Na Dustan Shekidele, Morogoro.
KAMA kawaida Kipengele Pendwa cha habari kali ya kitaa kinaendelea Leo Jumanne kwenye Blog Pendwa ya www.shekideletz.blogspot.com.
Wiki iliyopita Mwandishi wa habari hizi aliingia Mtaani kusaka habari hiyo kali na kushudia sehemu ya Stend Mpya ya Daladala iliyojengwa kwa Mamilioni ya Pesa miaka ya hivi karibuni ikigeuzwa Dampo la takataka.
Wakizungumzwa na Mtandao huu baadhi ya wafanyabiashara wa Stend hiyo iliyopo Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, walisema
“Dampo hili limekuwa kero kufuatia taka hizi nyingi zikiwa ni mabaki ya vyakula vya mama Ntilie wa Stend hii zikitoa harufu kali kufuatia taka hizo kunyeshewa na mvua zinazoendelea”Alisema Ally Shabani ambaye ni derevawa boda boda wa eneo hilo.
Alioulizwa kawaida usafi unaanza kwa mwananchi mwenyewe kwa nini wao wasiwakamate na kuwashitaki kwa Afisa Afya wa Kata watu wanaotupa taka eneo hilo?
Alijibu” Kaka ofisi ya kata hiyo hapo na hafuru hii kali inafika ofisini kwao na wanaona kupitia madirisha watu wakitupa taka eneo hili la kukaa abiria wakisuburi magari”alisema boda boda huyo kwa Jazba.
Naye Mzee lbrahimu Mangwende alisema” Huyo bibi Afya akikuta uchafua nyumbani kwako akukupiga faini juzi kuna huyo Mwarabu anayejenga hili Ghorofa wamempigia simu wakimtaka asafisha eneo lake vinginevyo watampeleka mahakamani sasa wao mbona eneo lao la Stend jirani na Ofisi yao ya kata kuna dampo la taka “alisema Mzee huyo na kuongeza
“ Huo ni uonezi kwa wananchi kesho nitakwenda kulalamika kwa mwenyekiti Chaballa”alisema Mzee Mangwenda ambaye mjukuu wake ni winhga hatari wa JKT Tanzania Shiza Kichuya
Kufuatia harufu kali Mwandishi wa Mtandao huu aliradhimika kwenda duka la dawa kununua Barakoa na kusogea kwenye Dampo hilo kupiga picha.
Baada ya kupiga picha Mwanahabri huyo alitinga Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Mji Mpya, alipofika aliwakuta watu 4 akiwemo Polisi mwenye cheo cha nyota moja begani na Afisa Mtendaji Kata Adrew Tesha.
Baada ya kujitambulisha na kuomba kuongea na Afisa Mtendao chaajabu mmoja wawatu hao alimuhoji Mwandishi huyo akisema”sisi sote ni viongozi wa kata huyo ni Askari Kata na sisi ni Maafisi wa tendaji tuambie hiyo shida yako inahusu nini ili tukupatie muhusika”
Mwandishi akamwambia jamaa huyo kwamba anahitaji kuongea na Afisa Mtendaji wa Kata kuhusiana na mambo ya usafi.
Jamaa huyo aliyegoma kutaja jina lake alimuagiza Mwandishi huyo kuzungumza na Afisa Afya wa Kata ambaye hukuwepo ndani ya ofisi hiyo.
Mtandao huu alimtwangia simu Afisa afya huyo Bi Jackline Manjenje alipotakiwa kuelezea uwepo wa Dampo hilo alisema”Siwezi kujibu chochote mwenye jukumu la kujibu ni bosi wangu Afisa Mtendaji wa kata”
Mwandishi. Muda huu nimetoka ofisini na Afisa Mtendaji ameniambia nikuone wewe Bibi Afya kata.
Jackline . Hapana siwezi kuzungumza nenda kambane yeye akuambie.
Baada ya kuona watumishi hao wa kata wanakwepa. Mwandishi wa habari hizi alimtwangia simu Afisa habari wa Manispaa Bi Liliani Kazinja majibu yake haya hapa“
Binafsi sina taarifa hizo muda huu naendesha nikishuka nampigia simu Afisa Afya wa Kata then nitarudi kwako shekidele”.
Baada ya watumishi hao wa serikali kutupiana Mpira Mtandao huu ulimtafuta mwakilishi wawanchi Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa A ilipo Stend hiyo Bw Issa Kitukwa Maarufu lssa Chaballa ambapo alipoelewa na kuonyeshwa picha alisema.
“Hii sio sawa Shekidele ombi langu naomba nirushie hizo picha kesho nakwenda kwa mtendaji nikishindwa kupata majibu nakwenda Manispaa kwa Mkurugenzi nikiwa na ushahidi wa hizo picha”alisema Chaballa ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi kuu la Yanga mkoa wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment