Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, February 26, 2023

HUZUNI YATAWARA MAAFANDE RUVU SHOOTING WAKIPOKEA KICHAPO.

Baada ya mwamuzi kumaliza mchezo baadhi ya wachezaji wa Ruvu Shooting walijitupa chini kwa uchungu wa kufungwa nyumbani na Kagera Sugar
Wachezaji wawili wa Kagera sugar wakimfariji mchezaji wa Ruvu Kassim Suleman[aliyeketi chini]
Nahodha wa Ruvu Zuberi Daby akiinamisha kichwa chini kwa uchungu baada ya Mwamuzi kumaliza mchezo huo juzi.
Juma Kaseja [Kulia] akimfariji kocha msaidizi wa Ruvu.

 

 


 

                    Na Dustana Shekidele,Morogoro.

 

Huzuni imetawara baada ya Maafande wa Ruvu Shooting kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wageni wao Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa juzi uwanja wa Jamhuri Mkoani hapa.

 

Kichapo hicho kimeifanya timu hiyo ya Ruvu  kutoka  Mlandizi Mkoa wa Pwani kuendelea kuburuza mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoelekea ukingoni wakiwa na Pointi 17 huku Yanga inayoongoza ligi hiyo ikiwa na Pointi 65.

 

 Baada ya Mwamuzi kumaliza mchezo huo  baadhi ya wachezaji wa Ruvu walijiangusha chini kwa uchungu kwa kichapo hicho kinacho wasafishia njia ya kushuka daraja.  

 

Kufuatia hali hiyo baadhi ya wachezaji wa Kagera Sugar waliacha kushangilia ushindi huo na kubeba jukumu la kuwafariji wacheaji hao wa Ruvu.

 

Hali kadharika  Kocha msaidizi wa Kagera Sugar Juma Kaseja alitinga kwenye benchi la Ruvu na kumfariji kocha msaidi wa timu hiyo.

 

 Miongoni mwa mikakati ya maafande hao wa Ruvu ilikuwa kushinda michezo yote ya nyumbani wakipigania kutoshuka daraja, hivyo kupoteza mchezo huo muhimu nyumbani ndio sababu ya wachezaji hao kujawa na machungu moyoni.

 

 Baada ya mchezo huo Ruvu wanakwenda Mbeya kucheza mechi mbili ya kwanza watakipiga na Mbeya City huku gemu ya Pili wakikipiga na Tanzania Prisons timu zote hizo ziko kwenye janga la kushuka daraja.

 

Ruvu wakitoka Mbeya watareja nyumbani Morogoro kukipiga na ‘Wana ramba ramba’ Azam Fc inayopigania kushika nafasi tatu za juu.

 

Kwa mpangilio wa ratiba hiyo miujiza ya Mungu pekee ndio  inayohitajika kuinasua timu  ya Ruvu kujinasua na janga la kushuka daraja.

 

                               

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...