Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, September 29, 2022

MASHINDANO YA BANDARI 2022 BANDARI TANGA WAWATOA NISHAI BANDARI TANGA.


Mabaunsa wa bandari Dar licha ya kutuma kama nungu nungu lakini walivutwa kama ngoma na wababe wao Bandari kutoka jiji la mahaba la Tanga


..Wababe wa Dar Bandari Tanga wakiwavuta  mabaunsa wa Bandari Dar nje ndani

 


Na Dunstan Shekidele.Morogoro. 

Mashindano ya bandari na Maziwa yamezinduliwa Septemba 26 kkwa mchezo wa kuvuta kamba kati ya Mabaunsa wa kiume wa Bandari Tanga na wenzao wa bandari Dar es salaam.

 

Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Mgeni rasmi Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh Tabia Maulid Mwita, Mabaunsa wa bandari Tanga a.k.a Watu Kazi[Jezi za Bluu] waliwatoa ushamba Mabaunza wa Bandari Dar es Salaam[Jezi rangi ya bahari] kwa kuwavuta katika michezo yote miwili.

 

Baadae Mtandao huu utarusha hewani mabausa wa kike wa timu hizo wakionyeshana umwamba,hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

VIGOGO CCM NAO WATOA MSAADA KWA WAHANGA WA JANGA LA MOTO.


Vigogo wa CCM Kata ya Mji Mpya wakipozi mbele ya kamera za Mtandao huu kabla ya kukabidhi msaada kwa wahanga wa janga la Moro.
Kutoka kushoto waliosimama ni Katibu mkuu wa JWT Kata ya Mji Mpya Bi.Adella Mdede'Mrs Mlowa au Mwalimu Mlowa Chukia Abdallah Mjumbe wa halmashauri kuu JWT Kata. Kombo Nkumilwa Mwenyekiti wa CCM Kata.Melle Kunambi Katibu Mkuu wa CCM Kata.Seleman Kasanga Katibu Mwenezi Kata na Rehema Matonya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa ngoma C Kata ya Mji Mpya.
Waliochutama kutoka kushoto ni Zaituni Rajabu Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi tawi la Ngoma na kulia ni Amir Benne Mhasibu Kata ya Mji mpya..






 


 

             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi’CCM’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa.wiki iliyopita wametinga mtaa wa Makaburi C Kata ya Mji Mpya kuwapa pole Kata 9 zilizounguliwa na nyumba yao mwanzoni mwa mwezi huu.

 

Viongozi hao wa Chama tawara waliotinga kwenye eneo hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mji Mpya Kombo Nkumilwa, Katibu Mkuu wa CCM Kata Melle Kunambi, Katibu Mwenyezi Kata Selemani Kasanga na Katibu wa JWT Kata Adelle Mdede’Mrs Mlowa Maarufu Mwalimu Mlowa.

 

Wengine ni Chukia Abdallah Mjumbe Halmashauri Kuu JWT Kata, Zaituni Rajab Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi tawi la Ngoma na Rehema Matonya Mwenyekiti Serikali ya Mtaa wa Ngoma C Kata ya Mji Mpya kwa leseni ya CCM.

Vigogo hao wa CCM Kata waliongozana na Afisa Mtendaji Tekla Mbaruko mwenye gauni la kitenge pichani na Mwandishi wa habari hizi.

 

 Kabla ya kumkaribisha Mkuu wa msafara huo kuzungumza na wahanga hao  Mwenyekiti wa CCM Kata, Katibu Mkuu CCM Kata Bi, Melle Kunambia aliwapa pole wahanga hao kwa janga hilo la Moto akisema CCM Kata ipo pamoja nao kwenyekiti hiki kigumu wanachopitia.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata Nkumilwa,mbali ya kuwapa pole kaya hizo 9 pia aliwapa kifuta jasho la shilingi laki moja kwa maana kila kaya  elfu 11.

 

”Mtakumbuka siku ya tukio Jumapili iliyopita wakati nyumba inaungua majira ya saa 12 jioni mimi nilikuwa hapa mpaka saa 5 usiku nikihakikisha kaya zote 9 mnapata sehemu ya kulala kwa usiku ule”alisema Mwenyekiti huyo  aliyeingia madarakani takribani miezi 2 iliyopita baada ya kuibuka kidede kwenye uchaguzi mkuu wa CCM Kata akimbwaga mpinzani wake mkubwa Said Kondo aliyekuwa akikalia kiti hicho. 

