.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WANACHAMA wa Simba kutoka tawi la Shujaa ‘Ndugu wa Simba’lililopo Kata ya Mji Mpya Mkoani Morogoro jana mchana wamekodi ngoma na kufanya maandamano mitaa mbali mbali wakisheherekea watani zao Yanga kung’olewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi.
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo kwenye maandamano hayo alishuhudia yakianzia tawi hilo na kukatiza tawi la Yanga lililopo jirani kabisa na tawi la Shujaa wakitenganiswa na nyumba tatu pekee.
Baada ya kufika kwenye tawi la Yanga huku wakiwa na kapu lililoandikwa ‘Ubaya Ubwela walisimama kama dakika 4 wakicheza ngoma huku wakiimba wimbo wa kuwakejeri wenzao ‘Gusa achia turejee Jangwani’.
Wakati hayo yakiendelea wanachama wa Yanga waliokuwa na hasira ya kuikosa robo fainali licha ya kuvamiwa eneo lao walionyesha ukomavu wa hali ya juu walikaa walikaa baada ya kuona hawajibiwi mashabiki hao wa Simba waliondoka zao.
Mwandishi wa Mtandao huu alimshuhudia mmoja wawanachama wa Yanga aliyefahamika kwa jina moja la Minziro akiwarekodi kupitia simu yake huku akisema.
”Nimerekodi kama ushahidi shekidele ni shahidi sisi tunamachungu ya kufungwa wamekuja hapa kwetu na kigoma chao wametuzihaki tumevumilia hatukuwafanyia fujo sasa ikifika zamu yao na sisi tutakwenda pale kwao wavumilia kama sisi tulivyovumilia wakirusha ngumi Polisi watakwenda wao ushahidi huu hapa nimesharekodi”alisema Minziro ambaye ni fundi baiskeri nje ya tawi hilo la Yanga.
Kabla ya maandamano hayo kuanza majira ya saa 8 mchana Mwandishi wa habari hizi alizungumza na Katibu wa tawi la Shujaa Majuto Abdallah ambaye alipotakiwa kuelezea dhumuni la maandamano hayo alisema.
” Tumekodi Kigoma kusheherekea Yanga Kutolewa kwenye mashindano tunaandamana mitaa mbali mbali na maandamano haya yataishia hapa tawini saa 10 jioni tukishuhudia timu yetu ya simba kimfunga Mwarabu na kuongoza kundi”alisema Majuto.
Baadae Mtandao huu ulishuhudia Uongozi wa Yanga ukiwa na hasira ukitinga tawi la Shujaa nini kilifanyika endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment