Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, February 27, 2023

MZEE MBEZI AWAKUBALI MAKOCHA 3 WA KAGERA SUGAR.

Kutoka kulia ni Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime, Kocha Msaidizi wa timu hiyo Ulimboka Mwakingwe, Mdau wa Soka Mkoani Morogoro Mzee Mbezi na mwisho ni Kocha wa Makipa wa Kagera Juma Kaseja kwa pamoja wakipozi mbele ya Kameea za kisasa za Mrandao huu

 


 

               Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 

Mzee Omary Mbezi Mkazi wa Kichangani Manispaa ya Morogoro amevunja ukimya na kutoa lake la Moyoni kwamba anawakubali vilivyo makocha watatu wa timu ya Kagera Sugar.

Mzee Mbezi[Pichani mwenye kanzu] ambaye ndiye aliyetuzia kile Kiwanja tulichomjengea nyumba yule ndugu yetu Mlemavu Mohamed Matama.

 

Mara baada ya gemu ya  Ruvu Shooting na  Kagera Sugar iliyopigwa kwishoni mwa wiki  Uwanja wa Jamhuri Morogoro kukamilika kwa  Kagera kuwanyuka wenyeji wao Maafande wa Ruvu bao 1-0

 

 Mzee huyo shabiki ‘lia lia’ wa Mtibwa Sugar alishuka jukwaani kwa kasi na mkuvaa Mwandishi wa Mtandao huu akisema” Shekidele nawakubalisa sana makocha wale watatu wa Kagera najua unawamudu hivyo naomba msaada wako kawakusanye wote watu njoona hapa nipige nao pocha ya kumbuku”alisema Mzee huyo.

 

Mwandishi wa Mtandao huu yeye ni nani apigane na ombi na Mtu mzima huyo hivyo aliingia uwanjani na kuwakusanya makocha hao   akawapeleka kwa Mzee huyo na kuwapiga Picha.

 

Makocha hao ambao wote ni wakazi wa Kata ya Kihonda Maghorofani Manispaa ya Morogoro waliotimkia Kagera kutafuta Maisha kutoka kulia ni kocha Mkuu wa Kagera Sugar Meck Mexime, Kocha Msaidizi Ulimboka Mwakingwe[mwenye kanzu Mzee Mbezi, Kocha wa Makipa Juma Kaseja na wa mwisho kushoto ni Shabiki Kindaki ndaki wa Mnyama Simba Afande Mdoe.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...