Mwanzoni mwa wiki hii Viongozi na Wanachama wa Matawi Makuu ya Simba na Yanga  Mkoani Morogoro yenye Maskani yao Kata hiyo ya Mji Mpya kwa pamoja waliweka kando tofauti zao wakaungana kutoa Msaada kwa kaya hizo 9.

Wednesday, September 28, 2022

WAZIRI WA ZANZIBAR JUZI AMEFUNGUA MASHINDANO YA BANDARI MOROGORO


Mkuu wa Wilaya wa Morogoro akiwasili Uwanja wa Jamhuri Morogoro
...Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwasili uwanja wa Jamhuri Morogoro
Wafanyakazi wa Bandari na Maziwa wakiingia uwanja wa Jamhuri kwa maandamano yaliyoongozwa na Matarumbeta






Wanamichezo wa bandari waliofariki dunia kwa sababu mbali mbali
Kiongozi wa wamuzi Wilaya ya Morogoro Juma Simba akira Kiapo cha kutenda haki yeye na wamuzi wenzi kwenye mashindano hayo
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro  Mh Albart Msando akizungumza kwenye uzinduzi huo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania Juma Kijafara
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortnatus Muslim

             Kundi la wanamichezo hayo wakizagaa uwanjani
.....Waziri Tabia na mwenyeji wake Msando wakielekea uwanjani kuzindua mashindando hayo
        Waziri Tabia Mwita akifungua mashindano hayo

 

Mzee wa Nyakua nyakua akiwa na Mwandishi wa Mtandao huu.

. Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

WAZIRI wa Habari,Vijana, Utamaduni, na Michezo kutoka Serikali ya Mapunzi ya Zanzibar Mh Tabia Mauli Mwita, juzi amefungua mashindano ya 16 ya Bandari na Mziwa Tanzania bara na Visiwani.

 

 Zawadi wa wafanyakazi mia 5 kutoka Bandari za Dar es salaam, Tanga, Mtwara na Zanzibar pamoja na Maziwa ya Victor, Nyassa na Tanganyika kutoka Mikoa ya Mwanza na Kigoma wanashiriki mashindano hayo yaliyoanza Septemba 26 na kutamatika Octobar 3.

 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mashindano hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Jamhuri na Chuo Kikuu cha Kiislama Morogoro’MUM’ kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania Juma Kijafara ameiomba serikali  mashindano hayo yafanyike mara 2 kwa mwaka tofauti na sasa ambapo yanafanyika mara 1 kwa Mwaka. Naye Waziri wa Tabia Mwita aliwaomba waandaji mwakani Mashindano hayo yafanyike kwenye visiwa vya karafuu Zanzibar huku akilipokea ombi la Viongozi hao kuomba mashindano hayo kufanyika mara kwa Mwaka.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albeth Msando aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa aliwahakikishia usalama wanamichezo hao kwa siku 8 watakazokuwa mkoani Morogoro.

 

”RPC Musilim Mzee wa Nyakua nyakua yuko hapa anasikia ahadi hii hii, pia kwa Morogoro kuna vivutia vingi zikiwemo mbugha za wanyama hivyo mtakapopata nafasi tembeleeni vivutio hivyo” alisema Mkuu huyo wa Wilaya aliyetinga uwanjani hapo na suti ya kombati.

 

 Kabla ya Waziri huyo kuzindua mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya 5 mfurulizo Mkoani Morogoro,washiriki wote walisimama kwa dakika 1kuwaombea wanamichezo 2 waliofariki dunia siku kabla ya mashindano hayo kuanza

 

 Kama kawaida Mwandishi wa Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye ufunguzi huo hivyo endelea kuwa jirani na Mtanda huu muda wote.

 

Monday, September 26, 2022

DENT WA LA 7 APOKEAKICHAPA NA KUPOTEZA FAHAMU AKIDAIWA KUKWAPUA BAISKELI.

Mama Mzazi wa Mtoto huyo akihojiwa na Mtandao huu
           .....Mama huyo akiwa na Mwenyekiti wa Mtaa Ally Msungi
....Wasamalia wema wakimpepe mtoto huyo akidaiwa kupoteza fahamu kw akichapo
...Dent huyo wa la 7 akipelekwa kwenye Bajaji tayari kw akukimbizwa hospital


 


            Na Dunstan Shekide,Morogoro.

UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona ya Filahuni, wakati Jeshi la Polisi kwa sasa likiwa kwenye Oparesheni kabambe ya kupambana na Watoto sugu wa Mtaani ‘Maarufu Panya Road’ Mtoto Benjamin  Francis[13]anayesoma darasa la 7 shule ya Msingi Mtawara Mkoani hapa, amepokea kichapo ‘hevi’ kutoka kwa watu mbali mbali akiwemo baba yake Mzazi akituhumiwa kutoroka shuleni na kwenda Mtaani kutapeli baiskeli.

