Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, September 26, 2022

DENT WA LA 7 APOKEAKICHAPA NA KUPOTEZA FAHAMU AKIDAIWA KUKWAPUA BAISKELI.

Mama Mzazi wa Mtoto huyo akihojiwa na Mtandao huu
           .....Mama huyo akiwa na Mwenyekiti wa Mtaa Ally Msungi
....Wasamalia wema wakimpepe mtoto huyo akidaiwa kupoteza fahamu kw akichapo
...Dent huyo wa la 7 akipelekwa kwenye Bajaji tayari kw akukimbizwa hospital


 


            Na Dunstan Shekide,Morogoro.

UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona ya Filahuni, wakati Jeshi la Polisi kwa sasa likiwa kwenye Oparesheni kabambe ya kupambana na Watoto sugu wa Mtaani ‘Maarufu Panya Road’ Mtoto Benjamin  Francis[13]anayesoma darasa la 7 shule ya Msingi Mtawara Mkoani hapa, amepokea kichapo ‘hevi’ kutoka kwa watu mbali mbali akiwemo baba yake Mzazi akituhumiwa kutoroka shuleni na kwenda Mtaani kutapeli baiskeli.

 

Tukio hilo la kushangaza lililovuta umati mkubwa wawatu limetokea Jumatano iliyopita Majira ya saa 8 Mchana Mtaa wa Saadani Kata ya Mwembesono Manispaa ya Morogoro.

 

Wakati dent huyo akiendelea kupokea kichapo  baadhi ya wananchi walitoa taarifa sahihi kwa Mwandishi wa habari hizi aliyetinga fasta eneo la tukio na kumkuta dent huyo akiwa ‘amezima’ nje ya ofisi ya Mwenyekiti wa Mtaa huku akipatiwa huduma ya kwanza ya kuongezewa hewa kwa ‘kupepe na nguo’.

 

 Wakizugumza na Mtandao wa Shekidele Mshuhuda wa tuko hilo akiwemo Salum Juma walisema.

 

” Huyu mtoto ni mwizi sana hapa Mtaani anakwapua vitu vya watu akikodi baiskeli haludishi mpaka umtafute mitaa yote ya Morogoro hivyo  wakodisha wa baskeli wote waligoma kumkodishia baskeli zao.

 

 Kwa kutambua hilo leo Benja katumia utapeli kamchukua mtoto wawatu wa miaka kama 6 hivi kampa mia 2  kamtuma akakodishe baskeli ampelekee.

 

Alivyoletewa  baiskeli hiyo majira ya saa 4 asubuhi kaichukua na kuzunguka nayo mitaani huku akiwa na sare za shule na begi la madaftari”.walisema mashuhuda hao na kuongeza kudadavua.

 

Mmiliki wa baiskeli hiyo baada ya kuona muda unaenda baiskeli  hailudishwi toka  saa 4 mpaka saa 6 ilihali  kalipwa mia 2 ya nusu saa kamua kwenda kwa wazazi wa huyo mtoto aliyekwenda kukodi, alipofika wazazi hao wakashangaa wakamwita mtoto wao walipomuliza kasema alitumwa kukodisha baiskeli hiyo na Benja.

 

Hivyo wazazi hao kwa kushirikiana na mmiliki wa baiskeli hiyo wakaingia mtaa kumtafuta Benja na kufamikiwa kumpata Majira ya saa 8 mchana Kata ya Kichangani umbali wa takribani kilomita 2 kutoka Mtaa huu akiwa na baiskeli hiyo.

 

Kwa hasira wakamshushia Kichapo kisha wakamkamata na kumleta hapa kwa Mwenyekiti wa Mtaa ambaye aliwaita wazazi wake kwa lengo la kuendesha kesi hiyo cha ajabu baba yake alipofika kwa hasira kamchapa teke tumboni ghafla tukaona Benja amezimia ndio maana unaona tunampepea”alisema Shuhuda huyo.

