Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, January 28, 2025

HABARI KALI YA KITAA. STEND ILIYOJENGWA KWA MAMILION YA SHILINGI YAGEUZWA DAMPO LA TAKATAKA.





 

                

    Na Dustan Shekidele, Morogoro.

KAMA kawaida Kipengele Pendwa  cha habari kali ya kitaa kinaendelea Leo Jumanne kwenye Blog Pendwa ya www.shekideletz.blogspot.com.

Wiki iliyopita  Mwandishi wa habari hizi aliingia Mtaani kusaka habari hiyo kali na kushudia sehemu ya Stend Mpya ya Daladala iliyojengwa kwa Mamilioni ya Pesa miaka ya hivi karibuni ikigeuzwa Dampo la takataka.

Wakizungumzwa  na Mtandao huu baadhi ya wafanyabiashara wa Stend hiyo iliyopo Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, walisema

“Dampo hili limekuwa kero kufuatia taka hizi nyingi zikiwa ni mabaki ya vyakula vya mama Ntilie wa Stend hii zikitoa harufu kali kufuatia taka hizo kunyeshewa na mvua zinazoendelea”Alisema Ally Shabani ambaye ni derevawa boda boda wa eneo hilo.

Alioulizwa kawaida usafi unaanza kwa mwananchi mwenyewe kwa nini wao wasiwakamate na kuwashitaki kwa Afisa Afya wa Kata watu wanaotupa taka eneo hilo?

Alijibu” Kaka ofisi ya kata hiyo hapo na hafuru hii kali inafika ofisini kwao na wanaona kupitia  madirisha watu wakitupa taka  eneo hili  la kukaa abiria wakisuburi magari”alisema boda boda huyo kwa Jazba.

Naye Mzee lbrahimu Mangwende alisema” Huyo bibi Afya akikuta uchafua nyumbani kwako akukupiga faini juzi kuna huyo Mwarabu anayejenga hili Ghorofa wamempigia simu wakimtaka asafisha eneo lake vinginevyo watampeleka mahakamani sasa wao mbona eneo lao la Stend jirani na Ofisi yao ya kata kuna dampo la taka “alisema Mzee huyo na kuongeza

“ Huo ni uonezi kwa wananchi kesho nitakwenda kulalamika kwa mwenyekiti Chaballa”alisema Mzee Mangwenda ambaye mjukuu wake ni winhga hatari wa JKT Tanzania Shiza Kichuya

Kufuatia harufu kali Mwandishi wa Mtandao huu aliradhimika kwenda duka la dawa kununua Barakoa na kusogea kwenye Dampo hilo  kupiga picha.

 Baada ya kupiga picha Mwanahabri huyo alitinga Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Mji Mpya, alipofika aliwakuta watu 4  akiwemo Polisi mwenye cheo cha nyota moja begani na Afisa Mtendaji Kata Adrew  Tesha.

Baada ya  kujitambulisha na kuomba kuongea na Afisa Mtendao chaajabu mmoja wawatu hao alimuhoji Mwandishi huyo akisema”sisi sote ni viongozi wa kata huyo ni Askari Kata na sisi ni Maafisi wa tendaji  tuambie hiyo shida yako inahusu nini ili tukupatie muhusika”

Mwandishi akamwambia jamaa huyo kwamba anahitaji kuongea na Afisa Mtendaji wa Kata kuhusiana na mambo ya usafi.

Jamaa huyo aliyegoma kutaja jina lake alimuagiza Mwandishi huyo kuzungumza na Afisa Afya wa Kata ambaye  hukuwepo ndani ya ofisi hiyo.

Mtandao huu alimtwangia simu Afisa afya huyo Bi Jackline Manjenje  alipotakiwa kuelezea uwepo wa Dampo hilo alisema”Siwezi kujibu chochote mwenye jukumu la kujibu ni bosi wangu Afisa Mtendaji wa kata”

Mwandishi. Muda huu nimetoka ofisini na Afisa Mtendaji ameniambia nikuone wewe  Bibi Afya  kata.

Jackline . Hapana siwezi kuzungumza nenda kambane yeye akuambie.

Baada ya kuona watumishi hao wa kata wanakwepa. Mwandishi wa habari hizi alimtwangia simu Afisa habari wa Manispaa Bi Liliani Kazinja majibu yake haya hapa“

 Binafsi sina taarifa hizo muda huu naendesha nikishuka nampigia simu Afisa Afya wa Kata  then nitarudi kwako shekidele”.