 

Tukio hilo la kushangaza lililovuta umati mkubwa wawatu limetokea Jumatano iliyopita Majira ya saa 8 Mchana Mtaa wa Saadani Kata ya Mwembesono Manispaa ya Morogoro.

 

Wakati dent huyo akiendelea kupokea kichapo  baadhi ya wananchi walitoa taarifa sahihi kwa Mwandishi wa habari hizi aliyetinga fasta eneo la tukio na kumkuta dent huyo akiwa ‘amezima’ nje ya ofisi ya Mwenyekiti wa Mtaa huku akipatiwa huduma ya kwanza ya kuongezewa hewa kwa ‘kupepe na nguo’.

 

 Wakizugumza na Mtandao wa Shekidele Mshuhuda wa tuko hilo akiwemo Salum Juma walisema.

 

” Huyu mtoto ni mwizi sana hapa Mtaani anakwapua vitu vya watu akikodi baiskeli haludishi mpaka umtafute mitaa yote ya Morogoro hivyo  wakodisha wa baskeli wote waligoma kumkodishia baskeli zao.

 

 Kwa kutambua hilo leo Benja katumia utapeli kamchukua mtoto wawatu wa miaka kama 6 hivi kampa mia 2  kamtuma akakodishe baskeli ampelekee.

 

Alivyoletewa  baiskeli hiyo majira ya saa 4 asubuhi kaichukua na kuzunguka nayo mitaani huku akiwa na sare za shule na begi la madaftari”.walisema mashuhuda hao na kuongeza kudadavua.

 

Mmiliki wa baiskeli hiyo baada ya kuona muda unaenda baiskeli  hailudishwi toka  saa 4 mpaka saa 6 ilihali  kalipwa mia 2 ya nusu saa kamua kwenda kwa wazazi wa huyo mtoto aliyekwenda kukodi, alipofika wazazi hao wakashangaa wakamwita mtoto wao walipomuliza kasema alitumwa kukodisha baiskeli hiyo na Benja.

 

Hivyo wazazi hao kwa kushirikiana na mmiliki wa baiskeli hiyo wakaingia mtaa kumtafuta Benja na kufamikiwa kumpata Majira ya saa 8 mchana Kata ya Kichangani umbali wa takribani kilomita 2 kutoka Mtaa huu akiwa na baiskeli hiyo.

 

Kwa hasira wakamshushia Kichapo kisha wakamkamata na kumleta hapa kwa Mwenyekiti wa Mtaa ambaye aliwaita wazazi wake kwa lengo la kuendesha kesi hiyo cha ajabu baba yake alipofika kwa hasira kamchapa teke tumboni ghafla tukaona Benja amezimia ndio maana unaona tunampepea”alisema Shuhuda huyo.

 

 Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Saadan  Ally Msungi amethibitisha kutoka kwa tukio hilo.

 

”Mtoto huyu ni mtukutu sana hapa ofisini  kuna kesi zake kibao za wizi asububi akiwa na hizi  sare za shule kwa vile  haminiki kwa wizi katumia utapeli kampa mtoto mwingine mia 2 akamkodia baiskeli.

 

Alipokabidhiwa katokomea nayo toka asubuhi mpaka sahizi wamiliki wa baiskeli  walipoingia Mtaa kumsakana na kufanikiwa kumkamata Kichangani na kumleta hapa akiwa hana shati nikawaita wazazi wake baba yake kwa hasira alipofika hapa alimchapa pete mtoto kaluka juu alivyoanguka chini kapoteza fahamu muda huu  tumeita Bajaj tumkimbize hospital”alisema Mwenyekiti huyo.  

 

Baba wa Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Francis Edward baada ya tukio hilo anadaiwa kutoweka eneo hilo akihisi huenda amemuua mwanae kwa kichapo hicho.

 

Kwa upande wake Mama mzazi wa Mtoto huyo Bi Ferister Thomas aliyekuwepo eneo la tukio akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi huku akirekodiwa alikiri Mwanae huyo kuwa na tabia ya wizi.

 

“ Vitu viko wazi siwezi kumtete mwanangu kweli anatabia mbaya mfano asubuhi  kaaga  ana kwenda shule na sisi wazazi tunajua yuko shule, muda huu tunaitwa kwa mwenykiti tukielezwa kwamba anadaiwa kutapeli  baiskeli ya watu, siku za nyuma alifanya matukio ya kihalifu baba yake kapelekwa Polisi. hapa kwa mwenyekiti kila siku tunaitwa kwenye kesi zake.  

