Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, February 24, 2023

TAA ZA BARABARANI M0RO ZAENDELEA KUHUJUMIWA.




 


 

             Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 

Taa za barabarani Manispaa ya Morogoro zinazopendezesha Mji zinazidi kutoweka baada ya kukumbwa na hujuma mbali mbali zikiwemo kuibiwa na kugongwa na magari.

 

Juzi Mwandishi wa Mtandao huu Majira ya asubuhi akitokea maeneo ya Nane nane alikatiza barabara Mpya ya Kolla na kushuhudia taa mbili  zikiwa chini jirani na kituo cha Mafuta.

 

Mwanahabari huyo alitimiza majukumu yake ya Uandishi  kwa kuzipiga Picha taa hizo kisha kufanya mahojiano na Majirani wa eneo hilo kwa lengo la kujua taa hizo zimekubwa na kadhia gani, mashuhuuda hao walifunguka haya.

 

”Mara nyingi kunapokuwa na misafara ya Viongozi kwenye barabara ile ya Dar Magari mengi yakiwemo Malori hutumia njia hii ya Kolla, hivyo juzikati kuna Lori  lenye mzigo mkubwa baada ya kupishana na Lori lingine lilizidi kushoto na Kontena hilo likaziangusha taa hizi mbili”walisema mashuhuda hao ambao ni madereva wa boda boda wanaoegesha Pikipiki zao nje ya baa ya Vuga jirani na kituo cha Mafuta.

 

Walipoulizwa wao kama wananchi na taa hizo ni Mali ya wananchi zinazowasaidi kuwamulikia nyakati za usiku wamechukua hatua gani kuhusiana na tukio hilo la kihalifu? boda boda hao walijibu.

 

” Broo sisi tuchukue hatua gani kweli mwenye Lori baada ya kuzigonga taa hizi mbili alisimama kwa muda lakini baada ya kuona hakuna mtu yoyote anayemfuta na kumueleza lolote alipiga gia kaondoka, hatujua kama amekwenda kwenye mamlaka kulipa taa hizo au amekimbia”

 

Chaajabu siku iliyofutaa Majira hayo hayo ya asubuhi Mwanahabari huyo alikatiza tena eneo hilo na kushuhudia taa nyingine  ikiwa chini jirani eneo la  Maegesho ya Malori Kando kando ya barabara kuu ya Moro-Dar jirani na Uwanja wa Maonyesha ya Wakulima Nane Nane.

 

Moja ya kazi ya Uandishi wa habari ni pamoja na Upelelezi endelevu hivyo Muda huu wa asubuhi najianda kupita tena eneo hilo kuchunguza kama kuna taa nyingine imeangushwa chini au la.

 

 Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mtandao huu umebaini taa moja gharama yake ni Shilingi Milioni 3.

 

lkumbukwe barabara hii inyaoelekea makaburi ya Kolla inayoanzia eneo la Nane nane barabara Kuu ya Moro-Dar na kuishia barabara ya zamani ya Dar ikikatiza eneo la Bingwa  imejengwa kwa kiwango cha lami 2018.

 

Mwaka uliofuta 2019 Vibaka walivamia eneo la Makaburi ya Kolla na kuiba Taa kadhaa ambapo Jeshi la Polisi lilifanya doria nyakati za usiku na kufanikiwa kuwakamata vibaka hao na kuwapeleka mahakama kwa kesi ya uhujumu  uchumia.

 

Baada ya Jeshi la Polisi kufanya kazi hiyo nzuri matukio hayo ya wizi wa taa hizo za solla umekoma kwa sasa taa hizo zinapukutika kwa kugongwa na magari.

 

Mtandao huu unawakumbusha TARURA kutinga eneo hilo la tukio zilipo taa hizo na kuzifunga tena zisije zikaibiwa.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...