 

 Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Saadan  Ally Msungi amethibitisha kutoka kwa tukio hilo.

 

”Mtoto huyu ni mtukutu sana hapa ofisini  kuna kesi zake kibao za wizi asububi akiwa na hizi  sare za shule kwa vile  haminiki kwa wizi katumia utapeli kampa mtoto mwingine mia 2 akamkodia baiskeli.

 

Alipokabidhiwa katokomea nayo toka asubuhi mpaka sahizi wamiliki wa baiskeli  walipoingia Mtaa kumsakana na kufanikiwa kumkamata Kichangani na kumleta hapa akiwa hana shati nikawaita wazazi wake baba yake kwa hasira alipofika hapa alimchapa pete mtoto kaluka juu alivyoanguka chini kapoteza fahamu muda huu  tumeita Bajaj tumkimbize hospital”alisema Mwenyekiti huyo.  

 

Baba wa Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Francis Edward baada ya tukio hilo anadaiwa kutoweka eneo hilo akihisi huenda amemuua mwanae kwa kichapo hicho.

 

Kwa upande wake Mama mzazi wa Mtoto huyo Bi Ferister Thomas aliyekuwepo eneo la tukio akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi huku akirekodiwa alikiri Mwanae huyo kuwa na tabia ya wizi.

 

“ Vitu viko wazi siwezi kumtete mwanangu kweli anatabia mbaya mfano asubuhi  kaaga  ana kwenda shule na sisi wazazi tunajua yuko shule, muda huu tunaitwa kwa mwenykiti tukielezwa kwamba anadaiwa kutapeli  baiskeli ya watu, siku za nyuma alifanya matukio ya kihalifu baba yake kapelekwa Polisi. hapa kwa mwenyekiti kila siku tunaitwa kwenye kesi zake.  

 

Kwa sasa nimechanganyikiwa nina kazi mbili za kumchunga huyu Mtoto na tabia zake mbaya  lakini pia kumchunga baba yake apunguze hasira unajua tena wakulia wanahasira kali asije akamdhuru  na yeya akaishia magereza nikakosa vyote”alisema mama huyo huku akiangua kilio kwa uchungu.

 

 Alipoulizwa ana watoto wangapi na alipo muwe wake kwa sasa baada ya tukio hilo alijibu.

 

” Nina watoto 4 na huyu Benja ndio wa kwanza, kuhusu alipo Mume wangu kwa sasa nahisi baada ya kumpiga teke mtoto wake na kupoteza famua ameogopa ameondoka  eneo hili  hakumpiga sana nahisi na njaa imechangia Benja kupoteza fahamu kwani toka asubuhi saa 12 alivyokunywa chai hajala chakula mpaka muda huu wa saa 9”alisema Mama Benja.

 

Siku iliyofuata Mwandishi wa habari hizi alitinga shule ya Msingi Mtawara ambapo Mwalimu wa darasa la Saba Diana Kanyamwaswa alipotakiwa kuelezea tabia na maendelea ya Mwanafunzi wake Benjamini Francis alisema.

 

” Mtoto huyo ni mtukutu sana pia ni mtoro anasiku mbili hajafika shuleni  nasikia jana kakamatwa huko Mitaani na baiskeli ya watu”alisema Mwalimu huyo.

 

Hadi tuna kwenda mitamboni juhudi za kumpata baba wa mtoto huyo ili azungumzie tukio hilo ziligonga mwamba kwani licha ya Mwandishi wa habari hizi kutinga nyumbani kwake zaidi ya mara 3 na mara ya mwisho ikiwa  juzi jumamosi  mzazi huyo  hakupatikana huku mkewe akidai mumewe baada ya tukio hilo siku iliyofuata  alisafiri kuelekea jijini Dar es salaam.

 

Alipoulizwa maendelea ya kiafya ya Benjani Bi Felister alisema kwa sasa anaendelea vizuri baada ya juzi kuruhusiwa kutoka hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alipolazwa kwa siku .kadhaa

             

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...