Baada ya watumishi hao wa serikali kutupiana Mpira Mtandao huu ulimtafuta mwakilishi wawanchi Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa A ilipo Stend hiyo Bw Issa Kitukwa Maarufu lssa Chaballa ambapo alipoelewa na kuonyeshwa picha alisema.

“Hii sio sawa Shekidele ombi langu naomba nirushie hizo picha kesho nakwenda kwa mtendaji nikishindwa kupata majibu nakwenda Manispaa kwa Mkurugenzi nikiwa na ushahidi wa hizo picha”alisema Chaballa ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi kuu la Yanga mkoa wa Morogoro.

Tuesday, January 21, 2025

HAYA YANAYOENDELEA MATAWI YA SIMBA NA YANGA MORO SI UTANI WA JADI NI VITA.

Lundo la mashabiki wa Simba wakitoka tawi la Yanga wakiingia stend ya daladala ya Kaloleni

,,,,Mashabiki wa Simba akicheza ngoma kwenye nje ya tawi la Yanga

 Kiongozi wa tawi la Yanga Shabani Abdallah kushoto akimlalamikia kiongozi wa tawi la Simba Majutoa Abdallah


        Na Dustan Shekidele, Morogoro.

SIKU zote kazi za Mwandishi wa habari ni kuhabarisha kwenye maeneo ya Kuelemisha, Kukosoa, Kuburudisha na kushauri inapobidi kufanya hivyo kwa dhana ya kuendelea kulinda tunu yetu ya Amani kwenye Mitaa yetu, Kata,zetu  Wilaya, Mikoa na Taifa kwa ujumla.

Kwa alichokishuhudia Juzi Mwandishi wa habari hizi kwenye matawi Makuu ya Simba na Yanga, kinahatarisha Amani kwenye Mtaa wa Fumilwa ‘A’ Kata ya Mji Mpya Wilaya ya Morogoro  yalipo matawi hayo ambayo ukaribu wao unatenganishwa na nyumba tatu pekee.

 Hivyo Mwanahabari huyo anashauri Mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka za kuwakutanisha viongozi na matawi hayo kwa lengo la kurejesha Amani na upendo miongoni mwao,

Kwa sasa Viongozi na wanachama wa matawi hayo wamewekeana visasa vya  mapigana ya kuhatarisha Amani jambo ambalo alina afya kwenye mustakabri wa taifa letu.

      KWA NINI WAMEFIKA HAPO.

Juzi wananachama wa Simba kutoka tawi la Shujaa Ndugu wa Simba walikodi Kigoma Maarufu ‘Bad Party’wakafanya maandamani ambayo sina  hakika kama yanakibari cha Polisi au Mwenyekiti wa Mtaa.

Ifahamike Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Fumilwa A ni Issa Kitukwa Maarufu Chaballa ambaye pia ni Mwenyekiti wa tawi hilo la Yanga, hivyo sizani kama angekubali kutoa kibari kwa tawi la Simba kufanya Maandamano ya kwenda tawi la yanga kuwatania kwa kushinda kutoboa robo fainali.

 Tawi hilo la Shujaa Ndugu wa Simba walifanya maandamano Mara mbili awari waliandamana saa 8 wakikatiza tawi la Yanga na kuweka kambia kwa dakika kadhaa wakicheza na kuwaimbia nyimbo za kejeri watani zao hao.

Wakati hayo yakiendelea wanayanga waliokuwa na hasira ya kutolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabigwa Afrika,hawakuwafanya chochote badala yake waliweka ushahiri wa kuwarekodi kupitia simu zao.

Kama hiyo haitoshi Wana simba hao  majira ya saa 12 jioni baada ya gemu yao na CS Constantine kutamatika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-0 na kufanikiwa kuongoza kundi A, Wana Simba hao waliandamana tena  mitaa mbali mbali ya Mji Mpya wakikatiza  tawi la Yanga.

Akizungumza na Mtandao huu huku akirekodiwa kiongozi wa tawi la Yanga Shaban Abdallah Maarufu Shabani Yanga alisema.

