Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, January 14, 2025

HABARI KALI YA KITAA. MZUNGUKO WA BARABRA MSAMVU WATAJWA KUWA NAMBA MOJA TANZANIA. MENEJA TANROADS AKWEPA KUZUNGUMZA .



                

         Na   Dustan Shekidele,Morogoro.

KAMA Kawaida kipengele  Pendwa cha habari kali ya Kitaa kinaendelea leo Jumanne kwenye Blog Pendwa wa Shekidele.   [www.shekideletz.blogspot.com].

Wiki iliyopita Mwandishi wa Mtandao huu aliingia mtaani kusaka habari kali ya Kitaa na kushuhudia wananchi wakibishana kuhusiana na ukubwa wa mzunguka wa barabara wa Msamvu’ Round About.’

Kundi moja  walidaI Round About hiyo ni kubwa kuliko zote Tanzania  huku kundi la pili likipinga.

Kufuatia mvutano huo  Alhamis iliyopita Mwandishi wa habari hizi  alitinga Ofisi ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Eng. Razack Kiamba kwa lengo la kujua kama ni kweli mzunguko huo  ni mkubwa kuliko yote Tanzania au la.

Siku hiyo Meneja huyo hakuwepo ofisini Mwahabari huyo alireja siku iliyofuata pia hakumkuta, wasaidizi walipouliozwa walidai bosi wao yuko nje ya ofisi kikazi.

Baada ya maelezo hayo Siku hiyo hiyo ya ljumaa Mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti alimpigia simu Meneja huyo zaidi ya mara 5 hakupokea.

Jumamosi na Jumapili kwa sababu sio siku za kazi Mwandishi huyo hakuhangaika kumpigia, Jana jumatatu alimpigia tena kwa namba nyingine pia hakupokea licha ya kupigia zaidi ya mara 3.

Kufuatia hali hiyo Mwanahabari huyo aliamua kumtumia ujumbe[sms]kama inavyosomeka kwenye simu, Meneja huyo alijibu kwa mkato akito pole kwa Mwandishi huyo kwa kuhangaika kumtafuta.

Baada ya majibu hayo yenye ujazo hafifu wa herufi nne Mwanahabari huyo aliamua kumtwangia simu safari hii alipokea na kutoa majibu ya mkato yenye kinga ya kuulizwa swali akisema.

’ Niko barabarani naelekea nyumbani nikifika nitakupigia’ hii ilikuwa jana saa 9 Alasiri, baada ya jibu hilo lenye tumaini, Mwanahabari huyo alibeba kamera yake ya kisasa yenye uwezo wa kupiga picha za juu na chini hadi kwenye mzungu wa msamvu na kumpiga picha kama unavyoonekana.

Chaajabu mpaka leo muda huu wa saa 7 mchana Meneja huyo hajampigia simu Mwandishi huyo,huenda bado hajafika nyumbani wake au amefika  lakini kamua kupuzia kutoa habari kwa wananchi.

 Viongozi wetu wakuu  wa serikali akiwemo Mh Rais, Makamo wa Rais,Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu Mara nyingi walitoa  matamko ya kuwataka Viongozi wa chini yao kutoa habari kwa wananchi kwa wakati sambamba na kuwa jirani na wananchi.

lnashanganza kwa Eng Kiamba kukwepa kupokea simu za wananchi mfano landa daraja limekatika Mwananchi ameamua kutoa taarifa kwa Meneja anapigiwa hapokei simu.

Kitendo alichofanya cha kukwepa  kutoa habari kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro waliohitajio kujua kama kweli Mzunguko wao wa Msamvu ndio mkubwa Tanzania au La ni kuwanyima haki yako ya Msingi.

Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwa sababu aliyekabidhiwa jukumu la kutupa majibu  amekwepa basi tuendelee kuishi kwenye hizo tetesi za si mtofahamu kwamba Round Abound ya Msamvu ni kubwa kuliko zote au La.

Nakumbuka miaka miwili iliyopita  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro waliitisha kikao kazi kwa Waandishi wa habari na wadai wa habari Mkoa wa Morogoro.

Kikao hicho kilifanyika lkulu ndogo [ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro] baadhi ya wadai wa habari walialikwa ni Kamanda wa polisi Mkoa, kamanda wa TAKUKURU, Kamanda wa Zima Moto.

Kamanda wa Uhamiaji, Mkurugenzi wa Manispaa. Meneja wa Tanesco. Meneja wa MURUWASA. Meneja wa TANROADS na Mganga Mkuu wa Mkoa.

Moja ya angenda ya kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Mwandishi wa habari hizi ni kwamba wadau hao  walitakiwa kutoficha habari sambamba na kutoa habari kwa wakati.

Agenda nyingine muhumi ilikuwa ulinzi na usalma kwa waandishi wa habari  wanapokua kazi wakitekeleza majukumu yao mkoani Morogoro.


 

No comments:

Post a Comment

LIGI YA MABIGWA BARA LA ULAYA.ARSENAL AMFANYIA KITU MBAYA BINGWA MTETEZI

              Na Dustan Shekidele. WASHIKA Bunduki wa Jiji la Maraha la London nchini England Arsenal   usiku wa leo imeishangaza duni...