Mkurugenzi wa MODICO Ngungamtitu akimjibu Bi Pili
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WALEMAVU kupitia Taasisi yao ya Morogoro Disability Devolopment and lmfomation Center Organization, ikiwa na maana ya Taasisi ya Maendeleo na Upashaji Habari kwa Watu wenye Ulemavu[MODICO] wametoa sauti kali wakiwakumbusha Viongozi wao juu ya Bima zao za Afya.
Hali hiyo imetokea kwenye hafla ya Siku ya Wapendanao ‘Valentine Day’iliyofanyika Februari 14 kwenye ukumbi wa Young Women Christian Association [Y.W.C.A.]Uliopo jirani kabisa na geti kuu la hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo siku hiyo Walemavu hao kupitia umoja wao huo wa MODICO waliamua kujinadalia sherehe ya kuonyeshana Upendo wenyewe kwa wenyewe kwenye kilele cha siku hiyo ya wapendao duniani.
Kwenye hafla hiyo Viongozi wa MODICO walitoa nafasi ya wanachama wao kuliza maswali kwa Viongozi wao baada ya nafasi hiyo kutolewa Walemavu wengi walinyoosha vidole wakiomba nafasi ya kuliza maswali ambapo Bi Pili Mohamed alikuwa wa kwanza kupewa nafasi hiyo aliuliza swali la ahadi ya Bima za Afya waliohadiwa toka Mwaka jana na Viongozi wa Manispaa ya Morogoro.
Akijibu swali hilo Mkurugenzi Mkuu wa MODICO Othuni Ngungamtitu alidai kwamba nao wanapigwa danadana na Viongozi wa Manispaa akiwaomba wanachama wake hao walemavu kuendelea kuwa na uvumilivu wakati juhuzi zao za kulifuatilia jambo hilo zikiendelea.
Baada ya kikao hicho Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuzungumza na Mkurugenzi huyo ambapo aliendelea kufafanua jambo hilo kwa kusema.
“ Wanachama wangu wanahaki ya kuuliza ishu hiyo ya Bima ya Afya kwa jazba, pale ndani nimeshindwa kufafanua zaidi lakini kwa vile umeniuliza acha nikupe ukweli ni kwamba April 12 2022 [Mwaka jana] tulikaa kikao chetu cha kwanza kilichohudhuriwa na wanachama 51
Kwenye kikao hicho tuliwaalika Vigogo wa Manispaa kutoka Vitengo mbali mbali a ambapo alifika Afisa wa Maendeleo ya Jamii TASAF, alifika pia Afisa wa kitengo cha Bima ya Afya Manispaa, alikuwepo Afisa anayeshungulikia Mikopo ya asilimia 2 ya watu wenye ulemavu kutoka Manispaa.
Kwenye kikao hicho Walemavu wenzangu alimuomba Afisa huyo wa Bima ya Afya kuwasaidi kadi za bima ya Afya ambapo dada huyo alikubali ombi hilo mbele ya kikao hicho lakini cha ajabu kila nikimpigia simu anadai swala hilo ameshalifikisha kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo anasuburi majibu”alisema Mkugurunzi huyo wa MODICO.
Kwa sauti ya upole Mtandao huu unaomba wahusika wote wa Bima ya Afya kuyatazama maombi ya ndugu zetu hao kwa jicho la huruma.
Ingia kurasa za facebook za Dustan Shekidele na ile ya shekidele Mkude Simba uangalia Clip Video za tukio hili A-Z
No comments:
Post a Comment