”Wazee wa kung’oa viti wameendeleza uchokozi wao wamepita hapa kwetu mara mbili wametuchokoza sisi hatukuwajibu chochote mbaya zaidi hii mara ya pili baada ya kuona hatuwajibu  wameamua kurusha mawe kwenye tawi letu shekidele unajua ndani ya tawi letu kuna TV kubwa mbili kwa bahati mawe yale hayakufika kwenye Tv.” Alisema Shabani na kuongeza

“Kinara wa vulugu hizo ni Yule lssa mwenye ulemavu wa ngozi sisi tumekusanya ushahiri wa video lazima tulipe kisasa hata vitabu vya dini vinasema kulipa kisasi ni haki, yaani wakifungwa mechi yoyote sisi viongozi tunawatuma watu wetu waende pale kwao wakifanye kama  walivyofanya kwetu, baada ya kupigwa mawe mimi nimekwenda  kwenye tawi lao kumueleza kiongozi wao Majuto ambaye amedai hakuwatuma wafuasi wao kurusha mawe”alisema shabani ambaye kwenye tawi hilo ni ujumbe wa kamati ya utendaji

Ni kweli Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia Shabani Abdallah akimlalamikia Katibu wa Shujaa Majuto Abdallah kulia mwenye nguo nyekundu kinachoonekana mbele yao ni kituo cha Polisi Kata ya Mji Mpya.

Miaka 2 iliyopita Yanga baada ya kuifunga Simba Mashabiki wa Yanga walifanya maandamano kufurahia ushindi wao walikatiza tawi la pili la Simba Maarufu Shujaa Ngome Kuu lililopo Mji Mpya Sokoni baadhi ya mashabiki hao  walirusha mawe kwenye tawi hilo na kumasua usoni Mzee Mbonde aliyekuwa akiuza karanga ndani ya tawi hilo.

Monday, January 20, 2025

HUU KWELI NI UBAYA UBWELA, SIMBA MORO WAFANYA SHEREHE KUFURAHIA YANGA KUNG’OLEWA LIGI YA MABINGWA













 

.
                Na Dustan Shekidele,Morogoro. 
WANACHAMA wa Simba kutoka tawi la Shujaa ‘Ndugu wa Simba’lililopo Kata ya Mji Mpya Mkoani Morogoro jana mchana wamekodi ngoma na kufanya maandamano mitaa mbali mbali wakisheherekea watani zao Yanga kung’olewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi. 
 
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo kwenye maandamano hayo alishuhudia yakianzia tawi hilo na kukatiza tawi la Yanga lililopo jirani kabisa na tawi la Shujaa wakitenganiswa na nyumba tatu pekee. 
 
Baada ya kufika kwenye tawi la Yanga huku wakiwa na kapu lililoandikwa ‘Ubaya Ubwela walisimama kama dakika 4 wakicheza ngoma huku wakiimba wimbo wa kuwakejeri wenzao ‘Gusa achia turejee Jangwani’. 
 
Wakati hayo yakiendelea wanachama wa Yanga waliokuwa na hasira ya kuikosa robo fainali licha ya kuvamiwa eneo lao walionyesha ukomavu wa hali ya juu walikaa walikaa baada ya kuona hawajibiwi mashabiki hao wa Simba waliondoka zao.
 
Mwandishi wa Mtandao huu alimshuhudia mmoja wawanachama wa Yanga aliyefahamika kwa jina moja la Minziro akiwarekodi kupitia simu yake huku akisema.
 
”Nimerekodi kama ushahidi shekidele ni shahidi sisi tunamachungu ya kufungwa wamekuja hapa kwetu na kigoma chao wametuzihaki tumevumilia hatukuwafanyia fujo sasa ikifika zamu yao na sisi tutakwenda pale kwao wavumilia kama sisi tulivyovumilia wakirusha ngumi Polisi watakwenda wao ushahidi huu hapa nimesharekodi”alisema Minziro ambaye ni fundi baiskeri nje ya tawi hilo la Yanga. 
 
Kabla ya maandamano hayo kuanza majira ya saa 8 mchana Mwandishi wa habari hizi alizungumza na Katibu wa tawi la Shujaa Majuto Abdallah ambaye alipotakiwa kuelezea dhumuni la maandamano hayo alisema.
 
