Kiongozi wa tawi la Yanga Shabani Abdallah kushoto akimlalamikia kiongozi wa tawi la Simba Majutoa Abdallah
Na Dustan Shekidele, Morogoro.
SIKU zote kazi za Mwandishi wa habari ni kuhabarisha kwenye maeneo ya Kuelemisha, Kukosoa, Kuburudisha na kushauri inapobidi kufanya hivyo kwa dhana ya kuendelea kulinda tunu yetu ya Amani kwenye Mitaa yetu, Kata,zetu Wilaya, Mikoa na Taifa kwa ujumla.
Kwa alichokishuhudia Juzi Mwandishi wa habari hizi kwenye matawi Makuu ya Simba na Yanga, kinahatarisha Amani kwenye Mtaa wa Fumilwa ‘A’ Kata ya Mji Mpya Wilaya ya Morogoro yalipo matawi hayo ambayo ukaribu wao unatenganishwa na nyumba tatu pekee.
Hivyo Mwanahabari huyo anashauri Mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka za kuwakutanisha viongozi na matawi hayo kwa lengo la kurejesha Amani na upendo miongoni mwao,
Kwa sasa Viongozi na wanachama wa matawi hayo wamewekeana visasa vya mapigana ya kuhatarisha Amani jambo ambalo alina afya kwenye mustakabri wa taifa letu.
KWA NINI WAMEFIKA HAPO.
Juzi wananachama wa Simba kutoka tawi la Shujaa Ndugu wa Simba walikodi Kigoma Maarufu ‘Bad Party’wakafanya maandamani ambayo sina hakika kama yanakibari cha Polisi au Mwenyekiti wa Mtaa.
Ifahamike Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Fumilwa A ni Issa Kitukwa Maarufu Chaballa ambaye pia ni Mwenyekiti wa tawi hilo la Yanga, hivyo sizani kama angekubali kutoa kibari kwa tawi la Simba kufanya Maandamano ya kwenda tawi la yanga kuwatania kwa kushinda kutoboa robo fainali.
Tawi hilo la Shujaa Ndugu wa Simba walifanya maandamano Mara mbili awari waliandamana saa 8 wakikatiza tawi la Yanga na kuweka kambia kwa dakika kadhaa wakicheza na kuwaimbia nyimbo za kejeri watani zao hao.
Wakati hayo yakiendelea wanayanga waliokuwa na hasira ya kutolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabigwa Afrika,hawakuwafanya chochote badala yake waliweka ushahiri wa kuwarekodi kupitia simu zao.
Kama hiyo haitoshi Wana simba hao majira ya saa 12 jioni baada ya gemu yao na CS Constantine kutamatika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-0 na kufanikiwa kuongoza kundi A, Wana Simba hao waliandamana tena mitaa mbali mbali ya Mji Mpya wakikatiza tawi la Yanga.
Akizungumza na Mtandao huu huku akirekodiwa kiongozi wa tawi la Yanga Shaban Abdallah Maarufu Shabani Yanga alisema.
”Wazee wa kung’oa viti wameendeleza uchokozi wao wamepita hapa kwetu mara mbili wametuchokoza sisi hatukuwajibu chochote mbaya zaidi hii mara ya pili baada ya kuona hatuwajibu wameamua kurusha mawe kwenye tawi letu shekidele unajua ndani ya tawi letu kuna TV kubwa mbili kwa bahati mawe yale hayakufika kwenye Tv.” Alisema Shabani na kuongeza
“Kinara wa vulugu hizo ni Yule lssa mwenye ulemavu wa ngozi sisi tumekusanya ushahiri wa video lazima tulipe kisasa hata vitabu vya dini vinasema kulipa kisasi ni haki, yaani wakifungwa mechi yoyote sisi viongozi tunawatuma watu wetu waende pale kwao wakifanye kama walivyofanya kwetu, baada ya kupigwa mawe mimi nimekwenda kwenye tawi lao kumueleza kiongozi wao Majuto ambaye amedai hakuwatuma wafuasi wao kurusha mawe”alisema shabani ambaye kwenye tawi hilo ni ujumbe wa kamati ya utendaji
Ni kweli Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia Shabani Abdallah akimlalamikia Katibu wa Shujaa Majuto Abdallah kulia mwenye nguo nyekundu kinachoonekana mbele yao ni kituo cha Polisi Kata ya Mji Mpya.
Miaka 2 iliyopita Yanga baada ya kuifunga Simba Mashabiki wa Yanga walifanya maandamano kufurahia ushindi wao walikatiza tawi la pili la Simba Maarufu Shujaa Ngome Kuu lililopo Mji Mpya Sokoni baadhi ya mashabiki hao walirusha mawe kwenye tawi hilo na kumasua usoni Mzee Mbonde aliyekuwa akiuza karanga ndani ya tawi hilo.
No comments:
Post a Comment