 

Kwa sasa nimechanganyikiwa nina kazi mbili za kumchunga huyu Mtoto na tabia zake mbaya  lakini pia kumchunga baba yake apunguze hasira unajua tena wakulia wanahasira kali asije akamdhuru  na yeya akaishia magereza nikakosa vyote”alisema mama huyo huku akiangua kilio kwa uchungu.

 

 Alipoulizwa ana watoto wangapi na alipo muwe wake kwa sasa baada ya tukio hilo alijibu.

 

” Nina watoto 4 na huyu Benja ndio wa kwanza, kuhusu alipo Mume wangu kwa sasa nahisi baada ya kumpiga teke mtoto wake na kupoteza famua ameogopa ameondoka  eneo hili  hakumpiga sana nahisi na njaa imechangia Benja kupoteza fahamu kwani toka asubuhi saa 12 alivyokunywa chai hajala chakula mpaka muda huu wa saa 9”alisema Mama Benja.

 

Siku iliyofuata Mwandishi wa habari hizi alitinga shule ya Msingi Mtawara ambapo Mwalimu wa darasa la Saba Diana Kanyamwaswa alipotakiwa kuelezea tabia na maendelea ya Mwanafunzi wake Benjamini Francis alisema.

 

” Mtoto huyo ni mtukutu sana pia ni mtoro anasiku mbili hajafika shuleni  nasikia jana kakamatwa huko Mitaani na baiskeli ya watu”alisema Mwalimu huyo.

 

Hadi tuna kwenda mitamboni juhudi za kumpata baba wa mtoto huyo ili azungumzie tukio hilo ziligonga mwamba kwani licha ya Mwandishi wa habari hizi kutinga nyumbani kwake zaidi ya mara 3 na mara ya mwisho ikiwa  juzi jumamosi  mzazi huyo  hakupatikana huku mkewe akidai mumewe baada ya tukio hilo siku iliyofuata  alisafiri kuelekea jijini Dar es salaam.

 

Alipoulizwa maendelea ya kiafya ya Benjani Bi Felister alisema kwa sasa anaendelea vizuri baada ya juzi kuruhusiwa kutoka hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alipolazwa kwa siku .kadhaa

             

 

Sunday, September 25, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU LEO JUMAPILI, MUNGU AMEAGIZA TUKAIJAZE NCHI.

Mtumishi wa Mtandao huu Pichani Kulia alitii agizo hilo la Mungu akaijaza nchi ya Tanzania kwa kuwaleta duniani watoto wawili aliofanana nao Tumaini Dastan Shekidele[[kushoto] na Neema Dastan Shekidele[Kati]
                                             Tumaini na Neema
...Tumaini na Neema wakiwa na Afande Sele ambaye ni rafiki mkubwa wa baba yao

 Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Mkali wa Mashairi Seleman Msindi' Afande Sele' akimkisi Mwanae Neema Dustan Shekidele

 

MWANZO 1. 27-29

“Mungu akaumba Mtu kwa Mfano wake,kwa mfano wa Mungu,alimwumba mwanaume na mwanamke aliwaumba.

 

Mungu akawabariki.Mungu akawaambia, Zaeni Mkaongeze,mkaijaze nchi na  kuitisha mkatawale Samaki na bahari na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

 

Mungu akasema tazama nimewapa kila mche utoao mbegu,ulio juu ya uso wa nchi yote pia na kila mti ambao matunda yake  yana mbegu  vitakuwa ndio chakula chenu”Hilo ndilo neno letu la Mungu leo Jumapili Septemba 25.                                          


Saturday, September 24, 2022

YANGA, SIMBA WAONDOA TOFAUTI ZAO WAUNGANA KUSAIDIA FAMILIA MOROGORO.

Wanachana wa Yanga na Simba wakitoka tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro wakielekea kukabidhi Misaada wa kaya 9
Mhasibu Msaidizi wa tawi la Simba Maarufu tawi la Shujaa Ngome Kuu Mogella 'DHL'akiteta jambo na Mwenyekiti wa tawi kuu la Yanga lssa Chabala huku wakielekea eneo la tukio








...Wenyetivi wa matawi ya Simba na Yanga Said Mkwinda wa kwanza kushoto mwenye jezi ya Simba na lssa Chabala mwenyekiti wa tawi kuu la Yanga wakimkabidhi madaftari Husna Bernard akipokea misaada hiyo kwa niaba ya wenzake
....Mmoja wawahanga hao akiangua kilio baada ya kuchomwa na maneno yaliyosema na mmoja wawahanga wenzake Husna Bernard
Kaimu mwenyekiti wa Tawi la Simba Samora Mwarabu naye akikabidhi Msaada wake kwa familia hizo
....Mzee Mwambeta ambaye ni mmoja wa viongzo wa Baraza la Wazee wa tawi la Simba naye akitoa msaada wake kwa familia hizo
Maafande wa Kikosi cha Zima Mato na Uokoaji Mkoa wa Morogoro wakizima Moto huo siku ya tukio Jumapili iliyopita.