” Tumekodi Kigoma kusheherekea Yanga Kutolewa kwenye mashindano tunaandamana mitaa mbali mbali na maandamano haya yataishia hapa tawini saa 10 jioni tukishuhudia timu yetu ya simba kimfunga Mwarabu na kuongoza kundi”alisema Majuto. 
 
Baadae Mtandao huu ulishuhudia Uongozi wa Yanga ukiwa na hasira ukitinga tawi la Shujaa nini kilifanyika endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

Tuesday, January 14, 2025

HABARI KALI YA KITAA. MZUNGUKO WA BARABRA MSAMVU WATAJWA KUWA NAMBA MOJA TANZANIA. MENEJA TANROADS AKWEPA KUZUNGUMZA .



                

         Na   Dustan Shekidele,Morogoro.

KAMA Kawaida kipengele  Pendwa cha habari kali ya Kitaa kinaendelea leo Jumanne kwenye Blog Pendwa wa Shekidele.   [www.shekideletz.blogspot.com].

Wiki iliyopita Mwandishi wa Mtandao huu aliingia mtaani kusaka habari kali ya Kitaa na kushuhudia wananchi wakibishana kuhusiana na ukubwa wa mzunguka wa barabara wa Msamvu’ Round About.’

Kundi moja  walidaI Round About hiyo ni kubwa kuliko zote Tanzania  huku kundi la pili likipinga.

Kufuatia mvutano huo  Alhamis iliyopita Mwandishi wa habari hizi  alitinga Ofisi ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Eng. Razack Kiamba kwa lengo la kujua kama ni kweli mzunguko huo  ni mkubwa kuliko yote Tanzania au la.

Siku hiyo Meneja huyo hakuwepo ofisini Mwahabari huyo alireja siku iliyofuata pia hakumkuta, wasaidizi walipouliozwa walidai bosi wao yuko nje ya ofisi kikazi.

Baada ya maelezo hayo Siku hiyo hiyo ya ljumaa Mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti alimpigia simu Meneja huyo zaidi ya mara 5 hakupokea.

Jumamosi na Jumapili kwa sababu sio siku za kazi Mwandishi huyo hakuhangaika kumpigia, Jana jumatatu alimpigia tena kwa namba nyingine pia hakupokea licha ya kupigia zaidi ya mara 3.

Kufuatia hali hiyo Mwanahabari huyo aliamua kumtumia ujumbe[sms]kama inavyosomeka kwenye simu, Meneja huyo alijibu kwa mkato akito pole kwa Mwandishi huyo kwa kuhangaika kumtafuta.

Baada ya majibu hayo yenye ujazo hafifu wa herufi nne Mwanahabari huyo aliamua kumtwangia simu safari hii alipokea na kutoa majibu ya mkato yenye kinga ya kuulizwa swali akisema.

’ Niko barabarani naelekea nyumbani nikifika nitakupigia’ hii ilikuwa jana saa 9 Alasiri, baada ya jibu hilo lenye tumaini, Mwanahabari huyo alibeba kamera yake ya kisasa yenye uwezo wa kupiga picha za juu na chini hadi kwenye mzungu wa msamvu na kumpiga picha kama unavyoonekana.

Chaajabu mpaka leo muda huu wa saa 7 mchana Meneja huyo hajampigia simu Mwandishi huyo,huenda bado hajafika nyumbani wake au amefika  lakini kamua kupuzia kutoa habari kwa wananchi.

 Viongozi wetu wakuu  wa serikali akiwemo Mh Rais, Makamo wa Rais,Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu Mara nyingi walitoa  matamko ya kuwataka Viongozi wa chini yao kutoa habari kwa wananchi kwa wakati sambamba na kuwa jirani na wananchi.

lnashanganza kwa Eng Kiamba kukwepa kupokea simu za wananchi mfano landa daraja limekatika Mwananchi ameamua kutoa taarifa kwa Meneja anapigiwa hapokei simu.

Kitendo alichofanya cha kukwepa  kutoa habari kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro waliohitajio kujua kama kweli Mzunguko wao wa Msamvu ndio mkubwa Tanzania au La ni kuwanyima haki yako ya Msingi.

Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwa sababu aliyekabidhiwa jukumu la kutupa majibu  amekwepa basi tuendelee kuishi kwenye hizo tetesi za si mtofahamu kwamba Round Abound ya Msamvu ni kubwa kuliko zote au La.

