Kikosi cha Kagera Sugar
Wamuzi pamoja na Mech Kamishina[Kamisaa wa Mchezo] wakiwa katika picha ya pamoja na Manahodha wa timu zote mbili
Mashambuliaji wa Kagera Yusuf Mhilu akigombea Mpira na beki wa Ruvu
Mshambuliaji wa Ruvu Baraka Mtuwi [kulia] akitafuta m,binu wa kumtoka beki wa Kagera Meshack Abrahama
Baada ya mbinu zake kufeli kufuatia kubannwa vilivyo na beki Meshack,
Bao la wazi kiungo fundi wa Ruvu Zuberi Daby Mkazi wa Kichangani Morogoro akiruka juu kufunba bao huku kipa wa Kagera Ramadhan Chalamanda akipuyanga na kuliacha gori wazi.
Hata hivyo Daby alishindwa kufunga bao hilo kufuatia kuukosa mpira huo wa juu na kusababaisha mashabiki wa timu hiyo kubaki midomo wazi.
Bao la Kagera lilianzia hapa, Hamis Kiiza kulia akiunyatia mpira mbele ya beki wa Ruvu
Kiiza kafanikiwa kunasa mpira huo na kufunga bao la ushindi akimuacha kipa wa Ruvu lsihaka Hakimu akidaka nyasi za uwanja wa Jamhuri huku mpira ukitinga wavuni kama unavyoonekana Pichani mpira huo ukinasa kwenye nyavu
Hamisi Kiiza 'Diezo[ akishangilia bao hio
.....Akipongezwa na wenzie
Furaha ya ushindi unapelekea wachezaji wa Kagera kubebena juu na jenga Mlima kama huo wa Uluguru unaoonekana pichani
....Wachezaji wa Kagera wakibusu mguu wa Kiiza uliofunga bao hilo la ushindi
Hamisi Kiiza akipozi mbele ya kamera pekee za Mtandao huu zilizokuwa nyuma ya gori la Ruvu
Hamiis Kiiza akichungwa na beki wa Ruvu
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Jahazi la Maafande wa Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani linazidi kuzama baada ya jana kukubari kichapo cha bao 1-0 nyumbani dhidi ya wageni wao Kagera Sugar.
Wanajeshi hao wa Jeshi la Kujenga Taifa’JKT’ kutoka Mlandizi Mkoani Pwani walioamua kuutumia Uwanja wa Jamhuri Morogoro kufuatia uwanja wao kukosa vigezo vya kutumika kwa michezo ya ligi kuu Tanzania Bara wanashika mkia kwenye ligi kuu wakiwa na alama zao 17.
Kwenye gemu hiyo ya Jana ‘Wajeda’hao walipambana kufa na kupota kusaka ushindi lakini walibanwa maeneo yote na Wakatamiwa hao kutoka Mkoani Kagera hadi hadi dakika ya 89 timu hizo zilikuwa sale ya 0-0.
Wakati Mwamuzi akijiandaa kupuliza kipenga cha kumaliza mchezo huo dakika ya 90 Mshambuliaji wa Kagera Sugar Hamis Kiiza’Diego’ raia wa Uganda alipeleka majozi kwa Maafande wa Ruvu Shooting baada ya kufunga bao hilo pekee dakika hizo za mwishoni mwa mchezo.
Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye gemu hiyo ikiwemo tukio la wachezaji wa Kagera Sugar kuwabembeleza wachezaji wa Ruvu waliokuwa wamejiinamia baada ya mcheo huo kutamatika.
Kwa matukio yote hayo endelea kuwa jirani na Mtandao Pendwa wa shekidele Muda wote.
Kwa sasa fungua Profaili la Mtandao huu ushuhudia matukio mbali mbali ya mchezo huo ikiwepo picha ya bao hilo pekee.
No comments:
Post a Comment