 

 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Wanachama wa matawi Makuu ya Simba na Yanga Mkoa wa Morogoro juzi wameweka kando tofauti zao na kuunga pamoja kwenda kutoa msaada kwa kaya 9 zilizokosa makazi baada ya nyumba waliokuwa wakiishia  kuteketea kwa Moto wiki iliyopita..

 

Nyumba hiyo  iko  Mtaa wa Makaburi C kata ya Mji Mpya  jirani kabisa na ofisi kuu za matawi hayo ya Simba na Yanga yenye nguvu kubwa kwa timu hizo kongwe nchini zenye makao yake Makuu Jijini Dar es Salaam.

 

Wanachma hao  waliongozwa na wenye viti wao wa matawi  Mwenyekiti wa tawi la Yanga lssa Kitukwa Maarufu lssa Chabala na Mwenyekiti wa tawi kuu la Simba Said Mkwinda. ambao kwa pamoja walimkabidhi vifaa vya shule, kwa wanafunzi wa familia  hizo kwa  mmoja wa wahanga hao Husna Bernard

 

Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi wenyeviti hao wa matawi ambao pia ni wenyeviti wa serikali za Mitaa kwa leseni ya CCM  Issa Chabala mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa A Kata ya Mji Mpya na Said Makwinda Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Simu C Kata hiyo hiyo ya Mji Mpya walisema wameondoa tofauti zao na kuungana kutoa Misaada kwa familia hizo.

 

“ Kama unavyofahamu Shekidele majirani zetu walipata majanga ya kuunguliwa na nyumba yao na kaya 9 zimeathirika na tukio hilo tunaamini kwenye familia hizo wapo mashabiki wa timu zetu za Yanga na Simba vile vile wahanga hao ni majirani zetu  kwa sababu hizo sisi viongozi wa matawi tumeketi kikao tukakubalia kuwashirikishe wanachama wetu kuchangia chochote kwa lengo la kuwapa misaada wenzetu hawa”walisema wenyeviti hao,

 

Kwa upande wao wahanga hao kupitia mwakilishi wao Husna Bernard wamewashukuru wanachama hao wa Simba na Yanga kwa Msaada huo.

 

” Tunashukuru sana kwa msaada ya madaftari kalamu na Soksi tunaamini kesho Vijana wetu watakwenda shule kwani toka tukio litokee hawajaenda shule baada ya madafutali yao na sale  zao shule kuteketea kwa Moto”alisema Husna na kuongeza kusema

 

” lngawa mpaka sasa hawana sale za shule watakweda shule na nguo za nyumbani mpaka tutakapopata wasamalia wengine wenye wa kusaidia sale hizo za shule,kikubwa wamepata Madaftari na kalamu kwani baadhi ya watoto wetu wako darasa la saba na mitihani ya taifa inakaribia hivyo kuendelea kukaa nyumbani wanapitwa na masomo”alimalizia kusema Husna kauli hiyo ilimzima mmoja waaanga hao kama anavyoonekana Pichani akifuta machozi.

 

 Nyumba hiyo iliteketea kwa Moto Jumapili iliyopita majira ya saa 12 jioni na kuteketeza nyumba hiyo iliyokuwa na nyumba 9 ambapo vifaa vyote vya wapangaji hao 9 ziliteketea kwa moto hali iliyosababisha kaya hizo 9 kuhifadhiwa kwa majirani nyakati za usiku na kwamba majira ya Mchana familia hizo zinashinda kwenye eneo la nyumba yao iliyoteketea kwa moto kwa lengo la kupokea pole na misaada kwa wasamalia wema. Mtandao huu unatoa wito kwa yoyote atakaye guswa na tukio hilo afike kwenye eneo hilo kuwaptia msaada familia hizo hasa chakula na sale za shule kwa wanafunzi wa familia hizo.

 

Kwa wale wageni eneo hilo alipotezi fika shule ya Msingi Mwembesongo kuna vijiwe vya boda boda mulize boda boda yoyote atakuonyesha eneo hilo kwa kile.

 

 

 

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...