Kocha Mgonja kulia akivutana na kocha Micho
....Vijana wa Kocha Micho
Na Dustan Sherkidele, Morogoro.
LIGI daraja la Nne Wilaya ya Morogoro imeendelea jana uwanja wa Saba saba kwa mchezo wa Dabi ya makocha wapale kutoka Same Kilimanjaro, Kocha Juma Mgonja anayeifundisha Moro Youth and Childeny Academy yenye maskani yake Chamwino na Kocha Juma Athuman ‘Maarufu Ticha Micho’ anayekinoa kikosi cha Moro Soccer Academy kutoka Mwembesongo.
Katika demu hiyo iliyotawaliwa na imani za kishirikina ilitamatika kwa timu hizo kutoka sare ya 0-0.
Katika hali ya kushangaza refa alipopuliza kipenga cha kuanzisha mpira Vijana wa Kocha Micho walibutua mpira Nje kwa makusudi ikidaiwa kuwa ni maelekezo ya Mganga.
Kuoana hivyo Vijana wa Kocha Mgonja nao waliokota mpira huo na kuwarushia tena Vijana Micho hapo sasa ‘ball’ likapigwa.
Baada ya gemu hiyo kutamatika makocha hao walikumbatiana huku wakitaniana kwa Lugha ya Kipale baadae wakabadilisha steshen wakaingia Lugha ya Taifa ya Kiswahiri, kwa kocha Mgonja kumuambia Kocha Micho maneno haya.
“Mpira ni mazoezi sio uchawi umeanza mpira kwa kubutua nje, timu yangu haturogi tunamuamini Yesu .”
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kocha Mgonja alisema timu yake hiyo mpya inamilikiwa na mmoja makanisa yaliyopo kata ya Chamwingo.
lkumbukwe kocha Mgonja kabla ya kutimkia timu hiyo alikuwa akikinoa kikosi cha Chamwino Ranger akiibua wachezaji wengi wanaochezaji Ligi mbali mbali Tanzania.
Kwa upande wa kocha Micho pichani kulia mwenye umbo dogo lililopelekea mashabiki kumfananisha na kocha wa zamani wa Yanga Mzungu Micho, awari alikuwa Moro Kids kabla ya kujiengua kwenye taasisi hiyo na kuanzisha Academy yake hiyo.
Hali kadhari Ticha Micho kwenye kalia yake ya ukoa ameibua wachezaji wengi wanaotamba kwa sasa ligi kuu miongoni mwa wacheaji hao ni Hamad Waziri’Kuku’anayekipiga Singida Big Stars, Shiza Kichuya anayekipiga JKT Tanzania na Hassan Kessy Kidingile aliyewahi kuzitumikia Simba na Yanga hadi anafifia kisoka Kessy alikuwa akiitumikia Tabora United
No comments:
Post a Comment