Nakumbuka miaka miwili iliyopita  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro waliitisha kikao kazi kwa Waandishi wa habari na wadai wa habari Mkoa wa Morogoro.

Kikao hicho kilifanyika lkulu ndogo [ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro] baadhi ya wadai wa habari walialikwa ni Kamanda wa polisi Mkoa, kamanda wa TAKUKURU, Kamanda wa Zima Moto.

Kamanda wa Uhamiaji, Mkurugenzi wa Manispaa. Meneja wa Tanesco. Meneja wa MURUWASA. Meneja wa TANROADS na Mganga Mkuu wa Mkoa.

Moja ya angenda ya kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Mwandishi wa habari hizi ni kwamba wadau hao  walitakiwa kutoficha habari sambamba na kutoa habari kwa wakati.

Agenda nyingine muhumi ilikuwa ulinzi na usalma kwa waandishi wa habari  wanapokua kazi wakitekeleza majukumu yao mkoani Morogoro.


 

Saturday, January 11, 2025

LIGI DARAJA LA 4 MORO,DABI YA WAPALE YAVUTIA MASHABIKI.

                                   Vijana wa Kocha Mgonja
                Kocha Mgonja kulia akivutana na kocha Micho

                                ....Vijana wa Kocha Micho






 

                             Na Dustan Sherkidele, Morogoro.
LIGI daraja la Nne Wilaya ya Morogoro imeendelea jana uwanja wa Saba saba kwa mchezo wa Dabi ya makocha wapale kutoka Same Kilimanjaro, Kocha Juma Mgonja anayeifundisha Moro Youth and Childeny Academy yenye maskani yake Chamwino na Kocha Juma Athuman ‘Maarufu Ticha Micho’ anayekinoa kikosi cha Moro Soccer Academy kutoka Mwembesongo. 
 
Katika demu hiyo iliyotawaliwa na imani za kishirikina ilitamatika kwa timu hizo kutoka sare ya 0-0.
 
Katika hali ya kushangaza refa alipopuliza kipenga cha kuanzisha mpira Vijana wa Kocha Micho walibutua mpira Nje kwa makusudi ikidaiwa kuwa ni maelekezo ya Mganga. 
 
Kuoana hivyo Vijana wa Kocha Mgonja nao waliokota mpira huo na kuwarushia tena Vijana Micho hapo sasa ‘ball’ likapigwa.
 
Baada ya gemu hiyo kutamatika makocha hao walikumbatiana huku wakitaniana kwa Lugha ya Kipale baadae wakabadilisha steshen wakaingia Lugha ya Taifa ya Kiswahiri, kwa kocha Mgonja kumuambia Kocha Micho maneno haya.
 
“Mpira ni mazoezi sio uchawi umeanza mpira kwa kubutua nje, timu yangu haturogi tunamuamini Yesu .”
 
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kocha Mgonja alisema timu yake hiyo mpya inamilikiwa na mmoja makanisa yaliyopo kata ya Chamwingo. 
 
lkumbukwe kocha Mgonja kabla ya kutimkia timu hiyo alikuwa akikinoa kikosi cha Chamwino Ranger akiibua wachezaji wengi wanaochezaji Ligi mbali mbali Tanzania. 
 
Kwa upande wa kocha Micho pichani kulia mwenye umbo dogo lililopelekea mashabiki kumfananisha na kocha wa zamani wa Yanga Mzungu Micho, awari alikuwa Moro Kids kabla ya kujiengua kwenye taasisi hiyo na kuanzisha Academy yake hiyo.
 
Hali kadhari Ticha Micho kwenye kalia yake ya ukoa ameibua wachezaji wengi wanaotamba kwa sasa ligi kuu miongoni mwa wacheaji hao ni Hamad Waziri’Kuku’anayekipiga Singida Big Stars, Shiza Kichuya anayekipiga JKT Tanzania na Hassan Kessy Kidingile aliyewahi kuzitumikia Simba na Yanga hadi anafifia kisoka Kessy alikuwa akiitumikia Tabora United

UJUMBE WA NANE LA MUNGU USALAMA WA WATU WAMUNGU.

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa kwenye msitu Mnene Matombo Wilaya ya Morogoro Vijiji ........Mwandishi huyo akiwa Juu ya Milima ya Mgeta wila...