabari huyo alikatiza tena eneo hilo na kushuhudia taa
nyingine ikiwa chini jirani eneo la Maegesho ya Malori Kando kando ya barabara kuu
ya Moro-Dar jirani na Uwanja wa Maonyesha ya Wakulima Nane Nane.
Moja ya kazi ya Uandishi wa
habari ni pamoja na Upelelezi endelevu hivyo Muda huu wa asubuhi najianda
kupita tena eneo hilo kuchunguza kama kuna taa nyingine imeangushwa chini au la.
Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mtandao huu
umebaini taa moja gharama yake ni Shilingi Milioni 3.
lkumbukwe barabara hii
inyaoelekea makaburi ya Kolla inayoanzia eneo la Nane nane barabara Kuu ya
Moro-Dar na kuishia barabara ya zamani ya Dar ikikatiza eneo la Bingwa imejengwa kwa kiwango cha lami 2018.
Mwaka uliofuta 2019 Vibaka
walivamia eneo la Makaburi ya Kolla na kuiba Taa kadhaa ambapo Jeshi la Polisi
lilifanya doria nyakati za usiku na kufanikiwa kuwakamata vibaka hao na
kuwapeleka mahakama kwa kesi ya uhujumu uchumia.
Baada ya Jeshi la Polisi
kufanya kazi hiyo nzuri matukio hayo ya wizi wa taa hizo za solla umekoma kwa
sasa taa hizo zinapukutika kwa kugongwa na magari.
Mtandao huu unawakumbusha
TARURA kutinga eneo hilo
la tukio zilipo taa hizo na kuzifunga tena zisije zikaibiwa.